3043; Roho mbaya.
Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya vikwazo vikubwa kwenye safari ya mafanikio ya wengi ni jamii inayokuwa inamzunguka.
Jamii hiyo inapokuwa na watu ambao hawana mafanikio wala hawapo kwenye safari ya mafanikio makubwa, inazuia watu wengine wasiyapambanie mafanikio.
Kwa kuwa safari ya mafanikio inamtaka mtu ajitoe sana na kusema HAPANA kwenye mambo mengi, jamii haiwakubalii kirahisi wale wanaotaka kufanikiwa.
Jamii inakuwa haikubali mtu yeyote awe tofauti na jamii hiyo.
Hivyo inatumia mbinu mbalimbali kuhakikisha watu wote wanabaki kuwa sawa.
Na njia kubwa kabisa ambayo jamii huwa inatumia sana ni kuwateka watu kihisia, hasa hisia za lawama, hatia na majuto.
Jamii huwalaumu wale ambao wanakwenda tofauti na kuwafanya wajione wana hatia kubwa ili kuwajengea majuto.
Jamii inawafanya wale wanaopambana kufanikiwa wajione kama ndiyo kikwazo kwa jamii nzima.
Moja ya njia kubwa ambayo jamii inatumia kwa watu wanaotaka kufanikiwa ni dhana ya roho mbaya.
Jamii inawaona wale wanaopambana kufanikiwa kama watu wenye roho mbaya sana.
Kwa sababu wanaweka kipaumbele zaidi kwenye mambo yao na kusema hapana kwenye mambo ya wengine, wanashutumiwa kuwa na roho mbaya.
Wale wenye mioyo myepesi, ambao ndiyo wasiofanikiwa huwa wananasa kwenye mtego huo. Kuona kweli kwamba wana roho mbaya kwa kuamua kuyaishi maisha yao na hivyo kubadilika na kufuata mkumbo wa jamii.
Wanachokuwa wamefanya ni kutaka kuonekana wana roho nzuri kwa jamii, ila ukweli ni wamechagua kuwa na roho mbaya kwao wenyewe.
Kuna vitu viwili vikubwa sana unavyopaswa kujua kwenye dhana hii ya roho mbaya ili uweze kuwa huru.
Kitu cha kwanza ni dhana nzima ya roho mbaya ni mtego unaokuwa umewekewa. Watu huwa wanaona mtu mwenye roho nzuri ni yule anayekubaliana nao na wanajufaika moja kwa moja kutoka kwao na watu wenye roho mbaya ni wale wanaofanya mambo yao, ambao hawawapi kile wanachotaka kwa namna wanavyotaka wao.
Hivyo roho mbaya siyo kile unachofanya wewe, bali mategemeo ya watu kwako.
Watu ni wabinafsi, wanapoona huwapi kile wanachotaka wao, wanakuona ni mbaya, hata kama hakuna lolote baya unalofanya.
Kitu cha pili ni lazima mategemeo ya upande fulani yapuuzwe ili maisha yaweze kuendelea. Kwa mfano kama kila mtu anataka kupata muda wako na ukampa kila mtu dakika 10 kwenye siku yako, siku nzima utaimalizia kwa watu. Kwa watu hao utaonekana una roho nzuri, lakini kwa upande wako mwenyewe utabaki kuwa na roho mbaya, kwa sababu umepuuza kutekeleza yale muhimu zaidi.
Hivyo inabidi uchague kuwa na roho mbaya kwa wengine, kwa kuweka vipaumbele kwenye mambo yako au uwe na roho mbaya kwako mwenyewe kwa kuweka vipaumbele kwenye mambo ya wengine.
Kwa kifupi, kama lengo lako ni kutokuonekana una roho mbaya kwenye maisha, hiyo yenyewe tayari ni roho mbaya kwako mwenyewe.
Utakazana kumridhisha kila mtu, ila utaishia kujipuuza wewe mwenyewe.
Huwezi kufanikiwa kwa kutaka kumridhisha kila mtu kila wakati.
Anza kwa kujiridhisha wewe mwenyewe na utaweza kuwaridhisha wale wanaoendana na wewe baada ya kuwa umefanikiwa.
Hili halimaanishi kwamba uwafanyie watu ubaya ili kufanikiwa.
Bali linamaanisha uweke kipaumbele kwenye mambo yako na kupuuza mengine yote ambayo watu wanataka kukuteka nayo ili uachane na ndoto zako kubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni kweli kwamba ukimpa kila mtu Muda wako inakuwa umepoteza siku mzima na kuwa na roho mbaya kwako mwenyewe. Inabidi tuseme hapana kubwa
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kutoa kipaumbele kwa mambo ya wengine ili uonekane una roho nzuri hiyo tayari ni roho mbaya kwako mwenyewe.
LikeLike
Chagua kuwadisapoint wengine au ujidisapoint wewe mwenyewe.
LikeLike
Nitakuwa roho mbaya kwa wengine kwa kuweka vipaumbele kwangu
LikeLike
Zingatia zaidi vipaumbele vyako.
LikeLike
uzuri ni kwamba hata unapofanya mambo yako, si yako pia ni kwa ajili ya wengine. lakini hao wanao ona uwajali ujue naohawakujali wala sio wako, watu wako ni wale wanaonufaika na mambo yako.
mfano muembe utaendelea kutoa maembe hata kama wewe unataka chungwa, hivyo ukisema muembe huu una roho mbaya kwa kuwa wewe unata chungwa, wewe ndio ukatafute mchungwa.
kadhaliki na ng’ombe hataendelea kutoa maziwa hata kama wewe unataka asali.
LikeLike
Dah, umeweka mifano ya nguvu sana hapa, mwembe hautajali wewe kuuita una roho mbaya kwa sababu haukupi machungwa. Tukielewa hili kwa kina tutafanya makubwa sana na kuacha kutaka kumridhisha kila mtu.
LikeLike
Kipaumbele cha kwanza ni yale ya muhimu zaidi kwangu.Naacha sana kuepuka kuonekana na roho mbaya kwa wengine kwa kuanza kuwa na roho nzuri kwanza kwangu.
LikeLike
Kama kweli watu wanakupenda, watakuunga mkono kwenye vipaumbele vyako. Kama wanaona una roho mbaya kwa kujali vipaumbele vyako, wanataka kunufaika kupitia wewe.
LikeLike
Unapofanya jambo lolote fanya kwa Ajili yako na sio kwa ajili ya mwingine na hiyo itakusaidia kupiga hatua kubwa sana katika kile unachokifanya…
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Jamii huwa haikosi la kusema, ukiishi kama wengine wanavyoishi hakuna atakusema lakini pale tu utakapochukua hatamu ya maisha yako, ndiyo wataanza kuongea.
Hakuna mtu ambaye anaweza kumpiga teke mbwa aliyekufa, ukiona husemwi, jua wewe umeshakufa. Jiridhishe kwanza wewe mwenyewe na mengine yatafuata.
LikeLike
Umesema vyema sana, mbwa aliyekufa hapigwi teke.
LikeLike
Ninaweka kipaombele kwenye malengo yangu makubwa niliyo nayo bila kujali wengine wataniona nina roho mbaya kiasi gani
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Sitajifanyia roho mbaya mimi mwenyewe
bali nitafanya kile kinacholeta manufaa kwa wote
shukrani kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahsnate sana kocha, nitakuwa na royo mbaya kwa wengine i kuyapa kipakumbele yale yenye mchango mkubwa wa maisha yangu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
kama lengo lako ni kutokuonekana una roho mbaya kwenye maisha, hiyo yenyewe tayari ni roho mbaya kwako mwenyewe.
Asante
LikeLike
Kabida.
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo hili. Nitajitahidi kuwa na roho nzuri kwangu mwenyewe.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa msimu huu wa hapana unatupa nafasi ya kutathmini maisha yangu na uwekezaji wa akili, nguvu na muda nimekuwa nasema hapana kwa vikao ambavyo havina tija na ninaendelea kupunguza haya majukumu ya kijamii kila wakati ili kupata muda kwa ajili yangu na maono makubwa. Hakika jamii ina kila aina ya mtego wa kutukwamisha tusifikie mafanikio
LikeLike
Ukilegeza tu, unajikuta upo kwenye kila kamati na hakuna hatua kubwa unazopiga.
LikeLike
Kuwaridhisha wengine hiyo pia ni roho mbaya kwako mwenyewe!
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Huwezi kuiridhisha jamii kwa kila inachotaka, muhimu ni kusimamia vipaumbele vya ndoto zangu bila kujali Dunia inasemaje
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kuliko uwe na rohombaya kwako mwenyewe uwe na rohombaya kwao maana maisha yako ni yako mwenyewe na siyo yao na usipokuwa na rohombaya utawagaia muda wako na kazi zako zitalala
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitaanza kwa kujiridhisha mimi mwenyewe kwanza halafu ndiyo nitaweza kuwaridhisha wale wanaoendana na mimi baada ya kuwa nimefanikiwa.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Uchaguzi ni wako. Kuwa na roho nzuri kwa
Watu au kuwa na roho nzuri kwako. Mimi nimechagua kuwa na roho mbaya kwa watu kwa na kuwa na roho nzuri kwangu.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nitakuwa na roho mbaya kwa wengine kwa kufanya mambo ya msingi kwa ajili ya mustakabali wa maisha yangu na si kwaajili ya kuwafurahisha wao.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Lawama ni sehemu ya maisha ya mafanikio, sitaziepuka kwa kuwa na roho mbaya kwangu
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Huwezi kufanikiwa kwa kutaka kumridhisha kila mtu kila wakati.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Watu ni wabinafsi, wanapoona huwapi kile wanachotaka wao, wanakuona ni mbaya, hata kama hakuna lolote baya unalofanya.
LikeLike
Kabisa yani.
LikeLike