2590; Kujipendekeza.
- Sisi binadamu ni viumbe wa kihisia, huwa tunafanya maamuzi kwa hisia na kisha kuyahalalisha kwa mantiki.
-
Chochote unachotaka kwenye maisha yako kinatoka kwa watu wengine. Unawategemea sana watu wengine, hakuna unachoweza peke yako.
-
Ukiwafanya watu wajisikie vizuri, watakuwa tayari kukupa unachotaka. Ukiwafanya wajisikie vibaya hawatakuwa tayari kukupa unachotaka.
-
Watu huwa wana msimamo hata kwenye mambo ya kijinga. Wakishachukua upande fulani, wataendelea kusimamia upande huo hata kama hawapo sahihi. Kwao msimamo ni muhimu kuliko usahihi.
-
Wajibu wako mkubwa ni kuwafanya watu wajisikie vizuri ili wakupe unachotaka. Kuwaweka kwenye msimamo wa kuendelea kukupa unachotaka.
-
Watu wanaweza kuita hilo kujipendekeza, ‘uchawa’, kimbelembele na mengine.
-
Kumbuka, dunia imegawanyika kwenye makundi mawili, wale wanaopata wanachotaka (ambao ni wachache) na wengine wote (ambao ni wengi).
-
Maisha ni maigizo, kilicho muhimu siyo hasa unachofanya, bali wengine wanavyochukulia kile unachofanya.
-
Wenye mamlaka makubwa na wanaofanya maamuzi ni wachache, hao ndiyo wa kuwajua na kwenda nao sawa.
-
Mara zote fanya kilicho sahihi.
Usivunje sheria au tararibu mbalimbali ili kupata unachotaka, unaweza kupata, lakini itakuja kukusumbua.
Usiwaumize wengine ili kupata unachotaka, hata ukikipata utatumia nguvu nyingi kukabiliana na maadui uliowatengeneza kuliko kufurahia ulichopata.
Hatua ya kuchukua;
Kwa kila unachotaja, jua watu gani wenye mamlaka makubwa juu ya hicho kisha wape kile wanachotaka ili nao wakupe unachotaka.
Tafakari;
Binadamu hatupendi deni, mtu anapotupa kitu fulani, tunahakikisha tunamlipa kwa namna yoyote ile. Hivyo unapotaka watu wakupe kile unachotaka, anza wewe kwa kuwapa kile wanachotaka wao.
Kocha.