2997; Wingi na ubora.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye kila kitu tunachofanya, kuna njia mbili za kukiendea; wingi na ubora.
Kwenye wingi unaangalia namba.
Na kadiri namba inavyokuwa kubwa, ndivyo matokeo yanavyokuwa mazuri pia.
Kwenye ubora unaangalia viwango.
Kadiri viwango vinavyokuwa vya juu, ndivyo matokeo yanavyokuwa mazuri.
Kwa bahati mbaya sana wingi na ubora haviwezi kwenda pamoja.
Ukiangalia wingi, inabidi uachane na ubora, maana vilivyo bora huwa siyo vingi.
Kadhalika ukiangalia ubora inabidi uachane na wingi.
Unapokuwa unaanza kwenye jambo lolote lile, utaanza kwa kuzingatia wingi.
Lakini kadiri unavyokwenda, utahamia kwenye kuzingatia ubora.
Kuanza na wingi kunakufikisha kwenye ubora kwa urahisi zaidi kuliko kuanza na ubora.
Tuangalie mfano wa mauzo.
Unapokuwa unaanza biashara, unakuwa huna wateja kabisa.
Hivyo mwanzo unaanza kwa kukazana kuwafikia wateja wengi zaidi ili uweze kufanya mauzo makubwa.
Kwa wateja wengi unaowafikia, manunuzi yao hayalingani. Lakini mwanzo watakuwa wanachukua nguvu zako kwa usawa.
Na hapo ndipo unapohitaji kubadilika na kuzingatia zaidi ubora kuliko wingi.
Hapo unaangalia wateja wachache wanaofanya manunuzi makubwa zaidi. Kwa kuwajua hao na kuwapa huduma bora zaidi, unapata fursa ya kuwauzia kwa wingi zaidi.
Kwa lengo lolote la mauzo ulilonalo, kuna wateja wachache bora wanaoweza kukufikisha kwenye lengo hilo.
Kama lengo ni kuuza milioni 100, unaweza kuuzia wateja elfu 1 wanaonunua kwa wastani wa laki moja, au wateja 100 wanaonunua kwa miloni 1, au wateja 10 wanaonunua kwa milioni 10.
Ipi rahisi na ipi sahihi?
Kwa haraka haraka inaonekana kuwauzia wengi ni rahisi kufikia lengo kuliko wachache.
Lakini kama tunavyojua, rahisi siyo sahihi na sahihi siyo rahisi.
Unaweza kuona kuwauzia wengi inarahisisha kufikia lengo.
Lakini kuwahudumia wengi hao kwa viwango vya juu kabisa unavyotaka siyo rahisi.
Pia kupata wengi waaminifu siyo rahisi, kuna ambao utakuwa tayari kuwapa zaidi, lakini akitokea mshindani wako, wanakuwa tayari kukimbilia kwenda kujaribu kwa mshindani na kukuacha wewe.
Kuangalia ubora kunaonekana ni kugumu, lakini ndiyo kuliko sahihi.
Hiyo ni kwa sababu idadi ndogo unaweza kuihudumia kwa ukaribu zaidi na kutoa thamani kubwa ambayo pia italeta marejesho makubwa.
Ugumu wa ubora ni kwenye kuufikia.
Kuwafikia wateja wachache na walio bora kunahitaji kazi kubwa sana.
Kunahitaji mtu kujitoa kweli na kuzama kwenye maisha ya wengine, kuwajua kwa undani na kuwapa kile ambacho kina manufaa makubwa zaidi kwao.
Hilo ni zoezi ambalo huwezi kulifanya kwa wengi.
Ndiyo maana unapoanza utazingatia wingi, kisha katika hao wengi utachagua wachache ambao utawahudumia vizuri zaidi na wakakupa matokeo makubwa zaidi.
Unapozingatia ubora, ni lazima uzame ndani kweli kweli, uwapende kwa dhati wachache uliowachagua na kuhakikisha nao pia wanakupenda na kukukubali.
Hilo ni zoezi ambalo huwezi kulikuza kwa haraka, lakini lina nguvu kubwa ya kukujengea sifa ya kipekee ambayo unaweza kuitumia kuwapata wengine walio bora.
Ukiwazingatia kweli wachache ambao ni bora, wanaofanya manunuzi makubwa, utaweza kuwashawishi wanunue zaidi na pia utaweza kuwaomba wakupe wateja wengine ambao ni bora kama wao.
Na hata pale inapotokea kuna washindani wako wanamwinda kwa mbinu mbalimbali, hawatakimbilia kwa washindani na kukuacha wewe.
Badala yake wataongea na wewe kwanza, kukujulisha kinachoendelea ili kuona kama unaweza kuboresha zaidi.
Tunapochagua kuweka juhudi kubwa zaidi kwa wachache walio bora, wanalijua hilo hasa na kulithamini. Ni kuthaminiwa huko ndiko kunaleta matokeo makubwa na mazuri.
Mwanzoni kazana sana na wingi,
Kadiri unavyokwenda hamia kwenye ubora zaidi.
Na kadiri unavyoendelea, tengeneza wingi ndani ya ubora.
Fikia wengi walio bora na hapo ndipo ulipo ufunguo wa ndoto kubwa ulizonazo.
Kama kweli unaweka muda, nguvu na umakini kwenye kile unachofanya, unaziona fursa za kufikia ubora ulio mwingi.
Hilo linahitaji kazi kubwa ili liweze kutokea.
Kazi ambayo hupaswi kuikimbia mtu mwenye ndoto kubwa kama wewe.
Kwenye maisha usifuate mkumbo wa kukimbilia wingi kama wengi wanavyokushauri na kufanya.
Wewe piga hesabu zako vizuri, ni idadi ya chini kiasi gani inaweza kukufikisha kwenye lengo lako.
Kisha weka kazi kwenye kufikia idadi hiyo ndogo ambayo ni bora zaidi.
Kwa namba ndogo utaweza kuzalisha matokeo makubwa kuliko kuhangaika na namba kubwa.
Msisitizo mkubwa ni utaanza na wingi kwanza kabla ya kwenda kwenye ubora.
Lazima uwafikie wengi kisha kuwachuja na kupata wachache ambao ni bora.
Kisha hao wachache ndiyo unaendelea kuwapa thamani kubwa zaidi ili waridhike na kukupa fursa zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nianze na wateja 100 wa ndoto, kutoka hapo wateja 1000 niliohudumia huku nikichuja wateja 10 muhimu niwahudumie kwa ubora wa hali ya juu, niwawashawishi wanunue zaidi na wanipatie wateja wengine kama wao!
LikeLike
Kanuni ya uhakika hiyo, inahitaji kazi, lakini matokeo yake ni mazuri.
LikeLike
Siangalii Tena uwing naangalia ubora
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana kocha kwa maelezo halisia,kama amvavyo inatokea na kukutana nayo,nitaanza na Jao wengi nikitafuta walio bora kwenye biashara yangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kuangalia ubora ni kugumu lakini ndiko kuliko sahihi, kuliko kuangalia wingi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Naweka viwango vikubwa vya ubora kwenye biashara yangu ili kuwafikia wateja wanaojali ubora na kuwauzia kwa wingi.
Asante sana kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,ntaanza kuweka nguvu kwa wengi na baadae kuwachuja na kuweka nguvu kwa wachache.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ubora kwanza. Anza na watu wengi na uwachuje wabaki wachache ndio utafanya nao kazi kwa ubora.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante sana Kocha, hapa umegusa mahala pake aisee!
“Unapokuwa unaanza kwenye jambo lolote lile, utaanza kwa kuzingatia wingi. Lakini kadiri unavyokwenda, utahamia kwenye kuzingatia ubora. Kuanza na wingi kunakufikisha kwenye ubora kwa urahisi zaidi kuliko kuanza na ubora.”
Hii imenifikirisha sana; hata wakati tunaanza kwenye kisima cha Maarifa tulikuwa wengi, lakini baadaye ulipojikita kwenye ubora, tumekuwa wachache, lakini bora sana. Hii mbinu hata Yesu Kristo aliitumia; alianza na wanafunzi/wafuasi wengi sana, lakini baadaye alichagua 12 tu wa kufanya naye kazi na kuwapa kile kilicho bora zaidi. Kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza kwenye hili.
Asante Kocha.
LikeLike
Kanuni hii ipo kila mahali, ni sisi kuizingatia ili tuweze kupata matokeo bora sana.
LikeLike
Asante Kocha.
Mwanzo nikazane na wingi,
Kadiri ninavyokwenda nihamie kwenye ubora.Na baadaye nitengeneze wingi ndani ya ubora.
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Fikia wengi walio bora na hapo ndipo ulipo ufunguo wa ndoto kubwa ulizonazo.
Kama kweli unaweka muda, nguvu na umakini kwenye kile unachofanya, unaziona fursa za kufikia ubora ulio mwingi.
Hilo linahitaji kazi kubwa ili liweze kutokea.
Kazi Ambayo Sipaswi Kuikimbia Mtu Mwenye Ndoto Kubwa Kama Mimi.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana KOCHA Dr MAKIRITA AMANI, kweli unapoanza jambo lolote lile unaanzia na wingi la baadaye unakuja kuanza na ubora.
Ubora ndiyo una nguvu kuliko wingi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa kutuwekea hii tofauti kati ya wingi na ubora.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante sana kocha, naanza na wateja kumi kwanza. Nawahudumia vizuri kwa viwango vya Hali ya juu. Wananufaika na huduma yangu, wanaendelea kuninufaisha na mimi. Kupitia wateja Hao wanailetelea wateja wengine. Wateja wengine nao Wananufaika kwa viwango vya juu na kunieletea wateja wengine. Na Hatimaye na scale up biashara na kunifikisha kwenye ndoto zangu.
LikeLike
Mpango mzuri sana.
Huwezi kushindwa kuwahudumia kwa ubora wa hali ya juu kabisa wateja 10 tu.
Na utakapofanya hivyo watakuletea wateja wengine wengi zaidi.
LikeLike
Nitakaa chini na kupiga hesabu zangu vizuri, ili niweze kuona ni idadii ya chini kiasi gani inaweza kunifikisha kwenye lengo langu.
Asante sana Kocha Dr.Makirita Amani
LikeLike
Vizuri, ni muhimu sana kujua namba zako za msingi, kisha kuzifanyia kazi kwa uhakika.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitatumia muda, nguvu na umakini kuufikia uwingi. Kwa kanuni ya 8O/2O (Pareto) nitawapata walio bora, na kuendelea kuongeza idadi yao kwa kadri ya uwezo wangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Wingi na ubora kisha twende kwenye wachache wenye ubora watakaohudumiwa kwa wingi. Asante
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Kwenye maisha sitakimbilia wingi kama wengi wanavyonishauri bali nitazingatia ubora , Asante Kocha.
LikeLike
Ubora ukifanyika kwa wingi unaleta matokeo makubwa sana.
LikeLike
Naweka ubora zaidi kuliko uwingi
Shukrani kocha.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana, tunaanza na wingi halafu tunafuatia ubora.
LikeLike
Humo.
LikeLike
Ni kweli hili naendelea kuliona hapo ninapowafikia wateja wengi napata wachache ambao wana uhakika na manunuzi makubwa na hapo nakita thamani na mwisho namuuzia kwa wingi kwenye biashara yangu napita mitaa mingi na huko nawatembelea na kuchuja lengo nipate wale wenye manunuzi ma kubwa ile niwape huduma kubwa na thamani kubwa na kudumu nao
LikeLike
Safi kabisa.
Huo ndiyo mpango mzima.
LikeLike
Nitawahudumia vizuri wateja bora ili wanipe manufaa makubwa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Wateja wachache bora ni rahisi kuwahudumia kuliko wengi wasumbufu.
LikeLike
Kweli kabisa, nguvu tunazotawanya kwa wengi tukizikusanya kwa wachache tutafanya maajabu makubwa.
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
I will always priotize Quality over Quantity……
LikeLike
Great, stay on that lane.
LikeLike
Wingi ndio unatupeleka kwenye ubora kwa kufanya mchujo sahihi.. Asante sana Kocha.
LikeLike
Baada ya kufika hatua fulani, mchujo ni muhimu ili kuweza kupiga hatua kubwa zaidi.
LikeLike
Wingi na ubora havikai pamoja.
Mara zote zingatia ubora.
Piga hesabu ni idadi ya chini kiasi gani unaweza kufikisha kwenye lengo lako , Kisha weka kazi ili kufikia
Idadi hiyo ndogo ambayo ni Bora zaidi.
ASANTE SANA KOCHA KWA MANENO MAZITO
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Tunaanza na Wingi Halafu tunakuja na ubora Asante ili kuwa na focus kubwa Asante Kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Tuanze na wengi Kisha tufanye kazi na wachache walio Bora ili kupata walio Bora wengi zaidi
Asante
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kweli kabisa kuhudumia wengi kuna poteza ubora wa huduma,
na kumridhisha kila mtu kila mteja ni kitu ambacho hakiwezekani..
LikeLike
Lazima tufanye uchaguzi tupo kwa ajili ya watu gani hasa.
LikeLike
Kwa hakika tumezoe kuhangaikia wateja wengi jambo ambalo linathiri ubora
LikeLike
Ubaya wa wengi ni pale wanapokuwa siyo bora. Ila bora wakiwa wengi bado ni vizuri, maana wanalipa vizuri kitu kitakachokuwezesha kuwahudumia vizuri pia.
LikeLike
Kwa kuwa mwanzo ni mgumu, ni bora kuanza na wingi na baadaye ndipo tukikite kwenye ubora
LikeLike
Hakika, mwanzo tunarusha nyavu kunasa yeyote, nyavu ikishalemewa tunaanza kuchuja ili kubaki na walio bora.
LikeLike
Naanza na wingi kisha nawachuja wachache amabao nitakwenda nao kwa ubora wa hali ya juu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ni kweli kabisa Kocha,
Nitaanza na wingi kwanaza halafu nitachaguo ubora kutoka katika wingi.
Asante Kocha
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kweli kabisa kocha,tunaanza na wingi kisha kwenye ubora kutokana na wingi. Hii Ni kanuni ya kuzingatia kwenye biashara yangu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike