2982; Kupangiwa cha kufanya.
Rafiki yangu mpendwa,
Tunajua maisha ni magumu na yana changamoto za kila aina.
Lakini sehemu kubwa ya ugumu wa maisha huwa tunaisababisha sisi wenyewe.
Hasa kutokana na matarajio tunayokuwa nayo kwenye yale tunayofanya.
Kwenye kila eneo la maisha, ugumu na urahisi huwa vinapishana.
Chochote ambacho tunakifanya kwa urahisi huwa kinakuwa kigumu na chochote ambacho tunakifanya kwa ugumu huwa kirahisi.
Tuchukue mfano wa biashara, watu wengi huwa wanaingia kwenye biashara kwa kuona itakuwa kitu rahisi kwao kufanya.
Wanaona watakuwa huru kufanya kile wanachotaka kwa namna wanavyotaka.
Wengi hujinasibu kabisa kwamba hakutakuwa na wa kuwapangia nini wafanye.
Mtazamo huo unafanya mambo yawe magumu sana.
Kwa sababu mtu anaianza biashara kama vile tayari ameshafanikiwa.
Akichagua nini afanye na nini asifanye.
Na kuona hakuna anayepaswa kumpangia kitu cha kufanya.
Matokeo ya hayo ni mambo kuwa magumu na hata biashara kushindwa.
Kushindwa kuweka juhudi sahihi kunakopelekea matokeo bora yasipatikane.
Kwa sababu mtu anapokuwa kwenye biashara anakuwa bosi wake mwenyewe, ambaye anaamua yeye mwenyewe atumieje muda wake, ni muhimu sana akawa na nidhamu kali binafsi.
Mtu anayeingia kwenye biashara na kuwa tayari kutoa muda wake kwa kila jambo bila kujali umuhimu wake, anayetaka kumfurahisha kila mtu, hawezi kupata mafanikio makubwa.
Ni yule anayekuwa mgumu kwake yeye mwenyewe, akijisimamia kufanya yaliyo sahihi na muhimu hata kama siyo anayopendelea kufanya ndiye anayefanikiwa.
Tumekuwa tunaona watu wengi wakifanya vizuri wanapokuwa wameajiriwa, kwa sababu wanapangiwa cha kufanya na kulazimika kukifanya hata kama hawataki.
Lakini watu hao hao wakienda kujiajiri wenyewe au kufanya biashara wanashindwa vibaya kwa sababu wanakuwa hawana wa kuwapangia cha kufanya na wao wenyewe hawawezi kujisukuma wafanye magumu wasiyoyapenda.
Hilo linafanya wahangaike na yaliyo rahisi na yasiyo na tija, kitu kinachopelekea kushindwa.
Kama mfanyabiashara mwenye uhuru na muda wako, hakikisha unaweza kujipangia kufanya mambo magumu na usiyoyapenda na kuyafanya kwa viwango vya juu kabisa.
Kama huliwezi hilo peke yako, tafuta mtu (Kocha) au watu (Kikundi cha uwajibikaji au bodi) ambao watakupangia cha kufanya na utafanya bila ya ubishi.
Kabla ya kuingia kwenye biashara, kila mtu huona biashara ni rahisi na mafanikio ni ya uhakika.
Lakini kila mtu anapoingia kwenye biashara mambo yanabadilika, zinakuwa ngumu na mafanikio hayaonekani.
Tatizo linaanzia kwenye kuingia na mtazamo huo wa urahisi na hivyo kufanya kila kitu kwa urahisi.
Matokeo yake ni unazalishwa ugumu ambao unakuwa ni kikwazo kikubwa.
Ukitaka mambo yako yaende kirahisi, anza kwa kuwa mgumu kwako wewe mwenyewe.
Hilo litakusukuma kufanya yaliyo magumu na sahihi badala ya kukimbilia yaliyo rahisi.
Na kama unajitapa hutaki kupangiwa cha kufanya, kwa sehemu kubwa umeshapotea.
Kinachoweza kukuokoa ni nidhamu kali binafsi, nidhamu ambayo wengine wanaona unajitesa.
Nje na hapo hutoboi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsante kocha.
Inabidi wakuone unajitesa. Nje na hapo hutoboi.
LikeLike
Jamii imekuwa laini sana, tukienda nayo tutaanguka vibaya.
LikeLike
Hakika, kama huna NIDHAMU kali ya kuamua na kufanya ni ngumu kutoboa.
Asante sana
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitaongeza kiwango cha nidhamu binafsi na kupanga mambo magumu ya kufanya pasipokuwa na visingizio
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Makala inafikirisha ni kweli inahitajika kazi kweli na lazima uwajibikaji kwenye kufikia malengo makubwa siku zote, hakuna kukwepa usimamizi
LikeLike
Hilo ni muhimu sana.
LikeLike
Asante sana kwa ushauri huu ni bora kuwa mgumu kwako binafsi
LikeLike
Lazima ianzie kwetu wenyewe
LikeLike
Ukitaka mambo yako yaende kirahisi, anza kwa kuwa mgumu kwako wewe mwenyewe
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha
Nidhamu kali na kujitesa kwa kufanya yale yanayopaswa kufanyika bila kujali napitia changamoto gani ndio kutaniwezesha kufanikiwa katika biashara yangu,kinyume na hapo siwezi kutoboa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,nidhamu ya kazi na kujitesa ndo njia ya kufikia malengo.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Tutaweza kuokoka na mtego kwa kuwa na nidham kali binafsi is
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitafanya yaliyo magumu na sahihi bila kujali jamii inavoniona!
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ni kweli bila nidhamu binafsi utakua haujajitendea haki wewe binafsi wacha waone unateseka lakini unajua unachokifanya wao watajionea baadae wakati uko mbali
LikeLike
Hawaoni unachoona.
LikeLike
Asante, Nidhamu Kali binafsi ambayo wengine wanaona ninateseka ndiyo itakayoniokoa.
LikeLike
Bila shaka.
LikeLike
Ukitaka mambo yako yaende kirahisi, anza kwa kuwa mgumu kwako wewe mwenyewe.
Hilo litakusukuma kufanya yaliyo magumu na sahihi badala ya kukimbilia yaliyo rahisi. Tofauti na hapo hutoboi.
Asante daktari Makirita Amani.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Pigheaded discipline and determination.
LikeLike
Lazima kuwa kichwa ngumu kweli kweli.
LikeLike
Hakika kocha, Kitu cha msingi ni, Kuchagua unateseka kwanza kwa sababu Gani, then unaweka nidhamu kali kweli kweli ya Kufanya kwa msimamo mpaka unapata unachotaka.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakika kitu pekee kwenye maisha ni kuweka Nidhamu kubwa kwenye maisha na ndio pekee
LikeLike
Hilo halina ubishi.
LikeLike
Nidhamu kali kwangu mwenyewe ya kufanya yale yasiyofurahisha ndiyo itakayonivusha.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Changamoto za kimaisha nyingi husababiswa na sisi wenyewe , kwa kutarajia mafanikio makubwa bila kuweka juhudi za dhati.
Wanaofanikiwa ni wale wanajisimamia kufanya yalio sahihi hata Kama hawapendi kufanya hivyo.
(Greatest)
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nahakikisha naweza kujipangia kufanya mambo magumu na nisiyoyapenda na kuyafanya kwa viwango vya juu kabisa.
Kwa kutafuta mtu (Kocha) au watu (Kikundi cha uwajibikaji au bodi) ambao watanipangia cha kufanya na nitafanya bila ya ubishi.
Asante
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Uhuru wa muda ni kuwa na nidhamu Kali binafsi ya kupanga na kuamua kufanya bila kuacha.
Ukitaka mambo yako yaende kirahisi, anza kwa kuwa mgumu kwako wewe mwenyewe.
Hilo litakusukuma kufanya yaliyo magumu na sahihi badala ya kukimbilia yaliyo rahisi.
Huu no msingi mkuu unatakiwa kuuamini na kuuishi milele.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nahitajika kuweka nidhamu kali ya kupanga na kufanya.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nahitajika kuweka nidhamu kali ya kupanga na kufanya. Asante sana Kocha.
LikeLike
Naanza Kwa kukuwa mgumu kwangu mwenyewe.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ili uweze kupata mafanikio kwenye kile unachofanya unatakiwa kuwa na nidhamu Kali ya kuamua na kufanya
Asante
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Nakuwa mgumu kwangu, nakaa kwenye mchakato, ni swala la muda tuu Juhudi hazipotei Bure.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nidhamu kali ndiyo msaada wangu,nje na hapo sitoboi
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Nikitaka mambo yangu yaende kirahisi, nianze kwa kuwa mgumu kwangu mwenyewe.
Hilo litanisukuma kufanya yaliyo magumu na sahihi badala ya kukimbilia yaliyo rahisi.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kama huwezi kujisimamia kuwa na kocha au bodi ya wakurugenzi
LikeLike