3085; Hamasa na kufanya.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna kitendawili kikali sana kwenye hamasa na kufanya kama ilivyo kwenye yai na kuku.
Watu huwa wanatumia muda mwingi kujadiliana kipi kilianza kati ya yai au kuku.
Inakuwa kitendawili kikali kwa sababu ukisema yai lilianza, utaulizwa lilitagwa na kuku yupi?
Na ukisema kuku alianza, utaulizwa kutoka kwenye yai gani?
Ukweli wa kitendawili hicho ni chochote kinaweza kuwa kilianza na haileti tofauti yoyote.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye hamasa na kufanya.
Watu wengi huwa wanasubiri mpaka wapate hamasa ndiyo wafanye kile walichopanga kufanya.
Halafu kwa bahati mbaya sana, hiyo hamasa haiji na hivyo wanajikuta wakisubiri kwa muda mrefu bila kufanya.
Ukweli ni kwamba, hamasa na kufanya vibakwenda pamoja, kila kimoja kikiweza kumchochea mwenzake.
Kama huna hamasa ya kufanya, hupaswi kusubiri mpaka hamasa ije ndiyo uanze kufanya.
Badala yake unatakiwa uanze kufanya hivyo hivyo na utaweza kujijengea hamasa ya kuendelea kufanya.
Kwa kufanya, unachochea hamasa inayokuwezesha kuendelea kufanya zaidi.
Kama wakati wowote ule utaamua kuamka na kuanza mwendo, maisha yatafunguka sana kwako.
Lakini kama utasubiri mpaka uwe na hamasa ndiyo ufanye, kamwe hutaweza kuanza.
Hamasa huwa ni zao la kufanya kama ambavyo kufanya pia ni zao la hamasa.
Hivyo kila unapokuwa na wasiwasi wa aina yoyote ile, anza kufanya kitu chochote kile.
Kila unapojiona huna hamasa, anzisha mwendo wowote ule.
Kwa kuwa kwenye mwendo, utaweza kubadili hali yako kutoka kutokuwa na hamasa mpaka kuwa na hamasa.
Usisubiri mpaka uwe na hamasa ndiyo ufanye yale uliyopanga kufanya.
Badala yake anza kufanya na hilo litakujengea hamasa ya kuendelea kufanya.
Kama ilivyo kwa kanuni ya mwendo, kitu kilichosimama huwa kinaendelea kusimama na kilicho kwenye mwendo huwa kinaendelea na mwendo.
Usikubali kusimama kwa sababu yoyote ile.
Mara zote endelea kuwa kwenye mwendo, hilo litajenga hamasa kubwa kwako itakayoendelea kukusukuma kuwa bora zaidi ya ambavyo upo sasa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Fanya na kisha hamasa ya kufanya itakuja.Asante kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitaanza kufanya hamasa nitakutana nayo huko huko
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitaendelea kufanya ili kuchochea hamasa ndani yangu katika biashara yangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hamasa na mwendo hufanya kazi pamoja, asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hamasa inachowewa zaidi kwa kufanya kwa msimamo
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni bora uanze kufanya, hamasa itakuja baadaye! Asante Kocha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hamasa inakuja kwa kuanza kufanya ,nimechagua kufanyia kazi niliyopanga kutekeleza ili nipate hamasa ya kuendelea kuliko subiri kuhamasishwa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ni bora kuanza au kuendelea kufanya ili kuchochea hamasa zaidi. Asante sana kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha,Nitaendelea na mwendo wa kufanya kazi ili niwe na hamasa na ubora zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitafanya kwa vitendo na sitosubiri mpaka nipate hamasa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Hamasa ni zao la kufanya kama ambavyo kufanya ni zao la Hamasa
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante, nitakuwa kwenye mwendo daima; sitasubiri hamasa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hamasa na kufanya vyote vinachocheana.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ukweli ni kwamba, hamasa na kufanya vibakwenda pamoja, kila kimoja kikiweza kumchochea mwenzake.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hamasa huwa inakuja kwa kufanya, kama huna hamasa anza kufanya na kaa katika kanuni ya mwendo na hamasa itakuja yenyewe.
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha,nitafanya na hamasa itNifuata.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Sitasubiri hamasa ili kufanya bali nitafanya ili kupata hamasa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni kweli kabisa kwa mfano kuna muda huwa naona uvivu kufua nguo nilizo zikusanya kwa muda mrefu, lakini nikisema nichukue mbili au tatu nizifue utakuta moyo na roho ingine inasema kwanini usimalizie zote ili kesho uendelee na mambo mengine hizi habari za nguo chafu ziwe zimeondoka…
Mara moja naanza kufua zote kwa kutegemea huo msukumo wa nguo chache nilizoanza nazo
LikeLike
Vizuri kwa mfano huu wa uhalisia kabisa, ndivyo mambo yanavyokuwa.
Lakini pia, muda unaotumia kufua si ungepaswa kuwa unauza zaidi halafu umlipe mtu au mashine ikufulie nguo?
LikeLike
Usisubiri mpaka uwe na hamasa ndiyo ufanye yale uliyopanga kufanya.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Usisubiri mpaka uwe na hamasa ndiyo ufanye yale uliyopanga kufanya fanya hamasa itafuata.
LikeLike
Asante sana kocha,nitaanza kufanya na hamasa itakuja sitasubili
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Lakini kama utasubiri mpaka uwe na hamasa ndiyo ufanye, kamwe hutaweza kuanza.
LikeLike
Kabisa
LikeLike