3019; Kwani namba zinasemaje?
Rafiki yangu mpendwa,
Unapokuwa na ndoto kubwa unazotaka kuzifikia kwenye maisha yako, utasikia ujinga mwingi sana.
Utashauriwa mambo mengi sana unayoweza kufanya ili kufikia ndoto hizo.
Lakini mengi katika hayo unayoshauriwa, yanakuwa ni ujinga mtupu.
Utashauriwa kutumia njia mbalimbali za mkato, ambazo huishia kuwa njia ndefu na zinazokugharimu sana kwa muda na fedha.
Utashauriwa kuchangamkia fursa mpya ambazo hupaswi kuzikosa, ambazo huishia kuwa usumbufu kwako na kuzidi kukuchelewesha.
Halafu kuna kundi kubwa la watu ambao wamekuwa wanafanya mambo yao kwa mazoea, ambalo litakupinga na kukukatisha tamaa kwenye mambo mapya na makubwa unayofanya.
Ukimsikiliza kila mtu kwenye maisha yako, utaishia kutokufanya chochote kipya na kikubwa, kwa sababu watu wengi hawajui hata ni nini wao wenyewe wanataka.
Utasikia mengi sana kutoka kwa kila mtu kwenye safari yako ya maisha.
Lakini hupaswi kulipa uzito kila unalosikia.
Kwa sababu mengi ni ujinga mtupu.
Kama kila mara unafanya au kubadili maamuzi yako kulingana na maoni ya walio wengi, hakuna hatua kubwa utakazoweza kupiga kwenye maisha yako.
Kwani walio wengi huwa hawapo sahihi, hasa inapokuja kwenye mambo mapya na makubwa.
Maoni ya walio wengi yamekuwa yanatokana na hisia na siyo mantiki.
Yanatokana na mazoea waliyonayo au matamanio wanayokuwa wameyapata.
Maamuzi yote makubwa na muhimu kwenye safari ya kuelekea kwenye ndoto zako kubwa, unapaswa kuyafanya kwa kuzingatia namba.
Anza kwa kuangalia namba zinasemaje, namba zako wewe mwenyewe na hata namba za wengine.
Mtu anapokuambia kitu fulani kinalipa sana, kabla hujakimbilia kukubaliana naye, kwa sababu unatamani sana kupata malipo makubwa, muulize mtu huyo akupe namba zinazothibitisha hilo.
Kwa asilimia kubwa watu wanakuwa hawana namba zozote, kwani wanachokuwa wanasema nao walisikia tu.
Hata kwako wewe mwenyewe, kwa kila maamuzi unayotaka kufanya, angalia kwanza namba zinasemaje.
Kama huna namba ambazo tayari zipo, fanya kwanza jaribio dogo ambalo litakupa namba kwa kiwango fulani, kisha tumia namba hizo kufanya maamuzi.
Kwenye maamuzi mengi tunayofanya huwa tunasukumwa zaidi na hisia.
Lakini uhalisia huwa hauendeshwi kwa hisia, bali kwa mantiki yake yenyewe.
Hivyo kama hutakuwa na namba sahihi wakati wa kufanya maamuzi, utaishia kufanya makosa.
Chukua mfano wa watu wengi wanaokuwa wanaanza biashara.
Kwanza wanaanza kwa mawazo ya kihisia, wamesikia au kuona kitu fulani kinalipa, siyo kwa namba zozote, bali kwa wingi tu wa wanaofanya.
Na hata wanapoanza, wanatumia mtaji wote walionao kununua vitu ambavyo kwa hisia zao wanaona ndiyo sahihi.
Wanapoanza biashara ndiyo wanagundua uhalisia ni tofauti sana na mipango ya kihisia waliyokuwa nayo.
Kwanza wanagundua biashara waliyoingia hailipi sana kama walivyokuwa wanaona kwa nje.
Pili wanagundua vitu walivyovipa kipaumbele siyo ambavyo wateja wanavitaka zaidi.
Hayo yanapelekea wengi kukwama na kushindwa kufikia ndoto walizonazo.
Ondoa hisia na matamanio yako binafsi kwenye maamuzi unayofanya.
Tumia namba zilizopo au ambazo utazijaribu katika kufanya maamuzi bora.
Na kila wakati nenda ukiboresha maamuzi yako kulingana na namba unazokuwa unaendelea kuzipata.
Ili uweze kutumia namba kufanya maamuzi bora na sahihi, lazima namba hizo pia ziwe sahihi.
Hivyo unapaswa kuchukua namba zote muhimu kwako kwa usahihi, kisha kuzichakata kwa usahihi na kutumia matokeo yake kufanya maamuzi.
Kwenye safari kubwa ya mafanikio tuliyopo, maamuzi yoyote unayoyafanya bila ya namba ni umbeya na huo hauwezi kukupa matokeo makubwa.
Kuwa mpenzi wa namba,
Kusanya namba nyingi uwezavyo,
Zichakate kwa usahihi,
Kisha zitumie kwenye kufanya maamuzi.
Wengi wanaposikia namba huwa wanazikwepa kwa kuona ni hesabu ngumu ambazo hawaziwezi.
Lakini hilo siyo sahihi, namba siyo hisabati. Ndiyo hisabati zinatumia namba, lakini siyo kila namba ni hisabati.
Chukua mfano huu rahisi;
Kwenye biashara yako umeuzia wateja 10 na kupata faida ya milioni 1.
Katika wateja hao 10, wawili wamekuingizia faida ya laki 8, na nane waliobaki wamekuingizia faida ya laki 2.
Je kama unataka kutengeneza faida zaidi, ni maamuzi gani utakayofanya?
Majibu yako wazi, wauzie zaidi wale wanaoleta faida kubwa.
Umewajua kwa sababu ya namba zilizopo.
Ukiwa huna namba utafanya maamuzi kwa hisia na kwa kubahatisha, kitu kinachokupeleka kwenye makosa mara zote.
Jambo muhimu la kukumbuka na kuzingatia kwenye kila maamuzi unayofanya ni hili; kama hakuna namba ni umbeya. Sasa kama unataka ujenge mafanikio yako makubwa juu ya umbeya, utakuwa unajidanganya wewe mwenyewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kama hakuna namba ni umbea.Maamuzi yoyote yaangalie namba.
LikeLike
Mamba ndiyo mpango mzima.
LikeLike
Ahsante sana kocha siku zote mitafanya maamuzi yangubkwakuangalia namba
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana Kocha chochote ninachofanya ni lazima kuwa na namba.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Katika kufanya maamuzi yoyote yale tunapaswa kutumia namba badala ya hisia.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kweli kabisa Kocha, watu wanaweza kukuvuruga na kukupeleka usikotarajia tofauti na malengo yako ya awali
LikeLike
Tuzingatie namba.
LikeLike
Asante sana kocha,ni namba tu na kukaa kwenye mchakato
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni sawa kochà Namba hazidanyi.
LikeLike
Tuzingatie sana namba.
LikeLike
ahsante kocha,
business is the number game.
LikeLike
Tuziheshimu namba.
LikeLike
Kwenye maamuzi mengi tunayofanya huwa tunasukumwa zaidi na hisia.
Lakini uhalisia huwa hauendeshwi kwa hisia, bali kwa mantiki yake yenyewe.
Hivyo kama hutakuwa na namba sahihi wakati wa kufanya maamuzi, utaishia kufanya makosa.
LikeLike
Tutumie namba kufanya maamuzi.
LikeLike
Kwenye maamuzi mengi tunayoyafanya uwa tumasukukumwa zaidi na hisia
Asante sana
LikeLike
Tutumie namba ili tusizinguliwe na hisia.
LikeLike
Kweli namba ndio kila kitu kwenye kufanya maamuzi
LikeLike
Bila namba tutayumbishwa sana.
LikeLike
Bila namba ni umbeya
LikeLike
Na umbeya hauna tija.
LikeLike
Hilo ni kweli kabisa biashara bila no ni umbea mtupu na no hazidanganyi ili uweze kuonveza mauzo au wateja anza kwanza no zinasemaje na hapo utaweza kuona uongeze kwa stail ipi katika list ya vifaa vyangu nimeenda mbali zaidi na kugundua kuwa kuna bidhaa zina faida kubwa lakini mtaji mdogo naweka nguvu huko lakini nisingeweza kujua bila kuangalia no
LikeLike
Vizuri sana kwa kutumia namba kufanya maamuzi sahihi.
Endelea kuzichakata namba vizuri ili kufanya maamuzi bora sana.
LikeLike
Kama hakuna namba ni umbea
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Bila namba maamuzi yataendeshwa na hisia tuu
LikeLike
Na hisia hazileti matokeo mazuri.
LikeLike
Asante kocha,nitakusanya namba nyingi niwezavyo na kuzichakata ili nifanye maamuzi kwa usahihi.
LikeLike
Kusanya namba na zichakate, kuna mengi ndani yake.
LikeLike
Nimejua kuwa maamuzi yote nitakayofanya kuelekea kwenye ndoto yangu kubwa lazima ya base kwenye namba
Bila kuangalia namba ni umbeya na umbeya hauna tija kwenye biashara.
Asante
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Namba kwanza, mengine ni umbeya
LikeLike
Tupambane na namba.
LikeLike
Namba ndiyo zinakufaya ufanye tathimini, ufanye maamuzi au ujue Kama unafanikiwa au inaanguka. Namba ni muhimu Sana maishani mwangu
LikeLike
Tuzingatie namba
LikeLike