2974; Umekufa au hutaki.
Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya vitu muhimu unavyohitaji sana kwenye safari yako ya mafanikio ni msimamo usioyumbishwa.
Na msimamo huo haupaswi tu kuwa kwenye yale unayotaka, bali pia kwenye yale unayoahidi.
Unapaswa kufanya neno lako kuwa sheria.
Kwamba ukiahidi unatekeleza kama ulivyoahidi na siyo kuanza kuleta sababu.
Unahitaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana ya kujisukuma kufanya kila ulichoahidi kwa namna ulivyoahidi.
Hilo litakujengea sifa ya kipekee na kufanya uaminike zaidi.
Japokuwa nidhamu na msimamo vinahitajika kwenye kila eneo, kuna eneo moja ambapo hivyo vina nguvu kubwa sana kwako.
Eneo hilo ni kwenye kujali sana muda.
Pale unapokubaliana na wengie kwenye jambo fulani, unapaswa kujali sana muda.
Unapaswa kutekeleza kwa muda mliokubaliana bila ya kuleta sababu.
Kama unataka uheshimike na kuaminiwa na kila mtu, wahi popote unakopaswa kuwa na pia tekeleza majukumu yako kwa wakati.
Hili ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wako kabisa.
Lakini wengi wamekuwa hawawezi kulitekeleza.
Watu wengi huwa ni wachelewaji kwenye kila miadi wanayokuwa nayo.
Na zaidi wanashindwa kutekeleza kitu ndani ya muda wanaopaswa kutekeleza, kama walivyoahidi au kupangiwa.
Na watu hao huwa hawana hata wasiwasi wowote, watakuja wamechelewa wakiwa tayari wana sababu kwa nini wamechelewa.
Watajitahidi kupangilia sababu zao ili kuonyesha kweli ni muhimu.
Lakini watu makini huwa hawazipi uzito sababu zozote ambazo mtu anazitoa pale anaposhindwa kukamilisha kile anachopaswa kukamilisha, iwe ni kuwahi mahali au kukamilisha majukumu fulani.
Watu makini wanajua kuna sababu mbili pekee za watu kushindwa kutekeleza wanachopaswa kutekeleza; wamekufa au hawataki.
Sababu nyingine yoyote tofauti na hizo mbili ni ya kujifanganya tu, haina mashiko yoyote.
Ili uweze kujenga imani na heshima kubwa kwa wengine, unapaswa pia kutumia sababu hizo mbili; umekufa au hutaki.
Yaani inakuwa hivi, pale unapoahidi au kutegemewa kwenye kitu fulani, unakifanya kweli kama ulivyoahidi au unavyotegemewa.
Ikitokea hujafanya, basi watu wajue wazi ni kwa sababu moja kati ya hizo mbili, umekufa au hutaki.
Kama umekufa, hilo linakuwa wazi, halihitaji maelezo.
Na kama hutaki, unaeleza wazi kwamba umeshindwa kufanya kama ulivyoahidi au ulivyotegemewa kwa sababu hutaki. Unawaeleza watu hilo kwa uwazi kabisa, na wala huhitaji kutetea zaidi.
Ni rahisi na inawapunguzia watu usumbufu unapoeleza hutaki kuliko unapotoa sababu nyingine zozote.
Sasa kama unaona siyo sahihi kuwaambia watu sababu ni hutaki, unajua cha kufanya, tekeleza kama ulivyoahidi au kutegemewa.
Kama inakuuma au hujisikii vizuri kuwaambia watu kwamba sababu ni hujataka, peleka maumivu hayo kwenye kutekeleza.
Tekeleza na watu wajionee na siyo kutengeneza sababu ambazo hazina mashiko.
Unapochelewa mahali kisha kueleza sababu ni umekutana na foleni, unadhani unamdanganya nani kwa mfano? Watu makini wanajua kama kweli ungekuwa unataka kuwahi, ungetoka mapema ili foleni isiwe kikwazo kwako.
Lakini kwa sababu hujataka sana kuwahi, umetoka kwa muda ambao foleni inakuchelewesha.
Unaposhindwa kutekeleza kile ulichoahidi na kuja na sababu nyingi za kwa nini umeshindwa, unadhani nani anazipa uzito?
Watu makini wanajua sababu ya kushindwa kutekeleza ni kwa sababu una vipaumbele vingine muhimu zaidi ya hilo uliloshindwa.
Utaona watu wanakuitikia na kuona umewapanga kwa sababu zako, lakini walio makini wanakuchora tu, na wanakuhukumu kwa hayo.
Wanajua wakati mwingine hawawezi tena kukutegemea kwa mambo ya aina hiyo.
Kwa kila jambo unalofanya watu wanalitumia kukuhukumu.
Ni bora ujiumize kwa nidhamu kali kabisa ili uhukumiwe vizuri na kuheshimiwa na kuaminiwa.
Kuliko ujisikie vizuri kwa kukosa nidhamu halafu uhukumiwe vibaya kwa kudharauliwa na kutokuaminiwa.
Huwezi kupata mafanikio makubwa kwenye maisha kama huna nidhamu kali binafsi, ambayo haileti sababu bali matokeo.
Huwezi kuheshimiwa na kuaminika kama huwezi kutekeleza mambo kwa wakati.
Simamia kwa ukali sana maeneo haya mawili; nidhamu binafsi na kujali muda, usiwe wa kukimbilia kutoa sababu kwenye maeneo hayo.
Hilo litakuwezesha kujenga sifa kubwa itakayokupa chochote unachotaka.
Msimamo wako uwe wazi kabisa, watu wakiona hujafanya kile ulichoahidi au unachopaswa, wajue wazi ni labda umekufa au hutaki.
Ifahamike hivyo na usiongeze sababu nyingine yoyote.
Jitese kwenye kukamilisha hilo, maana hakuna namna nyingine.
Ingekuwa sababu zinaleta mafanikio, kila mtu angekuwa na mafanikio makubwa.
Kwa sababu kila mtu ni mtoaji mzuri wa sababu.
Lakini tunajua vyema, sababu hazijawahi kuzalisha matokeo.
Usiwe mtu wa kutoa sababu, kuwa mtu wa kuzalisha matokeo, kuwa mtu wa kuwajibika.
Lazimika kwenda hatua ya ziada ili kutekeleza uliyoahidi au kukamilisha unayopaswa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hii ngumu kumeza lkn cna namna
LikeLike
Dawa chungu ndiyo inayotibu vizuri.
LikeLike
Watu makini wanajua kuna sababu mbili pekee za watu kushindwa kutekeleza wanachopaswa kutekeleza; wamekufa au hawataki.
LikeLike
Sisi tusimame kwenye utekelezaji.
Na ikitokea hatujatekeleza, iwe ni kwamba tumekufa.
Kama tunakuwa hai, tunatekeleza kama tulivyoahidi au kukubali.
LikeLike
Nnapaswa kufanya neno langu kuwa sheria.
Kwamba nikiahidi natekeleza kama nilivyoahidi na siyo kuanza kuleta sababu.
Msimamo wangu uwe wazi kabisa, watu wakiona sijafanya kile nilichoahidi au ninachopaswa, wajue wazi ni labda nimekufa au sitaki.
Sababu za kwa nini sijafanya, NOOOOOOOO. Siyo muhimu, hazihitajiki.
AHSANTE SANA KOCHA DR. MAKIRITA AMANI.
LikeLike
Na tukishakubali au kuahidi, basi swala la kutokutaka halipo, tunabaki na kifo.
Yaani kifo pekee ndiyo kitakachotutenganisha na ahadi zetu.
LikeLike
Asante kocha,ntajitahidi kuzingatia ahadi zangu sio kutanguliza sababu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ahsnate sana kocha, nitakuwa mtu wa kuwajibika na kutoa matokeo na siyo kutoa sababu
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Maneno haya ni magumu na mazito kidogo na yanapaswa kuyagawanya latika vipaumbele vyangu vyote ili kufikia Lengo kuu
LikeLike
Bila ya kujisukuma kwa viwango visivyokuwa vya kawaida, hatutaweza kupata matokeo yasiyokuwa ya kawaida.
LikeLike
Nidhamu binafsi na kujali muda. Asante sana Kocha Dr. Amani Makirita
LikeLike
Karibu.
LikeLike
ni kutekeleza km nilivyoahidi au kutegemewa vinginevyo nimekufa au sitaki
IMENIFIKIRISHA ni bora ujiumize kwa nidhamu kali kabisa ili uhukumiwe vzr kuheshimikana na kuaminika
kuliko ujisike vzr kwa kukosa nidhamu halafu uhukumiwe vibaya na kudharaulika na kutokuaminika
LikeLike
Ukiweza kutekeleza hili kwa ahadi unazowapa wateja wako, utapata kazi mpaka uzikimbie mwenyewe.
Nijaribu kwenye hilo.
LikeLike
Kwa hakika nidham ndio msingi wa mafanikio.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hakuna sababu nyengine nitakayotoa kwenye jambo. Sababu ni mbili tu nimekufa au sitaki.
LikeLike
Ahsante kocha, ni bora nijuhukumu kwa kuwa na nidhamu kali ili watu wani jukumu vizuri kwa uniheshimu na kuaminiwa.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Na kama upo hai, hakuna sababu, ni kufanya tu.
LikeLike
Majibu ni mawili TU ni labda umekufa au hutaki. Hapa Kuna majibu ya vitu vingi sana. Asante sana Kocha.
LikeLike
Kabisa, na tukiwa hai, ni kutoa matokeo tu.
LikeLike
Ahsante kocha, ni bora nijuhukumu kwa kuwa na nidhamu kali ili watu wani jukumu vizuri kwa uniheshimu na kuaminiwa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Sababu na visingizio ni dalili za uzembe na kukosa umakini.
LikeLike
Kabisa.
Ukiwa makini unafanya.
LikeLike
Asante Kocha,nahitaji kuwa na msimamo usiyoyumbishwa Kwa kufanya neno langu kuwa sheria na pia kujali sana muda wangu wangu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kweli nidhamu kali ya kuamua na kufanya bila kutoa visingizio kwenye swala la muda na nidhamu binafsi ni muhimu kwenye kuheshimika
LikeLike
Hakuna mbadala kwenye hilo kama tunataka kupiga hatua kubwa.
LikeLike
Siwezi kuheshimiwa na kuaminika kama sitaweza kutekeleza mambo kwa wakati. Sababu za kutokutimiza nilichoahidi hazikubaliki. Kwani ni sawa na kufa au kukataa kufanya.
Hapa Nidhamu inahitajika kwa kweli!!!!
LikeLike
Nidhamu ya kutisha yani,
Nidhamu ambayo watu wa kawaida wanakuonea huruma.
Lakini wewe unaisimamia,
Kwa sababu unajua nini unataka,
Na umejitoa kupata unachotaka.
LikeLike
Asante kocha
Nikishindwa kutekeleza yale niliyahidi basi niwe nimekufa au niseme tu ukweli kuwa sitaki,na si kutoa sababu yoyote ile mana watu makini hawatasikiliza sababu zangu bali watanidharau na kunihukumu kwa matendo yangu.
LikeLike
Hakika.
Kaa humo.
LikeLike
Nitakamilisha niliyoahidi kufanya bila kutoa sababu yoyote!
LikeLike
Vizuri.
Anzia hapo na usimame humo.
LikeLike
Nitakwenda hatua za ziada Ili kukamilisha nilichoahidi,kufika Kwa wakati kwenye miadi na kujituma sana Ili nizidi kuaminika na kutegemewa.
Sababu ni mbili tu
Nimekufa au
Sitaki.
Na sihitaji kutoa maelezo zaidi
LikeLike
Na kama uko hai, hakuna sababu.
Inahitaji kujitoa na kujitesa sana.
Lakini hakuna namna.
LikeLike
Sababu ni ushahidi kama wewe huwezi.
LikeLike
Tusiwe watu wa sababu, bali watu wa matokeo.
LikeLike
Umekufa au hutaki….sababu hazileti matokeo
Asante
LikeLike
Ukisharuhusu sababu, huwezi kupata matokeo.
LikeLike
Hàkuna sababu Ila nidhamu kubwa itatuweka salama na kutuheshimisha. Kweli hata mie huwa nafsi inanisuta kuwa kwanini sikuweka kipaumbele Cha kutosha na kutimiza nilichoahidi. Ingekuwa ninatafuta pumzi au jicho he ningeruhusu Hali hiyo itokee.??
Ukweli nin uzembe tu na kuvipa ushindi visingizio.
LikeLike
Tusiruhusu visingizio.
LikeLike
Sababu hazizalishi matokeo, fanya au kama hutaki sema hutaki huna sababu mbili zaidi ya hizi kama uko hai.
LikeLike
Tuache kujidanganya kwa visingizio.
LikeLike
Asante Sana kocha, ninaahidi kuzingatia Sana kuwa na
NIDHAMU BINAFSI kwa kutotoa sababu za kushindwa kutimiza kile nilicho ahidi kutimiza . PIA NITAJARI MUDA , asante .
LikeLike
Tuonyeshe matokeo, siyo sababu.
LikeLike
Natamani kuwa mtu wa matendo kuliko maneno,neno langu kuwa sheria kwangu ndiyo muhimu sana!
LikeLike
Nimemuelewa vizuri sana Kocha . Ni kutekeleza au kufa tu.
Asante sana Kocha
LikeLike