3087; Ni vita kubwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Msimu wa HAPANA ambao tupo ni moja ya misimu migumu sana kwenye maisha yetu.
Hiyo ni kwa sababu kupanga kusema HAPANA ni rahisi, lakini kumwangalia mtu usoni na kumwambia HAPANA ni zoezi gumu sana, ambalo wengi wanalishindwa.
Watu wengi wanakwama kwenye kusema HAPANA kwa sababu wanataka wamkatalie mtu kitu lakini wawaache watu hao wakiwa na furaha pia.
Ili kutimiza hilo, wamekuwa wanawaambia watu HAPANA ambazo ni nyepesi, zikiambatana na maelezo mengi yasiyokuwa muhimu.
Kinachotokea ni HAPANA zao zinakosa nyuvu na kujikuta wameshawishika na kukubali kitu ambacho walipanga kukikataa.
Kila mara unaposema NDIYO kwenye jambo ambalo ulipanga kusema HAPANA, unashusha hadhi na thamani yako. Unajidharau na kujiona huna mamlaka juu ya maisha yako. Hilo linafanya HAPANA yako nyingine iwe ngumu zaidi.
Zoezi la kusema HAPANA ni vita kubwa sana.
Kwa sababu unawakatalia watu kitu ambacho tayari walishajipanga kukipata kutoka kwako.
Hawatakubaliana na wewe kirahisi kwenye hilo.
Ili HAPANA yako iwe na nguvu, inapaswa kuelezwa kwa wazi na isiambatane na maelezo mengi.
Hilo linataka uwe tayari kuonekana una roho mbaya na hujali.
Ni vyema uwe tayari kupokea yote ambayo watu watayaleta kwako kwa sababu umewakatalia.
Usigeuze HAPANA yako kuwa NDIYO kwa sababu tu unataka kuwafurahisha watu wengine.
Huwezi kumfurahisha kila mtu na pia siyo wajibu wako kufanya hivyo.
Ni wajibu wa kila mtu kujifurahisha mwenyewe kwenye maisha yake.
Watu wanaokujali na kukuheshimu, watakubaliana na HAPANA yako na kuendelea kushirikiana na wewe kwenye mambo mengine muhimu na yanayoendana na NDIYO zako.
Lakini watu wasiokujali wala kukuheshimu, ambao wanataka kukutumia kwa manufaa yao, watakataa HAPANA zako na kulazimisha wapate kile wanachotaka wao bila kujali kuhusu wewe.
Hapo ndipo ilipo vita niliyokuambia,
Kwa sababu unahitaji kupambana na wote wanaokataa mipaka unayoweka kwenye maisha yako.
Kusema HAPANA ni kuweka mipaka na mtu anayekataa HAPANA zako ni sawa na anafanya uvamizi kwenye mipaka yako, kitu ambacho ni vita kubwa.
Unaposema HAPANA, imaanishe kweli na isimamie. Usijali sana upande wa pili umechukuliaje HAPANA yako, unachohitaji ni kulinda mipaka yako isishambuliwe na matakwa ya wengine.
Acha kutaka kuonekana mwema kwa kila mtu.
Acha kutaka kumfurahisha kila mtu.
Acha kusema NDIYO kwenye mambo ambayo ndani yako unajua yanatakiwa kuwa kwenye HAPANA.
Ukiweza kuishinda vita hii kubwa ambayo silaha yake ni neno HAPANA, utaweza kuweka mipaka sahihi kwenye maisha yako.
Mara zote kumbuka upo kwenye vita ya kulinda muda wako, nguvu zako na umakini wako.
Ukiwa mwepesi mwepesi utaburuzwa sana na wengine kwenye hayo maeneo matatu muhimu.
Matokeo yake ni unajikuta kila siku unachoka sana, lakini ukiangalia hakuna makubwa uliyokamilisha.
Matumizi sahihi ya neno HAPANA yatakuwa mkombozi mkubwa kwako.
Hii vita ingekuwa rahisi, kila mtu angekuwa ameshinda kwenye eneo hilo.
Siyo vita rahisi ndiyo maana wengi wanashindwa na kurudi kwenye maisha yao ya mazoea.
Wewe usikubali kurudi nyuma, songa mbele kama ulivyopanga, tumia neno HAPANA kwa usahihi na msimamo ili uweze kulinda yale muhimu zaidi kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Matumizi ya neno HAPANA yatakuwa mkombozi mkubwa kwako.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kusema hapana ni vita kubwa kwani unapambana kutowapa watu kile ambacho walishapanga kukipata kutoka kwako na wakati mwingine ni Kwa manufaa yao binafsi
LikeLike
Ingekuwa rahisi isingekuwa na maana.
LikeLike
Acha kutaka kuonekana mwema kwa kila mtu.
Acha kutaka kumfurahisha kila mtu.
Acha kusema NDIYO kwenye mambo ambayo ndani yako unajua yanatakiwa kuwa kwenye HAPANA.
Ukiweza kuishinda vita hii kubwa ambayo silaha yake ni neno HAPANA, utaweza kuweka mipaka sahihi kwenye maisha yako
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hakika ni vita inahitaji ujasiri kusema hapana
LikeLike
Siyo rahisi.
LikeLike
Hshindi unatokana na kusema hapana kwa wale aanapnipokonya rasilimali zangu muda fedha umakini wangu na kumbe hapana ni hapana isiambatane na maelezo
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ahsante sana, kocha nitasema hapana siku zotebili kulinda mipaka
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ninalinda muda,nguvu na umakini wangu kwa usema hapana kila wakati kwa yale ambayo hayanamchango kwenye kupiga hatua kubwa katika maisha yangu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kwa hakika vita hii ni ya kihisia zaidi na namna ya kuishinda lxima uwe mkomavu wa kihisia
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitatumia neno hapana ili kuweza kulinda muda wangu, heshima yangu na mambo yote ambayo hayana mchango na mimi.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Najua ni vita, lakini kama mpambanaji nimejiandaa kushinda,hivyo nitaendelea kutumia neno HAPANA ili kuokoa muda wangu na pesa zangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Nitatumia HAPANA kwa kusimamia mambo yangu sio kumfurahisha kila mtu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni rahisi kupanga au kusema kuwa utatumia neno HAPANA kwa yale ambayo hayaleti tija kwetu, lakini wakati wenyewe wa kulitumia ukifika inakuwa ngumu kufanya hivyo. Kwa maana hiyo ni kweli kabisa kuwa hii ni vita kubwa ambayo hatuna namna zaidi ya kupigana ili kufikia malengo yetu. Asante sana kocha
LikeLike
Lazima tuwe na ujasiri mkubwa ili kushinda hilo.
LikeLike
Unaposema HAPANA, imaanishe kweli na isimamie.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Tumia neno hapana kwa usahihi na msimamo ili uweze kulinda yale muhimu zaidi kwako
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana Kocha, kusema NDIYO ili kuwafurahusha watu baadala ya HAPANA ni usaliti mkubwa sana wa nafsi yako.
LikeLike
Hakika
LikeLike
huwezi kumfurahisha kila mtu, na sio jukumu lako kufanya hivyo.
kila mtu atafute furaha yake mwenyewe.
LikeLike
Kabisa, watu wasiwe wavivu kututegemea tuwape furaha.
LikeLike
Usigeuze HAPANA yako kuwa NDIYO kwa sababu tu unataka kuwafurahisha watu wengine.
Huwezi kumfurahisha kila mtu na pia siyo wajibu wako kufanya hivyo.
Asante sana
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Neno hapana limekamilika halina nyongeza. Asante kocha.
LikeLike
Ni sentensi kamili.
LikeLike
Nitasema hapana kwa kila kitu kinachoitaji kusema hapana.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Kusema hapana ni kuweka mipapaka, na mtu anaekata
a hapana zako ni sawa na kufanya uvamizi kwenye mipaka yako kitu ambacho ni vita kubwa.
Asante kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitaendelea kusema hapana
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Zoezi la kusema hapana ni vita kubwa sana.
LikeLike
Siyo kidogo.
LikeLike
Kutumia neno Hapana kunalipa sana. Na mimi nitahakikisha nalitumia sana kwani ndiyo litakalonivusha kwenye mambo yangu mengi.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Acha kutaka kuonekana mwema kwa kila mtu.
Acha kutaka kumfurahisha kila mtu.
Acha kusema NDIYO kwenye mambo ambayo ndani yako unajua yanatakiwa kuwa kwenye HAPANA.
Ukiweza kuishinda vita hii kubwa ambayo silaha yake ni neno HAPANA, utaweza kuweka mipaka sahihi kwenye maisha yako.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mara zote ninanapaswa kukumbuka kwamba Niko ktk
Vita kubwa ya kulinda muda wangu, nguvu zangu, pia umakuni wangu.
Hivyo matumizi sahihi ya neno HAPANA
Litakuwa mkombozi kwangu.
Asante Sana kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike