2984; Yai na kuku.
Rafiki yangu mpendwa,
Unakumbuka ubishani ambao tulipenda kuwa nao tulipokuwa watoto?
Kwamba kati ya yai na kuku kipi kilianza?
Ukisema yao ndiyo lilianza, swali linakuwa yai hilo lilitoka wapi kama siyo kutagwa na kuku?
Na ukisema kuku ndiye alianza, swali linakuwa kuku huyo alitoka wapi bila ya yai?
Ni ubishi fulani unaoweza kuonekana wa kijinga na kitoto, lakini unaelezea vyema mkwamo ambao tunakuwa nao mara nyingi kwenye maisha yetu.
Mkwamo ambao tusipoamua kuchukua hatua fulani, tunabaki tukiwa tumekwama kwa muda mrefu.
Tuchukue mfano mzuri wa mkwamo ambao watu wengi wamekuwa nao kwenye biashara, hasa kwenye mauzo.
Ili uweze kukuza mauzo kwenye biashara, unahitaji kuwa na timu.
Lakini wengi wanashindwa kuwa na timu, kwa sababu hawawezi kuilipa.
Na ili uweze kuilipa timu, lazima uwe na mauzo makubwa.
Unauona mkwamo hapo, unajiambia sababu ya kutokuwa na timu ni kutokuweza kuilipa.
Lakini pia unahitaji kuwa na timu ili uweze kufanya mauzo makubwa na kuweza kuilipa timu.
Usipochukua hatua mahali, unaishia kubaki na biashara ambayo imekwama kwenye maeneo yote mawili.
Inakuwa haina timu kwa sababu huwezi kumudu kuilipa.
Na wakati huo huo inakuwa haina mauzo makubwa kwa sababu haina timu.
Kuvunja hilo unapaswa kuanza na timu kama uwekezaji kwenye biashara.
Kuwekeza malipo ya awali kwa timu hiyo wakati bado biashara haiwezi kumudu.
Kisha kuongoza, kusimamia na kufuatilia timu hiyo vizuri ili iweze kukuza mauzo na iweze kumudu kujilipa yenyewe.
Usijikwamishe kwa ubishani usiokuwa na mwisho, chagua sasa kuingilia mahali, ambapo rahisi ni kuwekeza kwenye timu.
Unaweza kuwa unajiuliza kwa nini kwanza usikuze mauzo kabla ya kuwa na timu ili timu ikifika iweze kujilipa na kuendelea kukuza mauzo.
Jibu ni kuna ukomo utakaofikia kwenye kukuza mauzo kama hutakuwa na timu.
Hivyo kwa vyovyote vile, ni muhimu ujenge timu, ambayo ukiiwekea kazi vizuri, lazima iweze kujilipa.
Chukua mfano tayari biashara yako ina wateja 100 ambao wamewahi kununua katika kipindi chochote kile.
Je ni wangapi ambao huwa wanatudi kununua mara kwa mara?
Na je wangapi ambao wamewahi kukuletea wateja wengine zaidi?
Kwa wateja hao 100 tu waliopo, bado unaweza kuuza zaidi na kupata wateja wengi zaidi.
Lakini hilo litahitaji uwafanyie hao kazi kubwa, uwape huduma nzuri, uwafuatilie kwa karibu na kuwajua kiundani.
Peke yako hutaliweza hilo na hivyo unajikuta ukipoteza fursa nyingi za kuuza zaidi kama huna timu ya uhakika.
Mkwamo wowote ule unaojikuta umeingia kibiashara jiulize ni uwekezaji gani unapaswa kufanya ili kuweza kuondoka kwenye mkwamo huo.
Kwa sababu bila uwekezaji, wa muda, fedha na ujuzi, mengi sana yanakwama kibiashara.
Usiseme kipi biashara inaweza na kipi haiwezi, biashara inaweza kila kitu iwapo uwekezaji sahihi utapatikana.
Piga hesabu zako vizuri kwa kila uwekezaji utakaofanya ni marejesho gani unayotegemea.
Kisha fanya uwekezaji huo na fuatilia kwa karibu uyapate marejesho unayoyataka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsnate kocha nitawekeza katika timu ili kukuza mauzo
LikeLike
Nakubaliana na hilo
LikeLike
Vizuri, chukua hatua.
LikeLike
Vizuri kwa mpango huo.
LikeLike
Ahsante kocha.
Kwa kila mkwamo, jiulize ni uwekezaji gani unapaswa kufanya kwenye biashara ili kuvuka mkwamo huo.
LikeLike
Hakika, uwekezaji sahihi unakuvusha kwenye mkwamo wowote ule.
LikeLike
Mauzo yanatibu kila kitu kwenye biashara. Asante sana
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Biashara inaweza kila kitu endapo uwekezaji sahihi utafanyika.kujenga timu,timu chapa kazi kukuza mauzo kuleta fedha nyingi kwa biashara.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nachagua kuwekeza kwa timu
LikeLike
Umechagua vyema.
LikeLike
Asante kocha kweli kila kitu kinawezekana muhimu kuchukua hatua kubwa
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ahsante sana Kocha Dr Makirita Amani kwa makala bomba kabisa na uzi makini sana wa Leo.
Nitawekeza fedha zangu katika timu, Ili kuboresha na kukuza mauzo zaidi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ni kweli kila mkwamo wa biashara unaletwa na mauzo kuwa duni na mauzo kuwa duni sababu ni uwekezaji mmbovu wa team jambo la msingi hapo ni kuboresha team kwa kuwekeza kwao
LikeLike
Tutegue hicho kitendawili.
LikeLike
Ni kweli lazima tufanye maamuzi magumu
LikeLike
Hilo halikwepeki.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza: bila uwekezaji sahihi wa muda, fedha na ujuzi mambo mengi yanakwama kwenye biashara.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana Kocha
Nimefanya uwekezaji ktk biashara yangu i.e Sales Team, Mafunzo ya Chuo cha mauzo na Coaching services. Naamini nitafanikiwa sana kwa kukaa kwenye mchakato kwa msimamo bila kuacha.
LikeLike
Hakika, ni kukaa kwenye mchakato na kuupa muda uwekezaji uliofanya uweze kuzalisha matokeo bora kabisa.
LikeLike
Ni uwekezaji wa muda,fedha,ujuzi na uwekezaji nyingine muhimu Ili niondokane na mkwamo kwenye biashara.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Uwekezaji kwenye timu unaweza kuzaa matunda ikiwa nitawekeza Kwa watu sahihi
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Ukubwa wa biashara unaendana na Ukubwa wa timu.
LikeLike
Kama ulivyo mchezo wowote, ushindi unategemea sana timu.
LikeLike
Ahsante Kocha.
Kuwa na timu siyo hiari, ila ni lazima.
Kutokuwa na timu ni kujifungia ndani ya box.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ili kujikwamua kwenye mkwamo wa mauzo duni ni kujenga timu Bora , na hapo utapata mauzo bora
Asante kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Ili tuweze kufanikiwa kwenye biashara kuweza kupata mauzo makubwa lazima kwanza tufanye uwekezaji hasa wa timu ya kufanya nao kazi
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Bila kuwekeza kwenye timu kukuza mauzo ni changamoto,nawekeza kwenye timu ili niweze kukuza biashara na mauzo
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kweli kocha huu Ni mtego. Namna pekee ya kuupuka ni kuamua kukata mnyororo na kusongambele
LikeLike
Asante sana kocha hasa uliposema kutumia timu kama sehemu ya uwekezeji.
LikeLike
Kujali maslahi ya timu kwanza kabla ya biashara kuanza kufanya mauzo makubwa ndio Uwekezaji Bora unaweza kufanya kwenye biashara na marejesho yakawa makubwa zaidi kwa maana ya kuongeza mauzo maradufu kutokana na timu Bora.
LikeLike