2949; Upendeleo.
Rafiki yangu mpendwa,
Miaka ya nyuma niliwahi kuongea na rafiki yangu ambaye alikuwa ameomba kazi ya udaktari kwenye shirika fulani kubwa.
Alikuwa ananishirikisha baadhi ya maswali aliyoulizwa wakati wa usaili.
Moja ya maswali aliyoulizwa ni iwapo kuna foleni ya watu wanasubiria kuingia kwa daktari na kuna mtu wa kawaida na kiongozi wapo kwenye foleni, ataanza kumwita nani?
Yeye akajibu ataanza kumwita aliyeanza kufika.
Nilimwambia hakujibu kwa usahihi, hata kama mtu wa kawaida ndiye aliyetangulia kufika, alipaswa kumpa upendeleo kiongozi, kwa sababu akitoka hapo anakuwa na majukumu makubwa zaidi kuliko mtu wa kawaida.
Kocha mmoja wa mpira aliwahi kunukuliwa akisema iwapo mchezaji wake bora kabisa atasinzia wakati wa mazoezi, atahakikisha anapewa mto ili asiumie na pia mtu anakaa nyuma yake ili ilitokea ameyumba asianguke vibaya.
Lakini ikitokea mchezaji wa kawaida amesinzia wakati wa mazoea, atampa adhabu kali ili arudishe umakini wake wote kwenye mazoezi.
Kwa mifano hiyo miwili, unaweza kuona siyo sawa, kwa nini watu wote wasichukuliwe sawa, kwa nini kuwe na upendeleo kwa baadhi ya watu?
Hilo ndiyo tunakwenda kulijadili leo.
Pamoja na viwango na misimamo mbalimbali unayojiwekea kwenye maisha yako, kazi na biashara, unapaswa kuwa na upendeleo.
Kuna watu wachache sana, ambao wanaonyesha uwezo wa kipekee kabisa ambao unapaswa kuwapa upendeleo.
Hawa unawavumilia hata kama wanakwenda kinyume na utaratibu, kwa sababu matokeo wanayozalisha ni makubwa sana.
Kila sheria huwa ina upendeleo wake fulani, lakini huwa ni mchache na kwa matokeo ambayo siyo ya kawaida.
Sheria ikiwa na upendeleo mwingi, inaacha kuwa sheria.
Hivyo pamoja na vigezo vya juu unavyojiwekea kwenye maeneo yako mbalimbali, usiache kuwapa upendeleo wale wachache sana wanaokupa matokeo ya kipekee kabisa ambayo hakuna wengine wanaweza kukupa.
Inaweza kuwa ni mfanyakazi ambaye anakupa matokeo bora mno lakini kuna utaratibu hafuati. Au ikawa ni mteja anayeleta mamufaa makubwa kwenye biashara lakini anashindwa kutimiza baadhi ya vigezo ulivyoweka.
Kuwa na upendeleo kwa matokeo yasiyokuwa ya kawaida siyo kukosa msimamo au unafiki. Bali ni kuendana na uhalisia.
Vigezo na viwango unavyokuwa umeweka ni kwa ajili ya kuleta matokeo makubwa na ya uhakika.
Kama kuna ambao wanakupa matokeo hayo bila kutimiza vigezo na viwango vingine, unaweza kuwapa upendeleo kwa muda.
Upendeleo unapaswa kuwa wa nadra sana na kwa wachache mno ambao wamethibitisha kuweza kuzalisha matokeo ya viwango vya juu mno ambavyo hakuna mwingine anayeweza kufikia.
Lakini kwa wengine ambao wanazalisha matokeo ya kawaida, yanayozalishwa na walio wengi, wanapaswa kufuata kila kigezo na utaratibu uliopo.
Unaweza kusema wale unaowapa upendeleo watakusumbua kwa kuwa na kiburi. Watajiona wao ni muhimu kuliko wengine na itakuwa vigumu kwako kuwasimamia.
Hilo ni kweli, lakini wewe unawapa upendeleo siyo kwa sababu zao binafsi, bali kwa sababu ya matokeo wanayozalisha.
Hivyo kama kuna matokeo bora wanazalisha, unaweza kuvumilia usumbufu huo.
Lakini pale watakapoacha kuzalisha matokeo hayo ya tofauti, ndipo watakaposhangaa jinsi mambo yatakavyobadilika.
Kwenye ukurasa utakaofuata utajifunza hilo kwa kina, kupitia mfano wa kuku aliyekuwa anataga sana au ng’ombe aliyekuwa anatoa maziwa mengi. Wote huishia kuchinjwa pale uzalishaji wao unapopungua.
Hivyo pia ndivyo upendeleo unaotoa kwa watu unavyoisha.
Tunachoangalia ni mchakato na matokeo.
Haleti matokeo anapaswa kuwa kwenye mchakato kwa uhakika bila kuyumba.
Analeta matokeo makubwa sana na yasiyo ya kawaida, anaweza kuvumiliwa hata kama hakai kwenye mchakato.
Ila tu asiwe anatumia njia zilizo nje ya sheria kuzalisha matokeo hayo.
Kumbuka upendeleo tunaoongelea hapa ni kwa wachache wenye uwezo na vipaji vya kipekee kabisa na ambao matokeo wanayozalisha hakuna wengine wanaoweza kuyazalisha.
Hawa huwa ni wachache sana.
Usianze kutoa upendeleo kwa kila mtu kwa sababu tu amekufurahisha na matokeo fulani. Ni kwa wale wa kipekee sana, ambao huwa ni wachache mno na nadra kukutana nao.
Sheria au utararibu wowote ukiwa na upendeleo kwa wengi unakosa nguvu na kupuuzwa.
Hivyo hili ni eneo la kuwa nalo makini sana.
Pamoja na kuwa tayari kuwapa baadhi ya watu upendeleo, bado kuna mambo ya msingi anayopaswa kuyazingatia, ili upendeleo unaotoa usiwe wa kubomoa bali kujenga.
Lazima afuate taratibu za msingi zinazosaidia kujenga ushirikiano mzuri baina ya wote wanaojihusisha nao.
Msimamo lazima uwepo, lakini pia upendeleo kwa wachache wanaostahili haupaswi kukosekana.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsante sana Kocha kwa makala ya leo, nimejifunza mengi, hasa kutoka kwa huyu kuku na ng’ombe wanaoonekana kuzalisha sana lakini mara tu baada ya kukoma uzalishwaji basi huwa wanaishia kichinjwa.
Ahsante sana, naenda kulitumia somo hili kwenye team yangu ya mauzo
#NidhamUpendo
LikeLike
Asante sana nimefurahi sana kusoma makala hii
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kila SHERIA ina upendeleo wake fulani…..
LikeLike
Kabisa, ni vyema kutumia hilo kwa umakini mkubwa.
LikeLike
Msimamo lazima uwepo, lakini pia upendeleo kwa wachache wanaostahili haupaswi kukosekana.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Ahsante sana kocha, hii point ya upendeleo ni nimeielewa sana
LikeLike
Vizuri, inapaswa kutumika kwa tahadhari.
LikeLike
Asante kocha
Asili ina upendeleo,lakini upendeleo huo unakua na matokeo makubwa,upendeleo upo tu kwa yule anaeleta matokeo makubwa kwenye anachokifanya bila kuvunja sheria za asili,lakini kama matokeo ni ya kawaida lazima kukaa kwenye mchakato .Na kama matokeo hayapatikani na mchakato haufuatwi hapa lazima adhabu ihusike.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante Sana kocha kwa makala hii , nimejifunza kwamba
Ni juhudi zako tu ndio zitakazokulinda na si vinginevyo.
Toa matokeo Bora zaidi ya ilivyokusudiwa na utaona matokeo yake, unaweza kupitia kwenye mataa mekundu na trafiki akakuambia endelea na safari yako.
Pia makala hii imenizindua kwamba hatupaswi kutegemea hisani , Bali ni kujitahidi kufanya kwa ubora ili kutoa matokeo ya viwango vya juu kabisa
LikeLike
Tuweke juhudi.
LikeLike
Tunatakiwa kupapa upendeleo wachache wanaoletaatokeo makubwa kwenye biashara zetu. Mimi Kuna mteja ambaye Kila nikileta mzigo lazima anunue, kwahiyo hata kama siku hiyo amekuja na hela kidogo nampatia anachotaka
Pia mfanyalazi anayefanya vizuri kwenye mauzo namlpa zaidi
LikeLike
Lazima tutofautishe kwenye kujali.
LikeLike
Asante kocha kwa makala hii yenye funzo kubwa sana katika biashara zetu.
LikeLike