Rafiki yangu mpendwa,
Ushauri mmoja mfupi ambao nimekuwa nautoa sana na ambao naamini kila mtu akiuelewa dunia itakuwa bora sana ni huu; HAKUNA KITU CHA BURE.

Kila kitu kina gharama ambayo inaingia katika kukiandaa. Na kwa hii dunia ya kiuchumi ambayo tunaishi, gharama hizo zinapimwa kwa muda, juhudi na fedha.

Hakuna kitu chochote kile kinachoweza kupatikana bure. Hivyo unapoona kuna kitu unapata bure, jua wazi kuna namna unalipia bila wewe kujua au kuna wengine wanalipia kwa niaba yako.

Hili linatuleta kwenye njia kuu za mawasiliano tunazotumia sana kwenye zama hizi, ambazo kuu ni mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter na WhatsApp.

Mitandao hiyo imekuwa inajinadi ni ya bure kabisa, kwamba huwalipi wenye mitandao ndiyo uweze kuitumia. Ni wewe tu kujiandikisha na kuanza kutumia mitandao hiyo.

Lakini cha kushangaza sasa, mitandao hiyo hiyo unayoaminishwa ni ya bure, ndiyo imezalisha matajiri wakubwa duniani.
Mark Zuckerberg ambaye ni mkurugenzi wa kampuni inayomiliki mitandao ya Facebook, Instagram, WhatsApp na mingine, yupo kwenye kumi bora ya matajiri duniani.
Huyu ni mtu ambaye hajawaji kuwa na kazi au biashara ya aina nyingine nje ya mitandao hiyo ya kijamii.

Nini kinaendelea hapo?
Iweje mtu anayetoa huduma ya bure awe pia ndiye tajiri mkubwa duniani?
Unapojiuliza maswali hayo na kutafakari kwa kina, ndiyo unaona ukweli ambao umekuwa unafichwa kwa muda mrefu.

Ukweli ni kwamba, mitandao ya kijamii siyo bure kama inavyojinadi.
Na mbaya zaidi, mitandao hiyo imekugeuza wewe mtumiaji kuwa bidhaa ambayo inauzwa.

Ndiyo, utajiri mkubwa ambao mitandao ya kijamii imetengeneza, unatokana na kuuza umakini wa watumiaji wa mitandao hiyo.

Hivyo dili liko hivi;
Wanasema kutumia mtandao wao ni bure, na watu wanakimbilia kwa sababu wanapenda vya bure.
Wanateka umakini wa watumiaji hao kwa kuhakikisha wanatumia mitandao hiyo kwa muda mrefu.
Wanakusanya taarifa za watumiaji hao na kuziuza kwa wale wanaotaka kutangaza biashara zao.

Unajionea hapo mwenyewe, kwamba kwa matumizi yako ya mitandao ya kijamii, umegeuzwa kuwa bidhaa ambayo inauzwa, bila ya wewe kujua.

Inapokuja kwenye swala la fedha, watu hutumia kila mbinu ili kuzipata nyingi zaidi. Na moja ya mbinu hizo ni kuuza zaidi.
Makampuni ya mitandao ya kijamii yanapotaka kupata fedha zaidi, yanateka umakini wako zaidi na kuuza kwa wengi zaidi.

Ufanye nini kwenye hili?

Nilichokueleza hapa ni tone tu kutoka kwenye bahari ya mengi yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii ambayo hayana manufaa kwako.

Kwenye kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI nimekushirikisha kwa kina mbinu zote ambazo mitandao ya kijamii imekuwa inatumia kukuchukua mateka na kisha kukuuza kwa namna ambayo mitandao hiyo inataka yenyewe.

Kitabu hicho pia kina suluhisho la namna ya kuondoka kwenye huo utumwa ambao umetekwa na kuweza kuwa huru tena.

Ninachoweza kukuambia na kukuhakikishia ni kwamba kama umekuwa unatumia mitandao ya kijamii kwa muda sasa, akili yako haiko sawa tena.
Kuna namna mitandao hiyo imeshaharibu na kuteka akili yako bila ya wewe mwenyewe kujua.

Moja ya dalili za namna mitandao ya kijamii imeharibu akili yako ni kitu kinaitwa FOMO (Fear Of Missing Out). Hii ni hali inayotokea pale ambapo unakuwa hujatumia mtandao wa kijamii kwa muda, unaona kama unapitwa hivi. Hivyo unakimbilia kutumia kila mara ili usipitwe na chochote.

Hiyo ni dalili moja, lakini zipo nyingi ambazo zinaonyesha jinsi mitandao ya kijamii imekuteka na kukuuza bila wewe mwenyewe kujua.
Pata leo na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili uweze kupata uelewa na kuchukua hatua sahihi za kurudisha uhuru wako.

Wasiliana sasa na 0752 977 170 ili kupata kitabu hiki kizuri cha kukuondoa kwenye mateka na gereza ambalo mitandao ya kijamii imekushikilia.
Kama unatumia simu janja (smartphone) na mtandao wowote wa kijamii, hiki ni kitabu unachopaswa kusoma, maana wenzako wamejipanga kweli kweli kukuteka na kukuuza.
Kama huna maarifa sahihi ya kukwepa mitego yao, wataendelea kukutumia watakavyo wao.

Mimi kama rafiki yako nataka uwe huru kuyaishi maisha yako kwa namna ambayo ni sahihi kwako.
Ndiyo maana mara zote nimekuwa nakushirikisha maarifa ya kukuwezesha kuwa na uhuru huo.
Kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ni moja ya zana muhimu mno unazopaswa kuwa nazo ili kuvuka vyema kwenye zama hizi tunazoishi sasa. Kipate kitabu sasa kwa kuwasiliana na 0752 977 170 uletewe au kutumiwa ulipo.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.