3107; Kitu pekee kinachokuzuia.
Rafiki yangu mpendwa,
Ni ukweli usiopingika kwamba ili kupata mafanikio makubwa, lazima uchukue hatua kubwa sana.
Hatua ambazo hujawahi kuzichukua na wala hazijazoeleka kwa wale wanaokuzunguka.
Wale wote waliofanikiwa sana, huwa wanalijua hilo vizuri na wanalitekeleza. Wanajua hakuna mbadala wa kuchukua hatua kubwa, hivyo wanaanza kufanya hivyo mapema kabisa.
Tatizo lipo kwa wale ambao hawajafanikiwa.
Ukiwauliza kwa nini hawajafanikiwa, watakupa sababu nyingi sana na nzuri, zinazoweza kukushawishi.
Lakini sababu zote hizo wanazokupa zinakuwa za uongo.
Watakuambia wametokea kwenye mazingira magumu.
Watakuambia wana wategemezi wengi.
Watakuambia wamekosa kipaji na uwezo wa kipekee ambao wengine wanao.
Watakuambia hawana bahati.
Kitu kimoja ambacho hawatakuambia, ambacho ndiyo kweli kinawazuia ni uvivu.
Hutawasikia wakisema hawajafanikiwa kwa sababu ya uvivu wao wa kushindwa kuchukua hatua kubwa na za tofauti.
Inapokuja kwenye safari ya mafanikio, uvivu ndiyo kikwazo cha kwanza kinachowazuia walio wengi.
Sababu nyingine ambazo watu wanazitoa, ni matokeo tu ya uvivu.
Lakini kiini hasa cha kushindwa au kukosa ni uvivu.
Wengi hukataa hili kwa sababu huwa wanadhani kujishughulisha na mambo mengi ndiyo uchapa kazi.
Watakuambia wanaamka mapema, wanachelewa kulala na muda mwingi wanaweka kwenye kazi.
Lakini ukichunguza huo muda wanaokuwa wameweka kwenye kazi, sehemu kubwa ya muda huo wanakuwa wanaupoteza kwenye mambo yasiyokuwa na tija, yasiyo na mchango kwenye mafanikio wanayoyataka.
Ingekuwa kuweka muda mwingi kwenye kazi ndiyo mafanikio, masikini wengi ndiyo wangefanikiwa zaidi, maana wana muda mwingi wa kuweka kwenye jambo lolote lile na huwa wanaupoteza sana muda huo.
Kuchukua hatua kubwa sana na za tofauti kwa msimamo na muda mrefu bila kuishia njiani ndiyo mahali pa kuanzia kwenye safari ya mafanikio.
Utahangaika na mengi, lakini kama hutaanzia hapo kwenye kuchukua hatua kubwa na za tofauti, utajidanganya sana.
Tuchukue mfano wa mauzo, ambayo ni hitaji muhimu sana kwa kila biashara ili iweze kufanikiwa.
Kuna kuuza kawaida, kufungua biashara na kuwasubiri wateja waje kwenye biashara, kisha kuwauzia kawaida. Matokeo ya hilo yapo wazi, ni biashara ya kawaida ambayo itaandamwa na changamoto za kila aina.
Kuuza kwa tofauti kunahusisha kuwafikia wateja kule walipo, kuwashawishi kununua na kuwapa huduma bora kabisa ambayo hawajawahi kuipata mahali pengine.
Matokeo ya hilo ni biashara kuwa yenye mafanikio makubwa.
Kama utachukua hatua kubwa na za tofauti kwenye mauzo, lazima biashara itapata mafanikio makubwa.
Kama kila muuzaji atakuwa na sharti hili, kwa muda wote aliopo kwenye biashara, atakuwa anafanya mambo mawili tu, kuwa anaongea ana kwa ana na mteja au kuwa anawasiliana naye kwenye simu.
Kwa kutekeleza hilo kwa uhakika bila ya kupoteza muda kwenye mambo mengine yasiyokuwa na tija, lazima utazalisha matokeo makubwa na ya tofauti.
Sasa hebu niambie ukweli kabisa kutoka ndani ya moyo wako, nini kinakuzuia usichukue hatua kubwa na za tofauti kwenye yale unayofanya?
Utasema mengi, lakini utakataa kata kata kutaja uvivu kama kikwazo kikuu kwako.
Na kwa kutokuutaja uvivu, unaupa nguvu ya kuendelea kuwa kikwazo kwako kufanikiwa.
Kama mpaka sasa bado hujafanikiwa, na hapa mafanikio yakiwa ni ile aina ya maisha unayotaka kuwa nayo, kinachokuzuia ni kitu kimoja tu; UVIVU.
Ukiamua sasa kuachana na uvivu, ukaweka juhudi kwenye kuchukua hatua kubwa na za tofauti kwenye yale unayofanya, kwa msimamo na muda mrefu bila kuacha, huwezi kubaki hapo ulipo sasa.
Swali ni je utaukana uvivu na ufanye?
Au utaendelea kuuficha nyuma ya sababu mbalimbali unazojipa?
Ukabili ukweli ili ufanikiwe au jifiche nyuma ya uongo na usifanikiwe.
Maisha ni yako na maamuzi ni yako.
Muhimu tu ni ukiamua kujidanganya, usitake na wengine nao wakubaliane na uongo wako ili kukupa faraja.
Wasiofanikiwa ndiyo watakupa faraja kwenye uongo wako.
Waliofanikiwa watajua wazi unapokwama, ambapo ni kwenye uvivu na hawatakuonea huruma wala kukupa faraja kwenye hilo.
Ukabili ukweli ili upate mafanikio makubwa unayoyataka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Wasiofanikiwa ndio watakupa faraja kwenye uongo wako. Ukabili ukweli ili upate mafanikio makubwa unayoyataka.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitaendelea kuukabili ukweli Ili nipate mafanikio makubwa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kinachonikwamisha ni uvivu
LikeLike
Ushinde.
LikeLike
Nitajitahidi sana kujitenga na uvivu na uongo kwa kufanya yaliyo ya muhimu kwangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Uvivu ni kitu cha hatari sana.Uvivu ubapenda kujificha kwenye sababu ambazo si za kweli ila kutaka kuonekana ni za kweli kabisa na uba haki kwenye hilo.
LikeLike
Kweli
LikeLike
Kama kila muuzaji kwenye biashara yake atakuwa anafanya mambo mawili tu, kuwa anaongea ana kwa ana na mteja au kuwa anawasiliana naye kwenye simu na bila ya kupoteza muda kwenye mambo mengine, lazima atazalisha matokeo makubwa na ya tofauti sana. 🙏🙏
LikeLike
Hilo ni uhakika kabisa.
LikeLike
Ni kweli sababu kuu ni uvivu na uzembe na sababu nyingine ni kisingizio cha mbali sababu kuu ni uvivu na uzembe
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Huu ni ukweli kuwa pamoja na sababu zote zinazotufanya tusifanikiwe kwenye maisha sababu zilizo kuu ni uvivu na uzembe. Nitajitahidi kuepukana na uvivu na uzembe ili niweze kufikia malengo yangu. Asante kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha,
Kiini hasa cha kushindwa au kukosa ni UVIVU.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ukabili ukweli ili ufanikiwe au jifiche nyuma ya uongo na usifanikiwe.
Maisha ni yako na maamuzi ni yako.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kiini cha kushindwa na kukosa ni uvivu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Huu ndio ukweli kuhusu mafanikio
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ukabili ukweli ili upate mafanikio makubwa unayoyataka.
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hakika @kochadrmakirita
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Adui yangu katika mafanikio ninayoyataka ni uvivu tu,hakuna kingine.
LikeLike
Pambana na adui huyo.
LikeLike
Uvivu kweli na adui mkubwa wa kupambana nae mara zote
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Uvivu, Uvivu, Uvivu.
LikeLike
Sumu mbaya sana hiyo.
LikeLike