Rafiki Yangu,

2021 Bilionea Roy Alipokuwa Akihojiwa na Mwandishi Kutoka BBC London Uingereza Alinukuliwa Akisema “

 Usifanye Tu.

Usisome tu, chukua hatua.

Usibadilike tu, badilisha.

Usiahidi tu, thibitisha.

 Usiwaze tu, tafakari.

Usichukue tu, toa.

Usione tu, hisi.

Usionyeshe tu, fanya.

Usisikie tu, sikiliza.

Usionyeshe tu, tenda.

 Usiseme tu onyesha.

Usiishi tu, ishi.”


Swali la msingi kabisa kwako rafiki yangu ni hili; najua unayataka mafanikio kwenye maisha yako,

……lakini je una mwongozo sahihi wa kukufikisha kwenye mafanikio hayo?

Nimekuuliza swali hilo kwa sababu hapo ndipo watu wengi wamekuwa wanashindwa.
Wanayataka mafanikio,

….lakini hawana mwongozo sahihi wa kuyapata.

Kinachotokea ni watu kujikuta wakihangaika na kila njia au fursa inayopita mbele yao.

 Kila kipya anachosikia kinaleta mafanikio anahangaika nacho.

Mwisho anajikuta amehangaika na mengi, amechoka lakini hakuna matokeo mazuri ambayo ameyazalisha.

Hicho ndiyo ninataka kukuepusha nacho wewe rafiki yangu, kwa kuhakikisha unakuwa na mwongozo sahihi unaoufuata ,

…….ili kuweza kufika kwenye mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Habari njema ni kwamba mwaka huu 2022 unaweza kuharakisha safari yako ya mafanikio kwa kusoma KITABU; MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.

Huenda umesoma vitabu na maarifa mengi kuhusu mafanikio.


Na huenda umeshaona siri za mafanikio ni zile zile,

……….kujua unachotaka,

 ……….kujitoa kweli kukipata na kuwa mvumilivu katika kukifanyia kazi.

Unaweza Ukawa Unajiuliza Ni Kwanini Usome Kitabu Hiki Cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO?..

Jibu ni  kwa sababu kitabu hiki ni cha tofauti kabisa na vitabu vingine vya mafanikio.

Wakati vitabu vingi vya mafanikio vikikupa hamasa ya kukuonyesha inawezekana na unaweza,

Kitabu hiki ni mwongozo, kinakupa yale ya kufanyia kazi ili kweli ufanikiwe.

Hiki siyo tu kitabu cha kusoma na kujisikia vizuri kuhusu mafanikio, ukapata hamasa na ikaishia hapo.

Bali ni kitabu cha kuenda nacho kwa maisha yako yote, kukitumia kama rejea kwenye safari yako ya mafanikio.

Ni kitabu kinachogusa maeneo yote muhimu kwenye safari yako ya mafanikio.

Kikianza na maana ya mafanikio, ambayo haijawahi kufanana kati ya mtu mmoja na mwingine.
Wengi wanahangaika kukimbizana na mafanikio ambayo siyo yao, kwa sababu hayaendani na maana yao ya mafanikio.


Kitabu kitakusaidia kutengeneza maana yako ya mafanikio inayoendana na wewe.

Halafu kuna ubatizo wa mafanikio, kitu muhimu mno ambacho watu wengi wanakikosa na ndiyo maana hawafanikiwi.


Ninachoweza kukuambia ni hiki, watu wote waliofanikiwa wamepata ubatizo wa mafanikio na watu wote walioshindwa wamekosa ubatizo huo.


Kitabu kitakuonyesha jinsi ya kupata ubatizo huo ili ujipe uhakika wa kufanikiwa.

Kuna swala la maamuzi, ambalo kwa wengi limekuwa mtihani.

Wengi hufanya maamuzi kwa mazoea au kwa kusukumwa na hisia, kitu ambacho huwa hakileti matokeo mazuri.


Maamuzi unayofanya kila siku yanajenga au kubomoa mafanikio yako.


Kitabu kitakuongoza kufanya maamuzi bora kwako ili uweze kufanikiwa.

Falsafa ni muhimu sana kwenye maisha ya mafanikio.

Kama huna unachosimamia basi jua chochote kitakuangusha.

 Wengi wanaishi falsafa wasizozijua na ambazo hazina manufaa kwao.


Kwenye kitabu hiki unakwenda kujifunza falsafa bora kabisa inayoendana na maisha ya mafanikio ambayo ni falsafa ya Ustoa (Stoicism).

Hii ni falsafa ambayo wengi wa waliofanya makubwa hapa duniani wamekuwa wakiishi.


Kwenye kitabu utajifunza mazoezi muhimu ya kuiishi falsafa hii kila siku.

Kikubwa zaidi ni sheria 100 za maisha ya mafanikio unazokwenda kujifunza kwenye kitabu cha MWONGOZO wa maisha ya mafanikio.


Bila sheria ni rahisi mtu kuendeshwa na hisia ambapo matokeo yake huwa siyo mazuri.


Ili upate mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unapaswa kuzijua na kuzifuata sheria 100 muhimu utakazojifunza kwenye kitabu.

Na mwisho kitabu kina shuhuda za watu mbalimbali walioshiriki changamoto ya siku 30 za kufanya kitu bila kuacha hata siku moja.


Hii ni changamoto tuliyoianzisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA na ambayo imeleta matokeo makubwa sana kwa kila aliyeishiriki.


Kupitia kitabu utapata pia nguvu ya kujipa changamoto ya kufanya makubwa kwa upande wako.

Rafiki, hiki ni kitabu ambacho hupaswi kukikosa, maana ndiyo mwongozo sahihi kwako kufikia kwenye mafanikio makubwa ambayo unayataka kwenye maisha yako.

Maarifa hayo yote mazuri unakwenda kuyapata kwa gharama ya tsh elfu 19,999tu!

Badala Ya Tshs 29,999 SAVE Tshs (9,999) NZIMA.

Jipatie nakala yako ya kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO leo hii ili ukae sawa kwenye safari yako ya mafanikio na usibabaishwe na yeyote.

Kupata kitabu hiki, Piga simu au tuma meseji kwenda  namba 0752 977 170 na utaletewa kitabu kama upo Dar na kama upo mkoani utatumiwa kule ulipo.

Usiendelee kujichelewesha kwenye safari yako ya mafanikio,

Jipatie nakala yako leo hii ili uwe na mwongozo sahihi wa kufanikiwa kwenye maisha.

Kutoka kwa rafiki yako anayekujali sana.

Bwana Rama |Copywriter Of SOMA VITABU TANZANIA|

Karibu. www.somavitabu.co.tz