3064; Usawa usiowezekana.
Rafiki yangu mpendwa,
Sisi binadamu huwa tunapenda sana usawa kwenye kila eneo la maisha.
Tunapenda vitu vyote viende sawa ili tuyafurahie maisha yetu.
Lakini ukweli mchungu ni kwamba, hakuna usawa kwenye mambo yote na wala hautakuja kuwepo.
Mambo yote kwenye maisha huwa yanakwenda kwa kanuni za asili, ambazo haziangalii usawa bali msimamo uliopo.
Watu huwa wanatamani sana asili iende vile wanavyotaka wao, lakini asili huwa haiendi hivyo.
Na hapo ndipo wengi huvurugwa.
Moja ya eneo ambalo limewavuruga sana watu kwenye safari ya mafanikio ni kutaka usawa kati ya kazi na maisha.
Mafanikio makubwa yamekuwa yakitaka mtu aweke kazi sana.
Wakati huo huo watu wamekuwa wakitaka kuwa na usawa kati ya kazi na maisha.
Kwamba muda fulani uwe wa kazi tu na muda mwingine uwe wa maisha tu.
Hili ni jambo ambalo watu wengi sana wamelijaribu kwenye safari ya mafanikio na kuishia kushindwa vibaya.
Mafanikio makubwa hayataki utenganishe kazi na maisha, bali yanataka ufanye vyote kuwa kitu kimoja.
Mafanikio makubwa yanataka mtu uwe tayari kufanya kazi muda wote, kwa sababu fursa na changamoto huwa zinajitokeza muda wowote.
Kwa kutenganisha kazi na maisha kwenye safari ya mafanikio makubwa ni kupunguza kasi ya mafanikio au hata kuyazuia kabisa.
Mafanikio makubwa yanahitaji umakini na juhudi kubwa pia.
Siyo kitu unachoweza kufanya kwa urahisi.
Safari hiyo ni ngumu sana mwanzoni,
Hapo ndipo panapohitaji mtu aweke kila alichonacho.
Na hapo ndipo panapoamua kama mtu atapata mafanikio makubwa au atayakosa.
Inasaidia sana pale kile unachokuwa unafanya kinapokuwa ndiyo kitu unachopenda zaidi kufanya.
Hiyo itapunguza hitaji la wewe kutaka mapumziko au burudani.
Kama unachofanya ndiyo burudani kuu kwako, utakuwa tayari kukifanya muda wote bila ya kutaka mapumziko kwa ajili ya maisha.
Na kwa kuwa safari ya mafanikio unachagua kwa uhuru wako mwenyewe, chagua kile unachopenda sana ili usisumbuke na kutafuta usawa ambao haupo.
Kwenye ajira, wengi sana hutaka usawa wa kazi na maisha, kwa sababu wengi hawapendi kazi wanazofanya.
Ndiyo maana mwanzo wa wiki huwa wanachukia na mwisho wa wiki kufurahia.
Hilo limekuwa kikwazo cha mafanikio kwa wengi waliopo kwenye ajira.
Wanapokosea wengi wanaotoka kwenye ajira na kwenda kujiajiri ni kwenda na mtazamo huo huo wa kutenganisha maisha na kazi, kitu kinachopelekea washindwe vibaya.
Mafanikio makubwa huwa yanahitaji mtu atoe kafara kubwa pia.
Na moja ya kafara hizo ni kuweka muda wako wote na maisha yako yote kwenye kile unachofanya.
Hilo linamtaka mtu kusema hapana kwa mengine yote isipokuwa anachofanya.
Hilo linataka mtu kuweka maisha yake yote kwenye hicho anachofanya.
Mtu anapofikiria tu kuhusu swala la usawa, kuhusu kupata muda wa kupumzika, anakuwa ameanza kupoteza.
Madhara ya fikra hizo huanza kuonekana mapema sana kwa matokeo mabaya yanayojitokeza.
Kwenye safari ya mafanikio makubwa, hakujawahi kuwa na usawa wa kazi na maisha, bali kunaweza kuwa na vipaumbele.
Muda mwingi kipaumbele kinakuwa kwenye kazi, na hapo mtu anapaswa kuweka kazi hasa.
Na muda mwingine kipaumbele kinakuwa kwenye maisha, kulingana na uhitaji unaokuwepo.
Njia bora ya kwenda na hilo la kazi na maisha siyo kwa kuwa na sheria fulani ya usawa unayokuwa unaifuata, bali kwenda jinsi mambo yanavyotaka.
Kama kazi inakutaka muda mrefu zaidi kulingana na unyeti wake, unaipa muda huo mrefu. Na kama kazi ina ahueni kwa kipindi fulani unaweka muda na umakini kwenye maisha.
Ni vipaumbele na mahitaji na siyo sheria yoyote ile.
Uzuri ni kwamba, kwenye safari ya mafanikio makubwa, mambo huwa yanaenda yakibadilika.
Mwanzoni hitaji la kazi linakuwa kubwa sana kiasi cha maisha kuonekana kama hayapo kabisa.
Lakini kadiri mtu anavyoendelea kufanikiwa ndivyo hitaji la kazi linapungua na maisha kupata nafasi.
Hiyo ni mbele sana ya safari na siyo wakati ambapo mtu anakuwa anaanza.
Ukweli ni kwamba safari ya mafanikio makubwa ni ngumu sana sana.
Hitaji la usawa wa kazi na maisha ni kitu ambacho hupaswi hata kukifikiria mwanzoni mwa safari hiyo.
Unachopaswa kufikiria ni wapi panahitaji kipaumbele zaidi na kupeleka hapo umakini na juhudi zako.
Hilo linataka sana uwe unapenda kile unachofanya ili usiwe na starehe nyingine yoyote unayoitaka nje ya kitu hicho.
Pale unachofanya kinapokupa raha, hutafikiria kuhusu usawa wa maisha na kazi, utaifanya kazi kwa sababu siyo tena kazi kwako, bali mchezo unaokupa raha.
Ukishajiona unaharakisha kazi ili uende kwenye starehe na mapumziko, jua umechagua njia isiyokuwa sahihi na mafanikio makubwa kwako yatakuwa magumu sana.
Chagua vyema kile unachofanya ili uweze kukipa kila ulichonacho bila ya kuhangaika na usawa wa kazi na maisha.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kwenye safari ya mafanikio makubwa usawa wa kazi na maisha haupo, hasa katika hatua za mwanzoni.
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
kazi yako haipaswi kuwa kazi bali mchezo ambao kila muda unatamani kuucheza.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ahsante sana kocha, hamna usawa katika katika kazi na maisha kama kweli nahitaji mafanikio
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante Kocha. Huu ujumbe umekuja muda mwafaka kwangu. Sitakiwi kutenganisha kati ya kazi na maisha, bali niwe na vipaumbele.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Huwezi kutenaganisha kazi na maisha.
Nakwenda kutoa kafara kwenye muda wangu wote kwenye kile ninachofanya.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hakuna mjadala wa kazi wala usawa wa kazi kama kweli umasikini unakuumiza.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Umasikini haujali usawa wako, hivyo lazima kupambana nao sana.
LikeLike
Ahsante sana kocha kwa Uzi wa leo.
Nimechagua sehemu sahihi ya kuelimisha kwahiyo Sina uharaka wa kukimbia kimbia. Nitakaa hapo na kuufanya kama mchezo kwangu.
Nitaweka KAZI na maisha kuwa kitu kimoja kwangu
✅🤝🔥
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Chagua vyema kile unachofanya ili uweze kukipa kila ulichonacho bila kuhangaika uswa wa kazi na maisha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha, safari ya mafanikio ni burudani tosha.
LikeLike
Kama haikuburudishi kuna mahali unapotea.
LikeLike
Asante sana, kumbe hakuna usawa wa kazi na maisha, inatakiwa kuweka kazi na kuifanya kazi kuwa sehemu ya maisha.
LikeLike
Huo ndiyo mpango.
LikeLike
Mafanikio. Makubwa yanakutaka uyafanye maisha na kazi yako kuwa kitu kimoja. Kwa sbabau mafanikio makubwa ni magumu sana na asili kama inavyotwambia unapata kile unachokivumilia sana.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwa kuwa Niko mwanzoni mwa safari ya mafanikio makubwa,maisha yangu yote yatakuwa ni kazi mpaka hapo nitakapokuwa Nimepata mafanikio.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mafanikio makubwa hayataki utenganishe kazi na maisha, bali yanataka ufanye vyote kuwa kitu kimoja.
Asante sana
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Mtaweka kazi pale panapohijatika bila kuweka sababau
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Safari hii ni ngu,u mwanzoni inahitaji niweke kila kitu nilicho nacho.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante kocha,nitaweka mda mwingi kwenye kazi kuliko starehe na mapumuziko.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
حکومت usawa kwenye kazi starehe
LikeLike
Inasaidia sana pale kile unafanya kinapokuwa ndiyo kitu unachopenda zaidi kufanya.✍️
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Sio usawa wa kazi na maisha bali vipaumbele kwa sasa.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mafanikio makubwa yanataka mtu uwe tayari kufanya kazi muda wote.
LikeLike
Hilo halina ubishi.
LikeLike
kazi na maisha….visitenganishwe viwe sambamba
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Natakiwa kuwa tayari kufanya kazi muda wote, kwa sababu fursa na changamoto huwa zinajitokeza muda wowote.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
safari ya mafanikio makubwa ni ngumu sana
LikeLike
Lakini inawezekana.
LikeLike
Pale unachofanya kinapokupa raha, hutafikiria kuhusu usawa wa maisha na kazi, utaifanya kazi kwa sababu siyo tena kazi kwako, bali mchezo unaokupa raha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hakuna usawa kwenye kazi na maisha bali vyote huenda kwa pamoja. Asante kocha kwa somo hili
LikeLike
Karibu
LikeLike
Hakuna usawa kati ya maisha na kazi. Asante Kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante sana kocha, hapo Kazi ipo muhimu ni kuchagua kazi kwanza.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni kweli kazi kwanza na starehe miaka ijayo kwa sasa kazi masaa mengi
LikeLike
Starehe haziishi, ila nguvu ya kazi inaisha, tuitumie vizuri wakati tunayo.
LikeLike