2996; Fanya vitu vya maana.
Rafiki yangu mpendwa,
Sisi binadamu tuna rasilimali tatu ambazo zina uhaba mkubwa sana.
Rasilimali hizo ni muda, nguvu na umakini.
Hizo ni rasilimali ambazo ukishaziweka kwenye kitu kimoja, huwezi kuziweka tena kwenye kitu kingine.
Chochote unachofanya kwenye maisha yako, lazima utahusisha rasilimali hizo tatu, utaweka muda wako, utamia nguvu za mwili na umakini wa akili yako.
Hivyo basi, kama unakwenda kufanya kitu, basi hakikisha ni kitu cha maana kweli kwako wewe kufanya.
Fanya kitu ambacho kinaleta tofauti kubwa kwako na kwa wengine pia.
Fanya kitu ambacho utajivunia kweli ni matumizi sahihi ya rasilimali zako muhimu na matokeo yake kuwa yenye manufaa makubwa kwa kila anayehusika.
Muda wetu ni mfupi sana hapa duniani.
Nguvu za miili yetu zinapungua kadiri tunavyozitumia.
Na umakini wa akili zetu hauwezi kwenda kwenye mambo mengi kwa wakati mmoja.
Swali muhimu la kujiuliza ni unakwenda kutumiaje rasilimali hizo muhimu sana kwako ambazo zina uhaba mkubwa?
Jibu sahihi ni kutumia rasilimali zako adimu kwenye mambo ya maana, mambo ambayo ni muhimu zaidi na yenye mchango kwako na kwa wengine pia.
Mambo ya maana kufanya ni yale yanayoacha maana fulani kwa kila anayehusika.
Mambo ambayo ukiangalia nyuma unaona mchango wake kwenye hatua ambazo mtu umepiga.
Hiyo ndiyo njia sahihi ya kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Ndiyo njia sahihi ya kutoa thamani kubwa kwa wengine na wewe mwenyewe kupokea thamani kubwa pia.
Ni rahisi sana mambo yasiyo muhimu kuteka rasilimali zako tatu muhimu na kujikuta zinapotea bila manufaa.
Kuna mengi sana yanayowinda rasilimali hizo muhimu, mambo ambayo hayana tija yoyote.
Ni muhimu sana kila wakati kujikumbusha nini unafanya na kina umuhimu kiasi gani.
Unafanya hivyo kwa kujiuliza mara kwa mara, je hiki ninachofanya sasa ndiyo kitu cha maana zaidi kuliko vingine ambavyo ningeweza kuvifanya?
Kama jibu ni ndiyo endelea kufanya, lakini kama jibu ni hapana, acha mara moja kufanya na uende kwenye kile cha maana zaidi.
Maisha ni kuchagua,
Maisha ni vipaumbele,
Maisha siyo kufuata mkumbo.
Weka vipaumbele vyako kwa usahihi na vifuate vipaumbele hivyo bila kuyumbishwa na mengine yasiyo na maana.
Kila utakachofanya kwenye maisha yako, kitatumia muda, nguvu na umakini wako.
Hivyo badala ya kupoteza rasilimali hizo adimu kwenye mambo yasiyokuwa na tija, ni bora kuhakikisha unapeleka rasilimali hizo kwenye mambo ya maana zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hakika kocha.Na yale mambo yasiyo ya maana kwanza ni marahisi kufanywa na kila mtu,na yanakula umakini wetu na nguvu na muda wetu sana.
Ndiyo maana ni muhimu kuwa na vipaumbele kwenye siku yetu kuepuka kutawanya vitu hivyo vitatu kwenye mambo yasiyo ya maana marahisi kufanya
LikeLike
Bila vipaumbele tutasumbuka sana.
LikeLike
Kila unachofanya jiulize hiki ndio kitu sahihi kuliko vingine.
Ahsante
LikeLike
Mara nyingi tunakimbilia rahisi badala ya sahihi.
LikeLike
Umakini wetu Kwa sasa ndiyo bidhaa ya ghali sana.
LikeLike
Unawindwa na wengi sana.
LikeLike
Muda,nguvu na umakini.Hizii ni rasilimali adimu ambazo napaswa kuzitumia vyema.
LikeLike
Hakika, ukizitumia vibaya utakwama sana.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa hakika kuna vitu vingi sana vinawinda rasilimali zangu muhimu ni lazima kujiuliza kila wakati kuhusu matumizi ya muda, nguvu na umakini.
LikeLike
Hakika, tusipozijali hizi rasilimali watu watazitumia hovyo na kutupoteza.
LikeLike
Muda, nguvu na umakini.
LikeLike
Tukidhibiti hivyo vitatu tutaweza kufanya makubwa sana.
LikeLike
Muda, nguvu na umakini ni rasilimali ambazo siwezi kuzitawanya. Nitazielekeza kwenye mambo ya maana.
LikeLike
Hilo ndiyo jambo la msingi.
LikeLike
Kwa hakika nitakuwa nafanya vitu vya maana
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahsante sana kocha nitafanya yale yaliyo muhimu kwaajili ya biashara yangu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Natumia rasilimali muda ,akili na umakini wangu kwa mambo yenye tija katika maisha yangu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha,ntajitahidi kutumia nguvu,muda na umakini kwenye mambo yenye maana.
LikeLike
Tukae humu.
LikeLike
Rasilimali muhimu kwenye maisha yangu.
Muda, nguvu,na umakini kwenye mambo yangu.
Hivyo kuwa makini na hizi rasilimali 3. Muda unapotea. Nguvu zinaisha na weka umakini kwa kila chenye manufaa ambacho kitawacha alama kwenye maisha yako.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana kocha, nitalinda sana nguvu zangu,umakini na muda ili viwe na tija kwenye biashara na maisha yangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Muda, nguvu na umakini zikiwekwa kenye yale yaliyo muhimu sana yanazalisha matokeo kwa uhakika.
nitaweka muda, nguvua na umakini katika yale yanayo nipeleka katika ubilionea.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kocha,
“Mambo ya maana kufanya ni yale yanayoacha maana fulani kwa kila anayehusika” This is very powerful!
LikeLike
Thank you.
LikeLike
Ili kutumia vyema rasilimali zangu zenye uhaba ambazo ni Muda, nguvu na Umakini wangu lazima niweke vipaumbele vya kufanya Yale yaliyo muhimu zaidi na maana zaidi Kwa maisha yangu.
Asante Kocha.
LikeLike
Vizuri sana, kaa humo.
LikeLike
Muda, Nguvu na Umakini rasilimali adimu, nitazitumia kutengeneza thamani kwa ajili yangu na wengine pia.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana.
Nita hakikisha nina tunza na kilinda rasilimali zangu muhimu i.e muda, nguvu na umakini kwa uadilifu mkubwa ili kuongeza thamani na kufikia malengo niliyo nayo ya Ubilionea.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nita hakikisha nina tunza na kilinda rasilimali zangu muhimu i.e muda, nguvu na umakini kwa uadilifu mkubwa ili kuongeza thamani na kufikia malengo niliyo nayo ya Ubilionea. 🙏🏽
LikeLike
🔥
LikeLike
Badala ya kupoteza rasilimali hizi adimu;nguvu,muda na umakini kwenye mambo yasiyokuwa na tija kwako ni bora nitumie kwa mambo yenye tija kwangu na yenye kugusa maisha ya wengine pia. Asante sana Kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kwa Chochote nachofanya natakiwa kuangalia kama kina maana yoyote ikiwa na kina mchango wowote katika vipaumbele nilivyiweka ili kufikia ndoto zangu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Tupeleke nguvu muda na umakini kwenye vitu vinavyotupeleka kule Tunapataka
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ni muhimu kutunza nguvu na muda na kupeleka kule kwenye matokeo tunayoyahitaji
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Ni ngumu kuuweka umakini wako kwenye kitu kimoja kwa dunia hii ya utandawazi.
LikeLike
Lakini inawezekana.
LikeLike
Hiki ninachokifanya sasa ndicho cha muhimu kuliko mengine yote ambayo ningeweza kufanya? Hili ni swali muhimu sana la kujiuliza kabla ya kufanya kitu chochote.
LikeLike
Kabisa, haina maana ya kuwa bize kwa mambo yasiyo na tija.
LikeLike
Natumia rasilimali zangu muhimu ambazo Ni muda, juhudi na umakini kwenye vitu vya maaana. Shukurani Sana kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike