Rafiki yangu mpendwa,
Tukiwa tumebakiza siku moja pekee ya kupata nafasi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jamii ya tofauti na ya kipekee katika kuyasaka mafanikio, napenda kukushirikisha kitu kimoja muhimu sana.
Kitu hicho ni kauli ya kujiambia kila siku ambayo itakuwesesha kufikia lengo la utajiri ulilojiwekea kama tulivyojifunza kwenye makala iliyopita.
Nimeshakueleza mengi sana kuhusu KISIMA CHA MAARIFA na umuhimu wa wewe kuwa kwenye jamii hii. Hapa nitakwenda moja kwa moja kwenye kauli hiyo na kisha kukuonyesha kwa nini ni muhimu.

Kauli muhimu ya kujiambia kila siku ni hii;
“Mimi ……………………………….(andika majina yako kamili) kufika tarehe 30/09/2022 ninao utajiri wa thamani ya Tsh……….. (andika namba yako ya thamani ya utajiri unaotaka kufikia).
Utajiri huu unakuja kwangu kwa viwango mbalimbali katika muda nilionao. Ili kupata utajiri huo, ninatoa huduma bora kabisa kama muuzaji wa ………………….. (andika thamani unayotoa kwa wengine).
Ninaamini bila ya shaka yoyote kwamba nitapata utajiri huu na tayari nauona utajiri huo kwa macho yangu, ukisubiri kuja kwangu.
Tayari ninao mpango wa kukusanya utajiri huo na ninaufanyia kazi kila siku bila kuacha.”
Andika kauli hii kwenye karatasi nyeupe kisha weka tarehe na sahihi mwisho wa kauli hiyo na ifanyie lamination karatasi hiyo. Kila siku unapoamka soma kauli hiyo kwa sauti na kwa hisia huku ukijiona ni kitu ambacho kimeshakamilisha. Kabla ya kulala pia rudia zoezi hilo.
Kauli hii inaleta pamoja misingi yote ambayo tumekuwa tunajifunza katika kufikia mafanikio.
Baadhi ya misingi hiyo ni;
1. Lengo linalopimika kwa uhakika (kiasi cha utajiri unachotaka).
2. Muda wa kufikia lengo hilo (tarehe ambayo umepanga kufikia lengo).
3. Kuwa tayari kutoa thamani ili kupata utajiri unaoutaka, maana hakuna cha bure.
4. Kuamini ni kitu kinachowezekana, kitu kinachojenga fikra sahihi.
5. Kujiambia kauli hiyo kila siku hivyo kuziweka fikra zako kwenye lengo.
Rafiki, kama ambavyo nimekuwa nakushirikisha, kujifunza haya ni rahisi, lakini kuyaishi kwa uhalisia ili upate matokeo siyo rahisi.
Ndiyo maana nimekupa nafasi ya kuwa karibu na mimi, nikusimamie kwa uhakika katika kuiishi misingi hii na upate matokeo makubwa kwenye maisha yako.
Nafasi niliyoitoa ya wewe kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA ili tufanye kazi kwa karibu inaisha kesho.
Kama umekuwa unapokea jumbe hizi kwa muda na kuona zina mchango kwako, chukua hatua leo hii ujiunge.
Kwani nafasi ni chache na siku imebaki moja pekee.
Tuma sasa ujumbe kwenda namba 0717 396 253 ili kupata nafasi ya kuwa kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, jamii ya tofauti na ya kipekee kabisa katika kuyaendea mafanikio makubwa kwenye maisha.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.