2981; Fanya kinachopaswa kufanyika.
Rafiki yangu mpendwa,
Ili uweze kupata matokeo makubwa unayoyataka, lazima ufanye mambo mapya, makubwa na magumu.
Na ili uweze kufanya mambo hayo magumu, lazima ujitoe kafara.
Unapaswa kufanya kinachopaswa kufanyika na siyo unachotaka kufanya au unachoweza kufanya.
Unapaswa ujitoe kupitiliza na siyo kujiwekea ukomo wa nini unaweza na nini huwezi.
Ni mambo magumu yanayokutaka uteseke sana kwenye kuyafanya.
Lakini hata ukiyafanya kwa kuteseka, bado haimaanishi mafanikio yako ni uhakika.
Na hapo ndipo wengi hukwama.
Wengi hujiambia vipi kama wakijitoa sana na bado wasipate wanachotegemea, si watakuwa wamejitesa bure?
Wote walioshindwa ndiyo huwa wanawaza hivyo na ndiyo maana wameishia kushindwa.
Waliofanikiwa huwa wanawaza tofauti.
Wanawaza kwamba wajibu wao ni kujitoa kwa kila namna kwenye kufanya kile wanachopaswa kufanya, bila kujali matokeo yatakujaje.
Wanajua kilicho kwenye udhibiti wao ni hatua wanazochukua na siyo matokeo yanayokuja.
Wanaofanikiwa kuna nyakati wanajitoa kweli kweli na bado hawapati matokeo bora.
Lakini kwa kuwa hawakati tamaa, kwa kuendelea kufanya wanakuja kukutana na matokeo bora kabisa baadaye.
Hakuna matokeo yoyote makubwa ambayo yamewahi kupatikana kwa kufanya vitu vya kawaida.
Mafanikio yoyote yale yanataka mtu ujitoe sana kafara, uache vitu unavyopenda na ujiumize hasa.
Machozi, jasho na damu huwa vinaambatana na mafanikio yoyote makubwa.
Kama unafikiri kuna namna ya kukwepa haya na bado ukapata mafanikio makubwa, unajidanganya.
Maisha ni kuchagua mateso,
Kuwa tajiri kuna mateso yake, katika kuutafuta, kuutunza na hata kuukuza utajiri.
Na hata kuwa masikini pia kuna mateso yake, kuishi kwa kukosa yale muhimu unayotaka.
Tofauti kwenye maisha zinaletwa na mateso gani ambayo mtu yupo tayari kuyavumilia.
Pale unapotaka kitu chochote kile kwenye maisha yako, kuwa tayari kujitoa kupitiliza katika kukiendea.
Usijizuie wala kujionea huruma, jitoe hasa kwa kuhakikisha unafanya kila unachopaswa kufanya.
Usijali matokeo gani yatakuja, wewe fanya kwanza.
Ili uweze hilo ni lazima uache kujali watu wanasema au kukuchukuliaje.
Watu wa kawaida huwa wana tabia ya kuwacheka wale wanaojaribu makubwa halafu wakashindwa.
Sasa kama utajali hilo, hakuna chochote kikubwa utakachoweza kufanya, kwa sababu watu wa kawaida huwa hawana kazi nyingine zaidi ya kuhangaika na mambo ya wengine.
Wewe jali mambo yako, fanya unachopaswa kufanya bila kujali unaumia kiasi gani au wengine wanakuchekaje.
Kuna siku utakuwa unachekelea, wakati wao wanalia.
Na pia kumbuka, wengi wanaokucheka pale unaposhindwa, wanatumia hiyo kama fursa ya kujipooza na mateso makali wanayokuwa wanapitia.
Hakuna mtu mwenye furaha na maisha yake anafurahia kushindwa kwa mtu mwingine.
Hivyo badala ya kuwazingatia watu wa aina hiyo na ukaacha kufanya unapaswa uwaonee huruma kwa mateso makali wanayopitia, kiasi kwamba raha pekee kwao ni kuona wengine nao wanateseka.
Hata wale unaoona wanatumia nguvu nyingi sana kuonyesha wana furaha, labda kuweka mambo yasiyo halisi kwenye mitandao ya kijamii, kufanya starehe kupitiliza na mengine, hawafanyi hivyo kwa sababu wana furaha sana, bali wanafanya hivyo kwa sababu wanataka kuficha mateso makali wanayopitia.
Zote hizo ni sababu za msingi sana kwa nini unapaswa kujitoa kweli kwenye kile unachotaka bila kujali wengine wanafanya nini au wanakuchukuliaje.
Huwa wanasema mafanikio ni kama tai, mara nyingi utalazimika kuruka mwenyewe hata kama mazingira ni hatarishi kiasi gani.
Ingekuwa rahisi kila mtu angefanya na ingekosa thamani.
Ni ngumu ndiyo maana wengi hawafanyi na thamani yake inakuwa kubwa.
Usitake iwe rahisi, bali pambana wewe uwe mgumu.
Endelea kufanya kila kinachopaswa kufanyika. Ndiyo njia pekee ya kujenga na kutunza mafanikio makubwa unayoyataka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kuwa masikini Nako ni zaidi ya mateso. Nitakaa kwenye mchakato na majibu sahihi yatakuja Kwa wakati sahihi.
LikeLike
Ahsante kocha.
Kila kitu ni mateso umaskini unatesa na utajiri una mateso yake.
Chagua mateso sahihi kwako?
LikeLike
Ahsnate sana kocha nitaendelea kufanya kwa nidhamu hata kama sioni matokeo kwasasa
LikeLike
Asante kocha,mambo magumu na kutokata tamaa ndo njia kuu ya uhuru wa kifedha.
LikeLike
Ili kuyafikia mafanikio makubwa ninayoyataka kwenye maisha yangu napaswa kufanya kile kinachopaswa kufanyika,na mafanikio makubwa yangekua rahisi yasingekua na thamani.
Chenye thamani siku zote kinakua na gharama,ugumu na ili kukipapata mateso hayaepukiki.
LikeLike
Umaskini una mateso, utajiri una mateso. Chagua mateso utakayovumilia na ukae hapo.
LikeLike
Ahsante sana Kocha Dr Makirita Amani kwa makala nzuri ya leo ya kubaki kwenye mchakato kwa kufanya kile tu unachopaswa kufanya bila ya kujali matokeo.
Ahsante sana ✍️✍️✍️
LikeLike
kilicho kwenye udhibiti wangu ni hatua ninazochukua na siyo matokeo yanayokuja. Asante sana Kocha Dr. Makirita Amani
LikeLike
Furaha ya kweli haitokani na raha za muda mfupi bali kuweka kazi kubwa na ngumu kwa muda mrefu.
LikeLike
Nitaendelea kufanya kile ninachopaswa kufanya na siyo ninachotaka au nilichojipangia naweza.
Naamini bila ya shaka yoyote hakuna kinachoshindikana kwenye kuweka bidii Kwa msimamo ya kufanya kile ninachopaswa kukifanya.
LikeLike
Ni kweli Dr Kocha Makirita Amani. Mafanikio ni km Vile Tai.kuna wakati utapaswa kuruka mwenyewe
LikeLike
Ingekuwa rahisi kila mtu angefanya na ingekosa thamani.
Ni ngumu ndiyo maana wengi hawafanyi na thamani yake inakuwa kubwa.
Usitake iwe rahisi, bali pambana wewe uwe mgumu.
Asante sana
LikeLike
Maisha ni kuchagua mateso
Kuwa tajri Kuna mateso yake na kuwa maskini Kuna mateso yake
LikeLike
Nitafanya nachopaswa kufanya bila kujali watu wanasemaje au kufikiri nini!
LikeLike
Sitajisumbua wengine Wanafikiri au kunichuliaje, nitafanya kilicho sahihi.
LikeLike
Vizuri sana
LikeLike
naendelea kufanya kinachopaswa kufanyika
ndio njia pekee
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kweli inahitajika kujitoa haswa ili kufikia malengo makubewa ambayo mtu umepanga kufikia kwenye maisha kwa ujumla wake mpana na kutimiza malengo kwa ujumla, lazima kupitia mateso
LikeLike
Tunapaswa kujitoa sana.
LikeLike
Nitafanya kinachopaswa kufanyika na siyo ninachotaka kufanya.asante kocha
LikeLike
Safi
LikeLike
Napaswa kufanya kinachopaswa kufanyika na siyo ninachotaka kufanya au ninachoweza kufanya.
Napaswa kujitoa kupitiliza na siyo kujiwekea ukomo wa nini naweza na nini siwezi.
Ahsante sana Kocha Dr. Makirita Amani.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Maisha ni kuamua ujitese sasa ili kesho upate unafuu au upate unafuu sasa kisha mateso baadae
LikeLike
Wengi hawaelewi hili.
LikeLike