#SheriaYaLeo (94/366); Jua nani mwenye mamlaka.
Katika eneo lolote lile, iwe ni taasisi, biashara au jamii, kuna watu wachache au mmoja ambaye ndiye mwenye mamlaka makubwa.
Mara nyingi mtu au watu hao siyo wale wanaoonekana kuwa viongozi, wanaweza kuwa watu wengine kabisa, ambao wanafanya mambo yao nyuma ya pazia.
Unapotaka kupiga hatua zaidi kwa kile unachofanya au pale ulipo, ni muhimu uwajue wale wenye mamlaka makubwa na kwenda nao vizuri ili wasiwe kikwazo kwako.
Watu wengi wamekutana na vikwazo na kushindwa kukua kwa kutokujua wenye mamlaka makubwa.
Wanadhani viongozi wanaoonekana ndiyo wafanyaji maamuzi wakuu, kumbe kuna wengine ambao kwa nje hawaonekani kuwa na mamlaka makubwa, ila kwa ndani ndiyo wanafanya maamuzi yote makubwa.
Sheria ya leo; Popote ulipo na kama unataka kupiga hatua zaidi, jua wale wenye mamlaka makubwa ambao ndiyo wafanyaji maamuzi wakuu. Mara nyingi siyo wale wanaoonekana. Ukishawajua nenda nao sawa ili wasiwe kikwazo kufika unakotaka kufika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji