Rafiki yangu mpendwa,
Watu wanaotaka sana kufanikiwa lakini hawafanikiwi huwa hawakosi sababu na visingizio mbalimbali.

Wataeleza jinsi walivyotokea kwenye hali ngumu.
Wataeleza jinsi serikali ilivyo kikwazo kwao kufanikiwa.
Wataonyesha jinsi hali ya uchumi ilivyo mbaya na kuwazuia kufanikiwa.
Watakuwa na kila aina ya ushahidi kwa nini hawajafanikiwa.

Lakini hiyo yote ni kujifurahisha tu na kutokutaka kuukabili ukweli ambao upo mbele yao.
Kwa sababu katika mazingira hayo hayo wanayotumia kama sababu ya wao kushindwa, kuna wengine wengi ambao wameweza kufanikiwa.

Hivyo tatizo halianzii nje kwenye mazingira, uchumi au serikali, bali tatizo linaanzia ndani ya mtu mwenyewe.

Hii ni kusema kwamba kama hujafika kule unakotaka kufika, kinachokuzuia hakitoki nje, bali kipo ndani yako mwenyewe.

Na baada ya kutafiti kwa muda mrefu, kwamba kwa nini kwenye kazi au biashara ya aina moja kuna ambao wanafanikiwa na wanaoshindwa, nimekutana na jibu moja ambalo limenishangaza sana.

Jibu hilo ni msimamo.
Wanaofanikiwa wana msimamo mkubwa kwenye mambo yaliyo muhimu. Wakipanga wanafanya na hawaachi mpaka watakapopata wanachotaka.  Hata wakutane na magumu kiasi gani, wao huendelea na kile walichopanga, na hilo huwapa mafanikio makubwa.

Wanaoshindwa huwa hawana msimamo kwenye yale wanayofanya.
Wanaweza kupata wazo zuri, wakaweka mipango mikubwa na kuanza kulifanyia kazi. Lakini pale wanapokutana na magumu na changamoto, wanakata tamaa, hawaendelei tena.
Badala yake wanaenda kuanza kitu kingine kipya, huko nako mambo yanaendelea kuwa hivyo hivyo.
Ndani ya muda mfupi wanajikuta wamejaribu mambo mengi tofauti tofauti na hakuna hata moja ambalo wamefanikiwa.

Baada ya kuona msimamo ni kikwazo kikubwa kwenye mafanikio, tumetengeneza msimamo muhimu ambao wanajamii wa KISIMA CHA MAARIFA wanaufuata na kuusimamia kwenye kila siku ya maisha yao.
Kwa msimamo huo, wanakuwa na uhakika wa kufanya makubwa na kufanikiwa sana.

Kama umesahau au hujapata taarifa, KISIMA CHA MAARIFA ni jamii ya tofauti na ya kipekee kabisa ambayo ina watu wenye kiu ya mafanikio makubwa, wanaojifunza na kuiishi misingi sahihi, wanaoshirikiana na kutoa thamani kubwa kwa wengine.

Msimamo mkuu wa mafanikio uliopo kwenye KISIMA CHA MAARIFA una vipengele vikubwa vitatu;

Kipengele cha kwanza ni KAZI.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA kazi ndiyo rafiki wetu wa kweli, rafiki ambaye hawezi kutusaliti wala kutuonea wivu. Rafiki ambaye ukimpa umakini na yeye anakupa umakini mkubwa.
Tunaipa kazi kipaumbele kikubwa kwa sababu tunajua ni kupitia kazi ndiyo tunaweza kupata chochote tunachotaka.
Wakati wengine wakitafuta njia za mkato za kukwepa kazi, sisi tunaikaribisha kazi, tunaifanya kwa umakini na viwango vya juu na kupata matokeo bora.
Kwa kuweka msimamo kwenye kazi, unajijengea sifa nzuri, unazalisha thamani kubwa na kupata matokeo makubwa.

Kipengele cha pili ni UPENDO.
Kama unakumbuka kwenye IMANI kuu ya KISIMA CHA MAARIFA ambayo nilikushirikisha, ni UPENDO.
Na huu pia ndiyo msimamo wetu wa kila siku, kuanzia kwenye maisha yetu binafsi mpaka kwenye yale tunayofanya.
Tunajipenda na kujikubali sisi wenyewe, hivyo tunajithamini na kujiheshimu, tunajitambua na kutumia uwezo mkubwa ulio ndani yetu.
Tunawapenda na kuwakubali wengine jinsi walivyo, hivyo hatuhangaiki kuwabadili ili wawe kama tunavyotaka sisi.
Na tunapenda sana kile tunachofanya na hivyo hakiwi kazi kwetu, bali mchezo. Tunakifanya kwa viwango vya juu kabisa kwa sababu ni sehemu yetu.
Kwa msimamo wa upendo, hofu na chuki havipati nafasi na nguvu yetu yote inakwenda kwenye mambo sahihi.

Kipengele cha tatu ni HUDUMA.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tunayafanya maisha yetu kuwa huduma kwa wengine.
Kwa jinsi tunavyoishi na kwa kila tunachofanya, tunakuwa huduma kwa watu wengine.
Tunafanya yale tu yenye manufaa kwa watu wengine.
Hatufanyi chochote chenye madhara kwa watu wengine.
Tunajua kwa kuweka maslahi ya wengine mbele, maslahi yetu yatatimia pia.
Kwa msimamo wa huduma, tunagusa kila maisha tunayokutana nayo na kuacha alama nzuri zaidi.

Je ungependa kuwa kwenye jamii hii ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kuishi kwa msimamo huu kila siku na mafanikio yawe uhakika kwako?
Una bahati ya kipekee leo, kwani kuna nafasi chache kwa siku hizi chache kuweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Wasiliana sasa na 0717 396 253 ili kuweza kupata nafasi ya kuwa mmoja wa wanajamii wa KISIMA CHA MAARIFA.
Kumbuka nafasi ni chache sana na mwisho wa kupata nafasi hiyo ni tarehe 30/10/2021, hivyo kuna siku nne pekee.
Chukua hatua sasa ili uwe kwenye jamii inayokupa msukumo wa kufanya makubwa na kufanikiwa zaidi.

Pia kama bado hujapata kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO hakikisha unajipatia nakala yako sasa.
Kwani ndani ya kitabu hiki utajifunza sheria 100 za kuishi kila siku ili uwe na maisha ya mafanikio.
Ni sheria ndogo ndogo ambazo kwa sasa unazivunja bila ya kujua ni kikwazo kwako.
Kwa kuzijua sheria hizo na kuziheshimu, utashangaa jinsi maisha yako yatakavyoanza kubadilika yenyewe.
Kupata kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO wasiliana na 0752 977 170 leo na utatumiwa au kuletewa popote ulipo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.