3065; Maumivu hayajatosha.
Rafiki yangu mpendwa,
Sisi binadamu ni viumbe wa tabia, huwa tunaanza kujenga tabia, kisha tabia zinatujenga.
Asilimia kubwa ya yale tunayofanya kila siku, tunayafanya kwa tabia na mazoea na siyo kwa fikra.
Hilo ndiyo huleta upinzani mkali sana kwenye mabadiliko.
Watu huwa hawapo tayari kuachana na tabia na maumivu yao.
Njia pekee ya hilo kuwezekana ni kuyafanya maisha ya sasa kuwa magumu na yenye maumivu makali kiasi kwamba huwezi kuendelea kuvumilia.
Ni pale maumivu yanapokuwa hayawezi kuvumilika ndiyo mabadiliko huwa yanafanyika.
Kama maumivu yanavumilika, wengi huona bora waendelee na maumivu hayo kidogo kuliko kwenda kuanza kitu kipya kabisa.
Unafikiri ni kitu gani kinawafanya watu wabaki kwenye ajira ambazo hawazipendi na haziwalipi vizuri?
Pia unafikiri ni kitu gani kinawafanya watu waendelee kubaki kwenye biashara wasizozipenda na zisizowalipa vizuri?
Kote jibu ni moja, watu wanayaogopa maumivu ya badaliko kuliko maumivu ya kubaki kwenye mazoea waliyopo.
Kuna vitu viwili vya uhakika kuhusu mabadiliko ambavyo ndiyo hukwamisha wengi kubadilika.
Kitu cha kwanza ni kila mabadiliko huwa yanakuja na gharama zake.
Kitu cha pili ni kukosekana kwa uhakika wa matokeo mazuri.
Ili uweze kuvuka vitu hivyo viwili kwa uhakika, lazima uyakuze maumivu ya popote ulipo sasa.
Yafanye maumivu ya kubaki pale ulipo sasa kuwa makubwa sana kuliko maumivu ya mabadiliko.
Ukiona bado unakwama kwenye kubadilika, jua maumivu bado hayajakutosha, unaweza kuyavumilia.
Ukijikuta kwenye hali hiyo ya kukosa msimamo wa mabadiliko, ni muhimu uendelee kujisukuma mwenyewe kwa kujipa maumivu makali sana unapobaki pale ulipo.
Jipe maumivu ambayo huwezi kuyavumilia hata kwa muda mfupi ili wakati wote uwe mtu wa kuyakabili mabadiliko na kuyatumia kwa manufaa.
Nimalizie kwa hadithi fupi, ambayo nimewahi kuishirikisha ila nitairudia tena hapa ili tupate funzo.
Jirani mmoja alisikia mbwa wa jirani yake akibweka kwa uchungu mkali na kwa muda mrefu.
Jirani huyo alishindwa kuvumilia ubwekaji huo wa mbwa na kuamua kwenda kwa jirani yake kuona nini kinaendelea.
Alipofika alishangazwa kumwona jirani yake akiwa amekaa anasoma gazeti bila wasiwasi wowote, huku pembeni yake mbwa akiwa amekaa kwenye moto na kuendelea kubweka.
Mtu huyo alimuuliza jirani yake iweje amekaa kwa utulivu wakati mbwa anapata maumivu ya kuungua moto.
Jirani huyo alimjibu kwa upole; huyo mbwa hajafungwa kukaa hapo, yuko huru kutoka hapo alipo, lakini kwa sababu anaweza kuyavumilia maumivu hayo, amechagua kuendelea kuyavumilia badala ya kuamua kuondoka.
Rafiki, ni maumivu gani unayoyang’ang’ania kwenye maisha yako ili tu ubaki kwenye mazoea badala ya kwenda kwenye mabadiliko?
Ni wakati sasa wa kukuza maumivu ya chochote ambacho unataka kukibadili ili usijidanganye na kuyakwepa mabadiliko.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kama maumivu yanakuumiza utachukua hatua na kubadilika haraka, ila kama unaona watu wanavumilia na hawachukui hatua maana yake wameridhika na hali hiyo ya maumivu.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
maumivu yangu ni kutokufikia lengo la mauzo kwa muda sasa.
LikeLike
Umeridhika na matokeo unayopata.
LikeLike
Kweli, ni maumivu bado hayajatosha.
LikeLike
Yakiwa hayavumiliki, mtu unachukua hatua sahihi.
LikeLike
Ukiona bado unakwama kwenye kubadilika, jua maumivu bado hayajakutosha, unaweza kuyavumilia.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hakika Huwezi kuendelea kuvumilia ikiwa maumivu unayoyapata ni Makali zaidi otherwise utakuwa unayaoenda
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mbaya zaidi ni pale maumivu yanapokuwa yamezidi na kufyonza hata nguvu ya mabadiliko.
Kurasa hii imenifikirisha na kukumbuka kifo cha kusikitisha cha simba Bobjunio niliona akipigana sana kujinusuru lakini dakika ya mwisho akashindwa kabisa na hapo ndio ukawa mwisho wake.
LikeLike
Asante sana kwa kuongeza tafakari hii.
Angalau hata yeye alijaribu kupambana.
Kuna wengi wanakubali kushindwa bila hata kupambana kabisa.
LikeLike
Hakuna mabadiliko bila kuwa na maumivu.Licha ya kutokua na uhakika kwenye mabadiliko,maumivu yakikuchosha utaamua kubadilika na kuchagua maumivu mengine.Watu wakiridhika jua hawajaumia vya kutosha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hili ni Kweli kocha maumivu yakiwa ni makali hufanya mabadiliko haraka sana.
LikeLike
Asante.
LikeLike
Ukiona unakwama kwenye Kubadilika, jua badao maumivu hajakutosha, unaweza kuyavumilia
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ahsante sana kocha Kwa Uzi wa Leo
Ili kuondoka kwenye mazoea napaswa kujitengenezea maumivu ambayo nadhani nisipoondoka pale nitakuwa masikini kitu ambacho kwangu ni kosa kubwa Sana.
Naenda kujenga zaidi maumivu makali kwenye mazoea niliyonayo.
✅🤝🔥
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni pale maumivu yanapokuwa hayawezi kuvumilika ndiyo mabadiliko huwa yanafanyika.
Kama maumivu yanavumilika, wengi huona bora waendelee na maumivu hayo kidogo kuliko kwenda kuanza kitu kipya kabisa.
Asante sana
LikeLike
Asante sana.
LikeLike
Nimejifunza njia Bora ya kufanya mabadiliko ni :
Kujipa hisia za maumivu ambayo huwezi kuyavumilia hata kwa muda mfupi ili kila wakati niwe na uwezo wa kuyakabili mabadiliko na kuyatumia kwa manufaa.
Asante Sana kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Maumivu bado hayajanitosha kabisa, naweka kuyavumilia.
LikeLike
Hupaswi kuvumilia, unapaswa kuchukua hatua.
LikeLike
Asante kocha,Sintaweza kuvumilia maumivu lazima nifanye mabadiliko ili niweze kuwa na uhuru wa kifedha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
nitabadilika na sitoogopa maumivu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hapo kwenye maumivu kazi ipo. Wengi hatutaki maumivu
LikeLike
Na hapo ndipo tunapokwama.
LikeLike
Ni wakati sasa wa kukuza maumivu ya chochote ambacho unataka kukibadili ili usijidanganye na kuyakwepa mabadiliko.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Maumivu yakitosha utabadilika tu.
LikeLike
Hakuna ubishi.
LikeLike
Ni kweli kabisa kuwa maumivu bado hayajatosha ndiyo maana inachukua muda mtu kuchukua hatua. Asante kocha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Maumivu yangu kuona nafanya mabadiliko yakifikia mauzo na kuzidi,kweli hayajatosha hebu nipambane
LikeLike
Mapambano ni lazima.
LikeLike
Niko hapa kwaajili ya kiwango cha maumivu ninachopata kinakimudu, lakini nahitaji sana kupata maumivu mengine mapya na magumu ili niondoke hapa
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike