2955; Kupendwa au kuheshimiwa?
Rafiki yangu mpendwa,
Wajibu wetu wa kwanza kama viongozi kwenye biashara zetu ni kuwafanya watu wafanye vitu ambavyo hawataki kufanya, lakini vyenye manufaa kwao.
Na hilo halitakuweka kwenye nafasi ya kupendwa sana na watu hao unaowaongoza, kwa sababu utakuwa unawasukuma kuondoka kwenye mazoea.
Hakuna kitu kinachowafanya watu wajisikie vizuri kama kukaa kwenye mazoea.
Sasa kitendo cha wewe kuwasukuma kutoka kwenye mazoea waliyojijengea, hakitapokelewa kwa urahisi.
Kitaonekana ni kigumu, kibaya na kisicho wezekana.
Kama utakachokuwa unataka ni kupendwa na watu unaowaongoza, hutawalazimisha kwenye mabadiliko hayo, kwa sababu hutaki wajisikie vibaya.
Hivyo utawaacha waendelee na mazoea ili wajisikie vizuri na kukupenda.
Njia hiyo inaonekana rahisi na itakayokupa umaarufu kwa sababu ya kupendwa.
Lakini mapenzi ni hisia tu, haitachukua muda kabla watu hao hao wanaokupenda wataanza kukuchukia.
Hapo ni baada ya kuwa wamebaki pale walipo na kushindwa kupiga hatua.
Upande wa pili ni kuheshimiwa.
Kuheshimiwa kunakuja pale unapowawezesha watu kufanya mabadiliko yenye tija kwenye maisha yao.
Awali wanakuwa wabishi kwa sababu hawataki mabadiliko.
Watakuchukia kwa yale utakayokuwa unasimamia.
Lakini mabadiliko watakayoyaona kwenye maisha yao, yatawafanya wakuheshimu sana.
Uzuri wa heshima huwa inadumu muda mrefu. Hata kama mtu hakupendi, akishakuheshimu kwa kile sahihi ulichofanya, ataendelea kukuheshimu kwa muda mrefu.
Heshima ya mtokeo bora unayokuwa umezalisha huwa inadumu kwa muda mrefu. Na hiyo inakupa fursa za kuendelea kufanya makubwa zaidi.
Sisi ni binadamu, inapokuja kati ya kupendwa na kuheshimiwa, huwa ni rahisi kwetu kukimbilia kupendwa.
Hiyo ni kwa sababu tunajali sana wengine wanatuchukuliaje.
Kama unachoangalia ni matokeo ya muda mfupi, utakimbilia kupendwa.
Lakini kama unachoangalia ni matokeo ya muda mrefu, utakimbilia kuheshimiwa.
Ili ukae upande wa kuheshimiwa, unatakiwa kutokujali watu wengine watakuchukuliaje.
Wewe unachopaswa kufanya ni kusimama kwenye yale yaliyo sahihi na kupuuza mengine yote.
Unapaswa kujiwekea viwango vya juu sana, kuwatendea wengine haki na kuzalisha matokeo makubwa.
Watu watakuchukia awali kwa sababu unavuruga mazoea yao.
Lakini watakuheshimu sana baadaye watakapoona matokeo makubwa na tofauti kwao.
Kama utakosa msimamo kwenye yale unayofanya, utakata tamaa haraka kabla hujarika kwenye hatua ya kuheshimika.
Mwanzo wa mabadiliko yoyote yale huwa unachukiwa na wote wanaohusika nayo.
Ni pale matokeo makubwa na mazuri yanapopatikana ndiyo heshima kubwa inapojengeka.
Hilo halitakuwa rahisi, kwa sababu utalazimika kuwasukuma sana watu kutoka kwenye mazoea yao.
Kutakuwa na upinzani mkubwa sana, wapo watakaokukimbia, wengine watasema mambo mengi mabaya kuhusu wewe.
Lakini hupaswi kuruhusu yote hayo yawe na athari kwako.
Hupaswi kuyafanya yakuondoe kwenye njia sahihi.
Kipaumbele chako kama kiongozi siyo kumfurahisha kila mtu, unajua hilo haliwezekani.
Kipaumbele chako ni kuleta mabadiliko chanya, kitu kinachoweza kujidhihirisha, lakini kwa nguvu na gharama kubwa.
Kama kiongozi, wajibu wako ni kuchochea moto kila wakati bila kuchoka.
Hata kama umechoka kiasi gani, hupaswi kuonyesha hilo kwa unaowaongoza.
Hata kama una wasiwasi juu ya jambo lolote, hupaswi kudhihirisha wasiwasi huo.
Wewe ni sura ya mbele ya kile unachosimamia, hivyo unapaswa kuwa kwenye hali sahihi mara zote.
Hili linakupa kazi mara mbili, kitu ambacho siyo kibaya kwa kuangalia matokeo makubwa unayokwenda kuzalisha.
Usihangaike na kupendwa, hizo ni hisia za muda ambazo huwa hazidumu. Maana watu wa kwanza kukuchukia huwa ni wale wale waliokuwa wanakupenda.
Badala yake hangaika na kuheshimiwa, heshima inayotokana na mabadiliko uliyosababisha huwa inadumu milele.
Kama kiongozi unapaswa kusimama kwenye yale yaliyo sahihi, ambayo yanaleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wengine.
Usijali sana wengine wanakuchukuliaje, wewe jua matokeo ya tofauti utakayoyaleta yatakujengea heshima kubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante kocha sitahangaika na kupendwa nitaangalia zaidi kuheshimiwa Kwasababu heshima haiji mda huohuo heshima inakuja baadaye
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha
Bora kuheshimiwa kuliko kupendwa bila kufanya jambo lenye manufaa kwa wengine kwa kusimamia kilicho sahihi.
Heshima inadumu kwa muda mrefu hata kama mtu hanipendi lakin nilifanya jambo lenye thamani na manufaa kwake basi ataendelea tu kuniheshimu.
Watu wanaokupenda sana ndio wanaokua watu wa kwanza kukuchukia,thamani nayotoa kwa wengine ndiyo itakayonipa heshima ya kudumu.
LikeLike
❤️
LikeLike
Asante sana kocha kwa maarifa haya , ninachagua kuhesgimiwa nitafanya kitu sahihi wakati bila kuhitaji kupendwa
LikeLike
Vizuri kabisa.
Kaa humo.
LikeLike
Nashukuru kocha kweli kabisa kuvunja mazoea kinahitaji kazi hasa sio mchezo ndogo
Maana unaweza kujitoa kufanikisha hilo ila watu wanaokuzunguka wakakukwamisha usipo usoma mchezo vema.
Hivyo nitafanya kile kitachonipa heshima na sio kupendwa.
LikeLike
Asante kocha,inabidi ukiwa kiongozi utafute heshima si watu wakupende,kwa sababu heshima inaletwa na kazi na nguvu kubwa ulioifanya ingawa inachukua mda.
LikeLike
Asante sana kochs Heshima inadumu kwa muda mrefu hata kama mtu hanipendi lakin nilifanya jambo lenye thamani na manufaa kwake basi ataendelea tu kuniheshimu.
Watu wanaokupenda sana ndio wanaokua watu wa kwanza kukuchukia, thamani nayotoa kwa wengine ndiyo itakayonipa heshima ya kudumu kwa wakati wote
LikeLike
Nimekufahamu sana Kocha ingawa hili linahitaji ujasiri mkubwa sana. Nitafanyia kazi
LikeLike
Asante sana kocha, nimejifunza kitu muhimu sana hapa. Yaani, kama ninachoangalia ni matokeo ya muda mfupi, nitakimbilia kupendwa. Lakini kama ninachoangalia ni matokeo ya muda mrefu, nitakimbilia kuheshimiwa.
LikeLike
Ahsante sana Kocha.
Nimejifunza mengi sana kwenye makala ya leo,…
….ila kikubwa ni kuhakikisha naleta mabadiliko sahihi Kwa watu ninaowaongoza kufanya kazi ili baadae waniheshimu kwa matokeo na mabadiliko makubwa watakayokuwa wamepata.
🔥🔥🔥🔥🔥✍️✍️✍️✍️
LikeLike
Usitafute kupendwa, tafuta kuheshimiwa, watakuchukua mwanzo lakini baadaye watakushujuru baada ya kuanza kuona matokeo ya kuwatoa kwenye mtazamo
LikeLike
Kipaumbele changu Kama Kiongozi ni kuleta mabadiliko chanya.💪🏾
LikeLike
Asante Kocha.
Nachagua kuheshimiwa maana Heshima inadumu muda mrefu.
Nitasimamia kilicho bora ili kuleta mabadiriko sahihi na chanya
LikeLike
Asante sana kocha kwa maarifa haya , ninachagua kuhesgimiwa nitafanya kitu sahihi wakati bila kuhitaji kupendwa
LikeLike
Bora kuheshimiwa kuliko kupendwa.Asante kocha kwa hili.
LikeLike
Kama kiongozi unapaswa kusimama kwenye yale yaliyo sahihi, ambayo yanaleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wengine.
Asante sana Kocha, ninaondoka na hii.
LikeLike
Asante sana Kocha. Kweli heshima ni bora na itadumu kuliko kupendwa
LikeLike
Karibu
LikeLike
1.Kama unachoangalia ni matokeo ya muda mfupi, utakimbilia kupendwa.
Lakini kama unachoangalia ni matokeo ya muda mrefu, utakimbilia kuheshimiwa.
2.Hata kama umechoka kiasi gani, hupaswi kuonyesha hilo kwa unaowaongoza.
LikeLike
mazoea yanamfanya mtu ajisikie vizuri.Mabadiliko hayapendwi kwa kua ubongo haupendi vitu vipya na vigumu.Ukifanya kwa mazoea utapendwa sana maana ni rahisi,haihitaji nguvu.
LikeLike
Nachagua kuheshimiwa, kupendwa ni hisia za muda tuu ila heshima inadumu.
Sihitaji kujali watanionaje au wananichukiliaje.
Mara zote nitatenda haki na kusimamia utekelezaji Wa mfumo Wa biashara.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ili nikae upande wa kuheshimiwa, natakiwa kutokujali watu wengine watanichukuliaje.
Napaswa kuwa na msimamo, kusimama kwenye yale yaliyo sahihi na kupuuza mengine yote.
Ahsante Sana Kocha.
LikeLike
Nitahakikisha naheshimiwa badala ya kupendwa katika maisha yangu.
LikeLike
Heshima ni Bora kuliko kupendwa
Asante sana
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante Sana. Nimejifunza Mambo mengi lakini mawili
Muhimu kabisa ni:
1.Usihadaike na KUPENDWA kwa sababu kupendwa ni hisia ambazo huwa hazidumu
2. HESHIMA inayotokana na mabadiliko uliyoyasababish
a daima hudumu milele
LikeLike
Hakika, tufanye yanayojenga heshima.
LikeLike
Asante sana Kocha 🙏🏽, nitayaishi haya yote unayotu fundisha kupitia makala hizi muhimu sana kwetu, pia nitawaelekeza managers wangu umuhimu wa kuheshimika kuliko kupendwa na wale wanao waongoza.
LikeLike
Vizuri kabisa.
Tufanye yale yanayojenga heshima.
LikeLike
Watu wengi wanafanya vitu Ili wapendwe na hii imekuja kuwakosesha mafanikio ya muda mrefu.
Simamia kile unachotaka bila kujali wengine wanakuchukuliaje.
LikeLike
Kabisa.
Tatizo ni kinachopendwa na wengi huwa siyo sahihi.
Na kilicho sahihi huwa hakipendwi na wengi.
Inahitaji roho ngumu kuvuka hilo.
LikeLike
Nitahakikisha naacha alama hapa dunianina kwa wale ninaoshrikiana nao ili waniheshimu maisha yao yote.
LikeLike
Safi kabisa,
Jikumbushe hili mara zote.
LikeLike
Nafanya na kusimamia Mambo sahihi ili niheshimiwe
LikeLike
Safi.
LikeLike
Ni bora kuheshikiwa kuliko kupendwa. Kama wwwe si mbinafsi utachagua kuheshimiwa badala ya kupendwa. Viongpzi wa kisiasa ndo hupenda kupendwa kuliko kuheshimiwa. Lakini sisi viongozi wa biashara tunapaswa kuchagua kuheshimiwa na siyo kupendwa.
LikeLike
Kabisa,
Na ndiyo maana wanasiasa wengi hupendwa mwanzoni na kuja kuchukiwa baadaye, kwa sababu wanatafuta kupendwa na siyo kuheshimiwa.
Huku viongozi wengi wa kibiashara (hasa wale wanaofanikiwa) huchukiwa mwanzoni na kuja kupendwa baadaye, wanapokuwa wamejenga heshima.
LikeLike
Heshima ni kitu cha bure lakini ni gharama kukipata
LikeLike
😀😀
Bure kutoa,
Ila gharama zana kupata.
LikeLike
Kipaumbele changu kama kiongozi siyo kumfurahisha kila mtu bali kuleta mabadili chanya
LikeLike
Kabisa,
Huwajibiki kuwapa watu raha,
Unawajibika kuwapa watu matokeo.
LikeLike
Kama kiongozi, wajibu wako ni kuchochea moto kila wakati bila kuchoka.
Hata kama umechoka kiasi gani, hupaswi kuonyesha hilo kwa unaowaongoza.
LikeLike
Mshumaa uliozima hauwezi kuwasha mshumaa mwingine.
Tuhakikishe mshumaa wetu unawaka muda wote, ili kuweza kuwasha mishumaa ya wengine wanaotuzunguka.
LikeLike
Napaswa kusimamia yaliyo sahihi mara sote.
LikeLike