Rafiki yangu mpendwa,
Inapokuja kwenye fedha, changamoto zimekuwa ni nyingi sana kwa walio wengi.

Mtu anaweza kujiwekea lengo la kuongeza kipato chake, analifanyia kazi kweli lengo hilo na kipato kinaongezeka.
Lakini sasa cha kushangaza ni hakuna tofauti yoyote ambayo mtu anaiona kwenye kipato hicho.
Licha ya kipato kuwa kimeongezeka, bado hazioni fedha ambazo zimeongezeka.

Na hilo limekuwa linatokana na tabia moja kubwa ya fedha. Tabia hiyo ni kadiri kipato kinavyoongezeka, ndivyo pia matumizi nayo yanaongezeka.
Hii ndiyo imekuwa inasababisha mtu asione mabadiliko ya kifedha licha ya kipato kuongezeka, kwa sababu chote kinamezwa na matumizi.

Ili kuondokana na changamoto hii, kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA tumeacha kuweka malengo ya ongezeko la kipato.
Badala yake tunaweka malengo ya ongezeko la utajiri.

Mchakato wa kuweka lengo la ongezeko la utajiri.
1. Unakokotoa thamani ya utajiri (net worth) ambao unao kwa mwaka unaomaliza.
2. Kukokotoa thamani hiyo unajumlisha thamami ya mali zote unazomiliki na kutoa thamani ya madeni yote unayodaiwa.
3. Kwa mali unazomiliki, thaminisha kwa bei ya soko kwa wakati husika. Yaani kama ingekuwa unauza kwa wakati huo, ungeuza kwa kiasi gani?
4. Baada ya kupata jibu, hapo ndipo ulipo kwa mwaka ambao unaumaliza.
5. Hatua inayofuata ni kuweka lengo la utajiri kwa mwaka unaofuata, ambalo ni mara mbili ya thamani uliyonayo sasa.

Hilo ndiyo lengo jipya ambalo unakuwa unalifanyia kazi.
Najua una maswali mengi kwenye hili, usihofu, unakwenda kupata majibu yote.

Swali la kwanza ni kwa nini mara mbili?
Jibu ni kwa sababu unahitaji namba ambayo unaifanyia kazi kwenye lengo, namba ya uhakika.
Na mara mbili ya kile ulichonacho sasa ni namba nzuri ya kuanzia.
Ni namba ambayo ipo ndani ya uwezo wa mtu kufanyia kazi na akaifikia.

Swali la pili ni namna gani mtu unaweza kufikia utajiri mara mbili ya ulionao kwa mwaka mmoja.
Jibu ni kwa kufanya mara mbili ya chochote ambacho umekuwa unafanya.
Kwenye biashara ongeza wateja mara mbili, ongeza mauzo mara mbili,  ongeza bidhaa na thamani mara mbili.
Kwa kuwa kuna kitu umekuwa unafanya kikakupa utajiri ulionao sasa (hata kama ni mdogo) kifanye kitu hicho hicho mara mbili ili kukuza zaidi utajiri wako.

Swali la tatu ni vipi kama umejenga utajiri ulionao kwa miaka mingi, unawezaje kuzidisha mara mbili?
Jibu ni zoezi hili la kuzidisha mara mbili lengo lake kubwa ni kuzifungua fikra zako zifikiri kwa ukubwa zaidi.
Kwa miaka mingi umekuwa unafikiri kwa hatua ndogo, ndiyo maana umekuwa unapata matokeo madogo na kuridhika nayo.
Sasa unakwenda kufikiri kwa ukubwa, kitu kinachotanua fikra zako na kukusukuma zaidi ya ulivyozoea huko nyuma.
Hivyo kwa kufanyia kazi kanuni hii kwa uhakika, utakuza utajiri wako kwa kasi ndani ya muda mfupi.

Rafiki, hiyo ndiyo dhana muhimu ya kukuza utajiri wako kila mwaka ili ndani ya miaka 10 uwe umefika kwenye uhuru wa kifedha na kuwa na maisha huru kabisa.

Pamoja na urahisi wa kueleweka kwa hili, bado siyo rahisi kwenye utekelezaji na ukiwa peke yako unaweza kuona kama unajidanganya.
Hilo linaeleweka kabisa na ndiyo limekuwa kikwazo kwako kwa muda mrefu na kukuzuia usipige hatua kubwa.

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana nimechagua kukupa nafasi ya kipekee, nafasi ya kufanya kazi kwa karibu kabisa ili uweze kupiga hatua hizo kubwa.
Nafasi hiyo inapatikana kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Hii ni jamii ya tofauti na ya kipekee kabisa ambayo ina watu wenye kiu ya mafanikio makubwa.
Kwa kuwa ndani ya jamii hii, unapata nafasi ya kuyaishi haya ninayokushirikisha hapa kwa vitendo ili kuweza kupata matokeo bora kabisa kwenye maisha yako.

Kwa bahati mbaya sana nafasi ndani ya KISIMA CHA MAARIFA ni chache mno na muda wa kujiunga pia umefika ukingoni.
Mwaka wetu wa mafanikio kwenye KISIMA CHA MAARIFA unaanza Novemba 1, hivyo unapaswa kuwa umejiunga mapema kabla ya huo mwaka kuanza, ili tufanye kazi kwa pamoja kwa mwaka mzima na uyaone matokeo ya tofauti.

Hivyo tarehe 30/10/2021 ndiyo mwisho wa kupata nafasi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kama unataka kweli kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako ndani ya mwaka mmoja ujao, jiunge sasa na KISIMA CHA MAARIFA.
Tuma ujumbe sasa kwenda namba 0717 396 253 ili kupata utaratibu kamili wa kuwa ndani ya jamii hii.

Rafiki, fursa ya kuyabadili maisha yako iko mbele yako sasa, ni wewe uchukue hatua sasa na unufaike au usichukue hatua na ubaki pale ulipo.
Baada ya yote, maamuzi ni yako, hivyo fanya maamuzi ambayo ni mema kwako.

Nakusubiri kwa hamu ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, maana najua hutabaki kama ulivyokuwa.

Na kama hujapata kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO jipatie nakala yako sasa. Hiki ni kitabu kinachokupa mwongozo kamili wa kuendesha maisha yako kila siku ili kufika kwenye mafanikio makubwa.
Kimesheheni mambo madogo madogo ambayo umekuwa huyapi uzito ila yanaathiri sana mafanikio yako.
Jipatie nakala yako ya kitabu leo kwa kuwasiliana na 0752 977 170 na utatumiwa au kuletewa kitabu popote ulipo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.