3110; Raha kufanya.
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa kuna kauli mbili ambazo huwa zinawachanganya watu wengi.
Ya kwanza inasema; Fanya kile unachopenda kufanya na fedha zitakufuata zenyewe.
Ya pili inasema; Kama unataka mafanikio makubwa usifanye kazi, bali fanya kile unachopenda.
Mkanganyiko ambao umekuwa unatokana na kauli hizo ni imani ambayo watu wengi wanayo kwamba vitu vingi ambavyo watu wanapenda kufanya, havifai kugeuzwa kuwa ndiyo kazi yao kuu ya kuwaingizia kipato.
Lakini huo siyo ukweli, hakuna kitu chochote ambacho mtu anakipenda kweli kisichofaa kugeuzwa kuwa kazi kuu ya kumwingizia mtu kipato.
Ambacho watu wengi wanakosa ni ujuzi wa kugeuza kile wanachopenda kufanya kuwa shughuli inayowaingizia kipato.
Kwa kifupi ujuzi wa kutengeneza kipato ndiyo unaokuwa unakosekana kwa wengi.
Njia pekee ya kuweza kupata mafanikio makubwa ni kufanya kile unachopenda kufanya, ambacho ndiyo kinakupa raha.
Hilo ni muhimu kwa sababu mpaka ufanikiwe itakuchukya muda na utapitia mengi magumu.
Kama kitu unakuwa hujakipenda kweli, hutaweza kuhimili magumu hayo na kuyavuka.
Kama unajiambia kile unachopenda hakiwezi kugeuzwa kuwa njia ya kuingiza kipato, unachomaanisha ni bado hujawa na ujuzi huo.
Hivyo unachohitaji ni kujenga ujuzi huo wa kugeuza kile unachopenda kuwa ndiyo njia kuu ya kukuingizia kipato.
Ujuzi wowote ule huwa unachukua muda kwenye kujifunza na kuufanya mpaka uwe kitu ambacho umekizoea.
Unahitajika kujifunza na kufanya kila siku bila kuacha kwa miaka mingi.
Na hapo ndipo sehemu nyingine ambayo wengi wamekuwa wanakwama.
Hakuna kitu chochote ambacho utajifunza na kukifanya kila siku halafu ukashindwa kuwa bora kwenye kitu hicho.
Hata kile ambacho unaanza ukiwa hukipendi, baada ya kuwekeza muda mwingi kwenye kitu hicho, mtazamo wako unabadilika.
Kadiri unavyokielewa kitu, unavyokuwa vizuri kwenye kukifanya ndivyo unavyozidi kupenda kitu hicho.
Hiyo ina maana kwamba ili upate mafanikio makubwa, siyo lazima uanze na kile ambacho tayari unakipenda sana.
Badala yake unaweza kujenga mapenzi makubwa kwenye kitu chochote kama utawekeza muda na juhudi za kutosha kwenye kujifunza na kufanya kitu hicho.
Umuhimu wa kuwa unapenda kile unachofanya ni kuweza kuendelea kufanya licha ya magumu na changamoto ambazo mtu anakutana nazo.
Lakini hilo linaanzia kwenye kujilazimisha kufanya kitu kila siku bila kuacha.
Hapo ndipo msingi mkuu wa mapenzi kwenye kitu unapojengwa.
Huwezi kufanya kitu kila siku bila kuacha halafu usiwe bora kwenye kitu hicho.
Na ili uendelee kufanya kila siku bila kuacha, lazima kitu kiwe kinakupa raha unapokifanya.
Kwa raha hiyo unakuwa tayari kurudia rudia kufanya kitu kinachokujengea ubobezi mkubwa.
Ni lazima mtu ujitoe sana kwenye kufanya kile ulichochagua kuwa njia yako kuu ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Ni lazima uendelee kujenga ubobezi kadiri unavyokuwa unaendelea kufanya.
Hilo linataka uanze na kiu kubwa ya kutaka kuwa bora zaidi, mtazamo chanya ya kujifunza na kujaribu vitu vipya, msimamo mkali kwenye kile unachofanya, uvumulivu na unyenyekevu.
Kwa kuwa na hayo, unaweza kugeuza chochote unachopenda kufanya kuwa ndiyo msingi mkuu wa mafanikio yako makubwa.
Muda lazima uwekwe, usidanganyike na njia za mkato.
Juhudi kubwa lazima ziwekwe, usidanganyike na vitu rahisi.
Uvumilivu mkubwa unahitajika, usidanganyike na kulala masikini na kuamka tajiri.
Unga’ng’anizi unahitajika sana, usidanganyike na kukimbilia mambo mapya na rahisi kile unapokutana na ugumu.
Kwa sababu ndiyo kitu unachopenda sana kufanya,
Kwa sababu ndiyo kitu kinachokupa raha kufanya,
Haimaanishi kwamba kitakuwa rahisi kwako kufanya.
Ugumu, changamoto na vikwazo havitakosekana kwenye kitu chochote unachochagua kufanya.
Jua wajibu wako ni kufanya na kuendelea kuwa bora kila siku kwenye hicho unachofanya.
Ukiyaangalia maisha yako mpaka kufika hapo ulipo sasa, hakuna kitu chochote ambacho umewahi kukitaka kweli na ukakikosa.
Chochote ulichokitaka hasa na kuwa tayari kujitoa kwa kila namna ili kukipata, uliishia kukipata.
Hivyo basi, unaweza kupata mafanikio makubwa unayoyataka kupitia kile unachopenda zaidi kufanya na kinachokupa raha kufanya.
Uzuri ni ukishakuwa unakipenda kweli kitu, utaweza kuvuka yote unayokabiliana nayo.
Utaweza kuweka kazi kwa muda mrefu bila kuchoka au kukata tamaa.
Mwisho wa siku, haijalishi nini kilianza, iwe ni ulianza kupenda kitu kisha ukakifanya au ulianza kufanya kitu ndiyo ukakipenda.
Muhimu ni ili upate mafanikio makubwa, lazima uwe unapenda sana kile unachofanya, kiwe ndiyo kinachokupa raha kubwa kwenye maisha yako.
Nje ya hapo utaweza kupata mafanikio ya kawaida, lakini siyo yale ambayo ni makubwa kabisa na ya kuwashangaza wengi.
Kila kitu kwenye maisha kinahitaji ujuzi.
Na ujuzi unajengwa kwa kujifunza na kufanya kila siku bila kuacha.
Hivyo hapo tunapata kanuni rahisi na ya uhakika ya kufanikiwa kwenye kitu chochote.
Jifunze na kukifanya kila siku bila kuacha.
Ukishaweza kujifunza na kufanya kila siku, kinachokuwa kimebakia ni muda tu.
Ni swala la muda kabla hujapata kile hasa unachotaka.
Hivyo uvumilivu na unga’ng’anizi vinahitajika sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Jifunze na kukifanya kila siku bila kuacha.
Penda kile unachofanya na utajikuta huna kazi ya kufanya kwa maumivu.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ukiweza kujifunza na kufanya kila siku bila kuacha, kinachokuwa kimebakia ili kufanikiwa ni muda tu.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kufanya kila siku kwa msimamo bila kuacha kile unachokipenda na lazima kikuletee mafanikio makubwa ahsante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Sitakubali kudanganyika na njia za mkato,mara zote nitafanya kile ninachopenda kufanya ili kupata mafanikio makubwa, Asante sana kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha,kila kitu kwenye maisha kinahitaji ujuzi na kukifanya mara kwa mara bila kuacha,hivyo uvumilivu na kukaa kwenye mchakato utaweza kutufikisha kwenye mafanikio.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mafanikio yanatokana na kufanya kitu unachopenda . Jifunze kitu hicho na fanya kila siku kwa kurudia rudia na ukifanya hivyo mafanikio ni suala la muda tu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kufanikiwa ni kufanya bila kuacha.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Jifunze na kukifanya kila siku bila kuacha. Asante sana kocha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ukifanya kila kila siku kwa kijisukuma, muda utaamua matokeo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ukikitaka kitu sana ukakifanya utakipata.Kile unachopenda sana unajikuta unapata msukumo kukifanya bila ya kuchoka.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hiyo ina maana kwamba ili upate mafanikio makubwa, siyo lazima uanze na kile ambacho tayari unakipenda sana.
Badala yake unaweza kujenga mapenzi makubwa kwenye kitu chochote kama utawekeza muda na juhudi za kutosha kwenye kujifunza na kufanya kitu hicho.
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ninachopenda kufanya Ni kipaji nilichopewa na Mungu ndiyo kazinya uhakika naihitaji kushurutishwa. Inalipa hamasa isiyoisha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ung’ang’anizi unahitajika sana ili kufanikiwa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitajifunza na kufanya kila siku ili kupata mafanikio makubwa ninayoyaitaji kwenye maisha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Muda lazima uwekwe, usidanganyike na njia za mkato.
Juhudi kubwa lazima ziwekwe, usidanganyike na vitu rahisi.
Uvumilivu mkubwa unahitajika, usidanganyike na kulala masikini na kuamka tajiri.
Unga’ng’anizi unahitajika sana, usidanganyike na kukimbilia mambo mapya na rahisi kile unapokutana na ugumu.
普通话
LikeLike
Kabisa
LikeLike