3016; Usiwe wa kawaida.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwa chochote unachofanya kwenye maisha yako, usikubali kuwa mtu wa kawaida.
Watu wa kawaida huwa wanaweza kuonekana ni wema kwenye jamii, lakini huwa hawapati mafanikio makubwa.
Mafanikio makubwa huwa yanapatikana kwa kufanya mambo kwa utofauti na ukubwa kuliko ilivyozoeleka.
Mafanikio makubwa ni zao la kwenda kinyume na kundi kubwa la watu.
Wakati watu wengi wanafanya vitu kwa namna fulani, unapaswa kwenda kinyume nao ili kupata matokeo ya tofauti.
Kukataa kuwa kawaida ni rahisi kusema kuliko kufanya.
Inataka mtu uwe na uvumilivu mkubwa, kwa sababu kitendo cha kukataa kuwa kawaida unakuwa umeanzisha vita na kundi kubwa la watu wa kawaida.
Utashutumiwa kutokujali wengine, kutokuzalisha vilivyo sahihi na kuonekana unajisumbua.
Lakini hayo yote ndiyo yanachangia kupatikana kwa matokeo ya tofauti na makubwa zaidi.
Mafanikio makubwa kwenye maisha hayatokei kama ajali, bali yanatengenezwa.
Watu wanaoyapata mafanikio makubwa kwenye jamii ni wachache sana.
Kwa sababu hao ndiyo wanaokuwa na uthubutu wa kutosha kukataa kuwa wa kawaida.
Wakati wengi wakifuata kundi na kufanya kwa ukawaida, wanaofanikiwa sana wanakwenda wenyewe na kufanya kwa ukubwa na utofauti.
Kawaida ni nzuri kufanya, haina ugumu kufanya na wala haina hatari.
Kawaida inaleta uvivu na uzembe ambavyo ni vikwazo vikubwa kwa mtu kupiga hatua kubwa.
Kawaida ni adui mkubwa wa mafanikio makubwa kwenye maisha.
Kama hujui uanzie wapi kwenye kukataa kuwa kawaida, anza kwa kwenda kinyume na kundi kubwa la watu.
Angalia ni vitu gani ambavyo kundi kubwa la watu linafanya, kisha wewe nenda tofauti na wanavyoendana wao.
Ona picha ya tofauti kwenye fikra zako na chukua hatua kubwa, tofauti na kwa wingi zaidi ya wengine wanavyofanya.
Utaweza kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha kama utakwenda kinyume na watu wengi wanavyoenda.
Watu wengi wanafuata mkumbo, wewe simama peke yako.
Watu wengi wanahangaika na mambo mengi, wewe weka mkazo kwenye mambo machache yaliyo muhimu zaidi.
Ona wasichoona wengine,
Fanya wasivyofanya wengine,
Weka mkazo mkubwa kwenye kila unachofanya.
Na jipe muda wa kutosha kupatikana kwa matokeo ya tofauti unayoyataka.
Matokeo bora kabisa yatapatikana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nafanya tofauti na kundi, nasimama mwenyewe na kupigana vita ya kutokufanya ya kawaida, kila mara napaswa kujiuliza je ninachokifanya ni cha kawaida ama ni kitu/namna isiyo ya kwaida kwa ubora?
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Nitaweka mkazo kwenye biashara yangu hadi matokeo makubwa yatakapopatikana, kuanzia leo nakataa kuwa wa kawaida
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Naona wasichoona wengine,nafanya wasichofanya wengine na nafanya kwa msimamo ili kupata matokeo makubwa kabisa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nimekataa kuwa wa kawaida na kuchagua kuwa na kufanya kwa utifauti ili niweze kupata matokeo yasiyo ya kawaida.
Asante kocha
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ukawaida/mazoea ni adui mkubwa kwenye mafanikio.
kuwa wa kawaida utapata matokeo yale yale ya kika siku na siyo hatua kubwa kwenye mafanikio
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Mafanikio makubwa yanapatikana kwa kufanya mambo ya utofauti kuliko ilivyozoeleka.
Pa kuanzia ili uweze kufanya mambo makubwa nenda tofauti na watu walivyozoeya kufanya.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nasimama pekee yangu kufanya yale yaliyokuwa makubwa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitahakikisha naona tofauti na wengine, Nafanya tofauti na wengine
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ili uwe wa tofauti fanya vitu vya tofauti
Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Naona wasichoona wengine,nafanya wasichofanya wengine na kataa kuwa wa kawaida.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ona wasichoona wengine,
Fanya wasivyofanya wengine,
Weka mkazo mkubwa kwenye kila unachofanya.
Na jipe muda wa kutosha kupatikana kwa matokeo ya tofauti unayoyataka.
Matokeo bora kabisa yatapatikana.
Ahsante Kocha.
Nakataa Kuwa Wa Kawaida.
LikeLike
Kataa kata kata.
LikeLike
Kawaida ni kufuata mkumbo, nasimamia misingi yenye manufaa kwangu badala ya kufuata mkumbo wa ukawaida.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mafanikio ktk Maisha hayatokei Kama ajari.
Kukataa kuwa wa kawaida kunakutaka kuwa mvumilivu.
Mafanikio makubwa ni zao la kwenda kinyume na kundi
Kubwa la watu.
ASANTE SANA KOCHA.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitajaribu kufikiri tofauti na wengi na kufanya tofauti na wengi
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kama hujui uanzie wapi kwenye kukataa kuwa kawaida, anza kwa kwenda kinyume na kundi kubwa la watu.
LikeLike
Kundi kubwa huwa lipo kwenye njia ya kupotea, nenda kinyume nalo.
LikeLike
Kuwa wa kawaida ni kutafuta kuwa na maisha ya kawaida. Tuyakatae ili tuwe na maisha yasiyo ya kawaida, yaani maisha ya mafanikio ambayo ni wachache huyafikia.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Bila kuwa wa tofauti utaishia kuwa wa kawaida.
Ukawaida ni ugonjwa nyemelezi wa anguko lolote lile kwenye maisha.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Nisiwe wa kawaida na kufanya ya kawaida.
Nataka kuona wasichoona wengine,
Kufanya wasivyofanya wengine,
Kuweka mkazo mkubwa kwenye kila nnachofanya.
Na kujipa muda wa kutosha kupatikana kwa matokeo ya tofauti unayoyataka.
Nachukua hatua kubwa…
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ili kupata matokeo kweli ni muhimu kujitofautisha
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Nimekuja kugundua kuwa matokeo ya tofauti unayapata kwa kwenda kinyume na watu wengi ina garama lakini ndiyo maana ikawa ya tofauti nenda kinyume nao wakukatae wote lakini wewe usijali kuna wakati watajua maana yako huko mbele na pia hakuna taiiri anayefanikiwa kwa kuwafurahisha watu
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Nahitaji kufanya tofauti na kundi kubwa linavyofanya.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kocha, nitajitahidi kujitafuta kila siku,ili kuwa na upekee wangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike