Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya sababu kubwa inayopelekea watu wengi kutokufanikiwa ni kuhangaika na njia za mkato za kufika kwenye mafanikio na yatakayodumu.

Kila mara huwa wanajitokeza watu ambao wanakuja na njia za mkato za kufika kwenye mafanikio.
Watu hao huwa na ushawishi mkubwa na kuonyesha kabisa mifano ya waliofanikiwa kwa njia hizo.

Lakini kila anayejaribu njia hizo za mkato za kufika kwenye mafanikio, hakuna anachofanikiwa zaidi ya kupoteza muda na fedha.

Rafiki, inapokuja kwenye mafanikio, njia za mkato ndiyo njia ndefu kuliko nyingine zozote. Kwa sababu ni njia ambazo huwa hazifanyi kazi kabisa, hivyo kuzitumia ni kupoteza bure muda na nguvu zako.

Mafanikio makubwa yanahitaji muda kuyajenga vizuri na yaweze kudumu.
Hakuna mafanikio yanayopatikana haraka na yakadumu kwa muda mrefu.
Mifano tunayo mingi ya waliowahi kushinda bahati nasibu au kupata fedha nyingi kwa wakati mmoja, waliishia kupoteza zote kwa kipindi kifupi.

Lakini pia ipo dhahiri kwenye asili, angalia mchicha na mbuyu. Mchicha unaota haraka lakini pia unazeeka na kufa haraka. Mbuyu unaota taratibu lakini unadumu kwa muda mrefu.

Rafiki, inapokuja kwenye mafanikio, yanayodumu ni yale yanayojengwa taratibu na kwa muda mrefu. Hayo ndiyo yanakuwa na mizizi imara ya kuyawezesha kudumu kwa muda mrefu.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 tukifanya mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu John Magori kwenye safari yake ya miaka 10 kwenye biashara. Ameweza kuanzia chini kabisa mpaka kufika juu kwa kujipa muda wa kujenga kitu imara na kinachodumu. Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA uweze kujenga mafanikio yako kwa muda sahihi.

Je muda sahihi wa kujenga mafanikio makubwa na yatakayodumu ni upi?
Tafiti nyingi ambazo zimefanywa kwenye eneo la mafanikio na ubobezi linaonyesha kwamba inahitajika angalau miaka 10 ya kujenga mafanikio makubwa na ambayo yatadumu kwa muda mrefu.

Hivyo miaka kumi ndiyo kiwango cha chini kabisa cha muda ambao mtu unahitaji ili kuweza kujenga mafanikio makubwa na yatakayodumu.
Chochote unachofanya, unapaswa kujiona ukiwa unakifanya kwa miaka kumi mbele ndiyo ujenge mafanikio makubwa.

Chini ya muda huo ni kujidanganya tu, utahangaika na mengi lakini hutaweza kujenga mafanikio makubwa na yatakayodumu.

Unawezaje kufanyia kazi mafanikio kwa miaka 10?
Rafiki, najua ukiisikia miaka 10 unaona ni mingi sana, hivyo kujenga mafanikio kwa kipindi hicho unaona ni kuchelewa.
Lakini nikuhakikishie hakuna kuchelewa kokote. Miaka kumi ni mingi ukiiangalia kwa mbele, lakini ukiangalia kwa nyuma, inaonekana michache.

Kuonyesha jinsi miaka kumi isivyokuwa mingi huwa napenda kutumia chaguzi zinazofanyika. Unaweza kuona wazi kwamba Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alishakuwa raisi kwa miaka 10. Kama una kumbukumbu akiwa anaingia na kutoka madarakani, unaweza kuona ni kama juzi tu.

Lakini naelewa, ukiwa peke yako ambaye unaiangalia miaka kumi huku wanaokuzunguka wanaangalia mwezi ujao inakuwa ngumu sana.
Na hapa ndipo ninapotaka kukupa fursa ya kipekee sana.
Fursa ya kuwa kwenye jamii ya kipekee ambayo inajenga mafanikio makubwa kwa muda sahihi na ushirikiano mkubwa.

Jamii hiyo ni KISIMA CHA MAARIFA, ambayo inajengwa na watu wenye kiu ya mafanikio makubwa.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA kwa sasa kila mmoja anafanyia kazi malengo yake ya mafanikio makubwa kwenye muongo wa 2020 – 2030.

Huu ni muongo ambao pamoja na mambo mengine, kila mmoja anapambana kufikia uhuru wa kifedha. Yaani kuweza kuwa na akiba, uwekezaji na kipato cha kutosha kuendesha maisha bila kulazimika kufanya kazi moja kwa moja.

Je wewe hupendi kujenga mafanikio ya aina hii?
Hupendi kufika kwenye uhuru wa kifedha ili maisha yako yawe huru?
Hutaki kujenga mafanikio ambayo yatadumu kwa muda mrefu?
Najua unataka yote hayo, lakini unajichelewesha kwa sababu hujawa sehemu sahihi.

Acha sasa kujichelewesha na njoo ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kuna nafasi chache ndani ya muda mfupi za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa siku chache kabla ya mwezi oktoba 2021 kuisha, una fursa ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili uwe mahali sahihi.
Baada ya hapo dirisha la kujiunga litafungwa mpaka tena kipindi kingine.
Ndiyo kwanza tupo mwanzo wa muongo wetu wa kufanya makubwa.
Karibu ujiunge nasi sasa ili uache kupoteza muda kwa kuhangaika na mambo yasiyo sahihi.

Kwa vyovyote vile, miaka 10 itapita. Siku siyo nyingi utashangaa mwaka 2030 huu hapa. Na kama utakuwa umejaliwa kuwa hai, hakuna kitu ambacho utajutia kama kutokuchukua hatua sahihi sasa.
Una fursa ya kuungana na watu sahihi na kuwa kwenye njia sahihi.
Karibu sasa ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kuwasiliana na namba 0717 396 253 leo hii ili usikose nafasi.
Zimebaki siku tatu tu kupata nafasi hii, chukua hatua sasa.

Pia hakikisha unapata na kusoma kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO ambapo ndani yake unajifunza kanuni sahihi za kujenga mafanikio ya uhakika na yanayodumu.
Kwa kuwa na mwongozo huo, kamwe huwezi kutapeliwa au kusumbuliwa na yeyote kwenye safari yako ya mafanikio.
Kwa sababu utakuwa unajua yale yaliyo sahihi kufanya na yasiyo sahihi.
Jipatie nakala yako ya kitabu leo kwa kuwasiliana na 0752 977 170 na utatumiwa au kuletewa kitabu ulipo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.