3047; Ni bora uache mapema.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna sababu kuu mbili kwa nini watu hawapati kile wanachotaka kwenye maisha yao.
Moja ni hawajui kwa hakika nini hasa wanachotaka.
Na mbili ni hawajajitoa kweli kweli kupata kile wanachotaka.
Pamoja na mahangaiko makubwa ambayo unaona watu wengi wanayo, sehemu kubwa ya watu hao hawajui wanachotaka.
Na wala sizushi hilo, wewe wafuatilie tu, utagundua mwaka juzi walikuwa na fursa fulani, mwaka jana fursa nyingine na mwaka huu fursa nyingine tena ya tofauti kabisa.
Hakuna mtu anayejua kwa hakika kile anachotaka halafu akawa anahangaika na kila kinachopita mbele yake.
Kwa wale wachache wanaojua nini hasa wanachotaka, wengi wao hawajajitoa kweli kweli kuhakikisha wanapata wanachotaka. Hawajawa tayari kulipa gharama kubwa inayohitajika kulipwa ili kupata kile wanachotaka.
Wanakuwa wanatamani kupata, ila hawajawa tayari kujitoa kafara ili kuhakikisha wanapata kwa uhakika.
Ni kama hawaamini upo uwezekako wa kupata kwa uhakika, hivyo wanachukulia kama kamari, wakipata sawa na wasipopata sawa.
Hapo unaweza kujionea mwenyewe kwa nini sehemu kubwa ya watu hawapati mafanikio kwenye maisha yao, hawajui mafanikio kwao ni nini na wale wanaojua hawajajitoa kwa kila namna kuyapata.
Leo nataka ufanye zoezi rahisi, kwa kuanza na kile unachofanya sasa.
Kama kuna sababu yoyote itakayokufanya uache kukifanya, basi ni bora uache kukifanya mapema.
Kama ukikutana na fursa nyingine nzuri utaachana na unachofanya sasa, ni bora uache na kwenda kwenye fursa nyingine nzuri.
Kama ukikutana na ugumu utaacha, basi acha sasa, maana ni hakika utakutana na ugumu.
Na hata kama ukipata mafanikio makubwa utaacha kufanya chochote unachofanya sasa, ni bora tu uache sasa, maana hautajitoa kwa kila namna kuyapata mafanikio hayo.
Asili huwa ipo tayari kupindisha hata kanuni zake, ili tu kumpa kile anachotaka, yule aliyejitoa kweli kukipata.
Na kabla haijampa anachotaka inampima kwanza kwa njia mbalimbali.
Inaleta kwake fursa ambazo zinaonekana ni nzuri kuliko anachofanya, akiacha alichokuwa anafanya na kwenda kwenye fursa mpya, asili inajua ni mtu asiyeaminika, hivyo inaendelea kumpoteza kwa fursa nyingine mpya kila wakati.
Pia asili ina tabia ya kuwaonjesha watu kile wanachotaka, inawapa mafanikio kiasi na kuwaangalia wanayapokeaje. Kama watayapokea mafanikio hayo kidogo kwa kiburi, kwa kuona hawahitajiki tena kupambana kama walivyokuwa wanafanya, basi asili inahakikisha inawazuia wasipate mafanikio makubwa zaidi, maana inajua wataleta ufaribifu mkubwa kwa wengi.
Ndiyo maana nakuambia leo ufanye zoezi hili la kukagua chochote ambacho kuna uwezekano wa wewe kukiacha, basi ukiache mapema.
Itaokoa muda na nguvu unazopoteza kwenye kitu ambacho hakuna mahali kinaenda.
Muda na nguvu unazotawanya kwenye mambo mengi unayoanza kufanya na kuacha, ukizikusanya kwenye kitu chochote kimoja kwa muda mrefu bila kuacha, lazima utapata matokeo makubwa sana.
Lengo la kukutaka uache mapema ni ili uchague kwa usahihi kile ambacho utajitoa kwa kila namna, ukusanye rasilimali zako zote hapo bila kuyumbishwa na chochote.
Hivyo pia ndivyo inavyokuwa kwa watu, kama kuna watu unaojihusisha nao na huoni ukijihusisha nao kwa kipindi chote cha maisha yako basi achana nao mara moja.
Kama kuna sababu yoyote itafanya uachane na mtu huko mbeleni, ni bora kuachana naye sasa.
Ni upotevu mkubwa wa muda kuendelea na watu ambao hujajitoa kweli kwenda nao kwa muda mrefu.
Huwa ni rahisi kwa watu kulalamika kwamba hawayapati mafanikio makubwa wanayoyataka.
Ila hutawasikia watu hao hao wakieleza jinsi ambavyo wao wenyewe wamekuwa wanazingua kwenye hiyo safari yao ya mafanikio.
Kwa mtu yeyote ambaye ameshaweka muda wa kutosha (angalau miaka 10) kwenye safari ya mafanikio na hajafanikiwa, tatizo siyo safari, bali tatizo ni yeye. Tatizo ni anakuwa anazingua, kwa sababu hakuna namna mtu anayejua anachotaka na kujitoa kweli kweli kukipambania kwa msimamo kwa kipindi chote hicho cha zaidi ya miaka 10, halafu asifanikiwe.
Ni kinyume kabisa na kanuni za asili.
Maana hata ukichukua tu tone la maji na likawa linaanguka kwenye mwamba mgumu, kwa kujirudia rudia bila kuacha, mwamba huo utavunjika. Huo ni uhakika na siyo kubahatisha.
Kama tone la maji lisilo na akili yoyote linaweza kufanya hayo makubwa, vipi kwa wewe mtu mwenye akili na uwezo mkubwa?
Nguvu ya tone la maji haijatoka kwenye tone lenyewe, bali kwenye msimamo wake.
Swali ni je wewe una msimamo kiasi gani kwenye kupata kile unachotaka kwenye maisha yako?
Kama huna msimamo mkali, ambao hauangushwi na chochote, ni bora tu uache mapema, maana hakuna namna utayapata mafanikio makubwa unayoyataka kama huna msimamo mkubwa na usioyumbishwa.
Hata kuchelewa kwa watu kufanikiwa kwenye maisha, kunatokana na mahangaiko mengi ambayo watu wanakuwa nayo awali.
Wanahangaika sana na kila njia, wakidhani kuna njia rahisi na ya mkato.
Ni mpaka muda umekwenda na wameshajaribu kila kitu ndiyo wanapata uelewa kwamba hakuna njia rahisi na ya mkato ya kupata wanachotaka, hivyo wanaamua watulizane kwenye kitu kimoja kwa msimamo, kwa sababu wanajua kitawapa matokeo.
Mtu yeyote anayewahi kuchagua kile atakachokwenda nacho kwa msimamo bila kuyumba, lazima atayapata mafanikio makubwa mapema.
Siyo kwa sababu ya bahati wala miujiza, bali kwa sababu ya kujua anachotaka na kuamua kulipa gharama ya kukipata.
Umeshazingua sana na mambo mengi ambayo umekuwa unayajaribu kwenye maisha yako kwa miaka mingi ambayo umekuwa kwenye utafutaji.
Sasa ni wakati muafaka wa kuamua hapo ilipochagua sasa ndipo utakaa kwa maisha yako yote na kupambania kwa msimamo bila kuacha.
Na kama ndani ya roho yako unaona huwezi hilo, kama hujioni ukipambania hapo kwa kipindi chote cha maisha yako kilichobaki, basi achana napo mapema, haina haja ya wewe kuendelea kupoteza muda na nguvu zako.
Kama bado unataka kuendelea na majaribio, endelea nayo, lakini jua hakuna jipya utakalogundua kwenye hii safari ya mafanikio.
Lingekuwepo ungeshaligundua kwenye mahangaiko mengi ambayo umekuwa nayo mpaka sasa.
Pamoja na hayo mahangaiko mengi ambayo umekuwa nayo, hujagundua jipya, hujaipata njia rahisi na ya mkato ya kufanikiwa.
Sasa kwa nini usiachane na hayo mahangaiko na kuweka rasilimali zako zote kwenye safari ya uhakika uliyoichagua?
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni bora uache mapema kuliko kuendelea kupoteza muda wako.
LikeLike
Haina maana.
LikeLike
Sitahangaika na fursa nyingine yoyote hadi nifanikiwe kupitia ninayofanya sasa
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
penda unacho kifanya au kiache, wapende unaojihusisha nao au achana nao.
LikeLike
Rahisi kama hivyo.
LikeLike
Sasa ni wakati muwafaka wa kuamuafaka wa kuamua kuachana na mambo mengi na kubakia na machache yale niliyoyachagua
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Na weka nguvu zote kwenye mchakato Wa kuelekea ubilionea, hakuna kingine muhimu.. najenga biashara ya uhakika,wateja waaminifu,timu bora na uwekezaji..
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Na weka nguvu zote kwenye mchakato Wa kuelekea ubilionea, hakuna kingine muhimu.. najenga biashara ya uhakika,wateja waaminifu,timu bora na uwekezaji..naachana na mengine yote Ili kuweka umakini wangu hapa
LikeLike
Safi sana, kaa humu.
LikeLike
Muda ulio kubalika ni sasa, ni bora uache mapema. Kujua unacho taka na kuweka kazi kwa juhudi kubwa inasaida sana.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Naweka kazi na juhudi kubwa kwenye nilichochagua kufanya had nione matokeo,sitahangaika na vitu vingine
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
muda uliobaki ni kiujenga kampuni ya MVFF mengine naachana nayo
yasinipotezee muda,nguvu,na fedha zng
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Asante Kocha naweka kazi hapa kwa kile nilichochagua
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mtu yeyote anayewahi kuchagua kile atakachokwenda nacho kwa msimamo bila kuyumba, lazima atayapata mafanikio makubwa mapema.
Siyo kwa sababu ya bahati wala miujiza, bali kwa sababu ya kujua anachotaka na kuamua kulipa gharama ya kukipata.
Asante
LikeLike
Hakika,
Ni kuamua kulipa mapema badala ya kukopa na kujichelewesha kufanikiwa.
LikeLike
Asante sana kocha nitaangalia miaka 50 ijayo kabla cjafanya chochote.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Msingi mkuu kwenyemafanikio,ni kuwa na msimamo usiyoyumbishwa kamwe.kutokuhangaika na mambo mapya mengi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Niachane na harakati za mafanikio mapema au niweke juhudi na nguvu zote kwenye kile nilichochagua.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni kweli tunajichelewesha wenyewe kupata mafanikio ajili ya kuchelewa kupata maarifa sahihi tukabaki tukirukaruka tu swala la kusema hapana halikuwepo
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Najituliza kwenye kitu kimoja na kufanya kwa uhakika na kupata matokeo kuliko kuhangaika kama nyani mtini mara tawi hili na lile.
Asili itanipa kile nachotaka kama nikitulia na kujitoa kwenye kitu kimoja.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Asante Kocha,kama sijioni nikipambania hapo kwa kipindi chote cha maisha yangu kilichobaki, basi niachane napo mapema, haina haja ya mimi kuendelea kupoteza muda na nguvu zangu. 🙏
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Sasa najua ninachotaka na nitapambana kukipata.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Haina maana kuendelea na jambo ambalo mbelezi nitakuja kuliacha baadae ni upotezaji wa rasilimali adimu kuwahi kutokea (Muda).
LikeLike
Kabisa.
LikeLike