Rafiki yangu mpendwa,
Kitu kimoja kikubwa sana ambacho nimejifunza kwenye huduma ya ukocha ninayotoa ni hiki; kila mtu anajua anachotaka, ila wengi hawana ujasiri wa kupambania kile wanachotaka mpaka wakipate.
Kwa kuwa wengi wamezungukwa na watu waliokata tamaa na ambao hawafanyi makubwa, nao pia wanajikuta wamekata tamaa na hawafanyi makubwa.
Hivyo kwenye ukocha huwa simpangii mtu afanye nini, bali namuuliza anataka nini na kisha namsimamia na kumwongoza kwa karibu mpaka apate anachotaka.
Simkubalii mtu kirahisi pale anapotaka kukata tamaa au kuishia njiani. Badala yake nakuwa naye karibu na kumpa mitazamo mbadala ili aweze kubaki kwenye safari yake.

Huduma ya ukocha inawasaidia sana watu kuacha kujihujumu wao wenyewe, kitu ambacho ni kikwazo kikubwa kwa mafanikio ya wengi.
Watu huwa wanajihujumu wenyewe na kujizuia kufanikiwa kwa kutokuwa na ujasiri wa kukiendea kile wanachokitaka.
Ndiyo maana nimekuwa nasisitiza sana kwa mtu yeyote aliye makini na anayetaka kufanikiwa basi anapaswa kuwa na kocha.
Changamoto kubwa kwenye hili imekuwa ni kupata kocha sahihi na pia kuweza kumudu gharama za ukocha.
Makocha sahihi kwa mafanikio wapo wachache sana.
Na pia gharama za kupata huduma hiyo ni kubwa.
Kwa kutambua hilo, kila mwaka huwa natoa nafasi ya watu kupata huduma ya ukocha bure kabisa kwa kushiriki kwenye CHANGAMOTO YA SIKU 100 za kufanya kitu bila kuacha.
Kwa kushiriki changamoto hiyo na kufanya kitu kimoja kwa siku hizo 100, unafanikiwa kujenga tabia kwenye kitu hicho na kuweza kuendelea kukifanya kwa muda mrefu.
Mwaka huu changamoto inakwenda kuanza tarehe 15/02/2022 mpaka tarehe 29/05/2022.
Napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha ushiriki changamoto hii ili uweze kujenga tabia itakayokufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Hatua za kuchukua ili kushiriki changamoto ni hizi;
1. Chagua kitu kimoja ambacho utakifanya kila siku kwa siku 100 bila kuacha.
2. Chagua ushahidi utakaouonyesha kwa wengine kila siku kwamba kweli umefanya.
3. Jiunge kwenye kundi maalumu la whatsapp la changamoto hiyo kwa kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/G91eD4TykPT8PjM1wyNukX
Karibu sana kwenye changamoto ya simu 100 za kufanya bila kuacha.
Chagua kujisukuma kufanya kitu kila siku kwa siku 100 bila kuacha na kwa hakika utajijengea tabia bora za mafanikio.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.