3115; Kufanya na matokeo.
Rafiki yangu mpendwa,
Tumejifunza na kuzoea kwamba tunapofanya kitu, tunaona matokeo mara moja.
Hivyo inapotokea tumefanya kitu na hatuoni matokeo, basi tunaona tulichofanya siyo sahihi na hivyo tunaacha kukifanya.
Hayo ni mazoea mabaya ambayo tumejijengea na ambayo ni kikwazo kwetu kupata mafanikio makubwa.
Ukweli muhimu unaopaswa kuujua kuhusu mafanikio ni kwamba yanatokana na kufanya.
Na kila ufanyaji huwa unazalisha matokeo yake, ni vile tu matokeo huwa hayafanani.
Hakuna ufanyaji ambao huwa unaenda bure.
Kufanya ambako kunazalisha matokeo huwa kuna sifa tatu ambazo ni kama ifuatavyo;
Kufanya kwa ukubwa,
Kufanya kwa muda mrefu,
Na kufanya kwa msimamo bila kuacha.
Tofauti kati ya wanaoshinda na wanaoshindwa kwenye maisha huwa inaanzia mahali pamoja tu, ambapo ni ufanyaji.
Wanaoshinda wanazingatia ufanyaji kwa sifa zote tatu.
Wanaoshindwa huwa wanaacha kufanya kitu mapema kama hawaoni matokeo.
Kama huridhishwi na matokeo unayoyapata sasa, mahali pa kuanzia ni kwenye ufanyaji.
Hapo ndipo mkwamo mkubwa unapokuwa umeanzia.
Huenda hujafanya kwa ukubwa ambao unahitajika, kwa muda mrefu inavyohitajika na kwa msimamo bila kuacha.
Hakuna namna unaweza kutenganisha ufanyaji na matokeo, hata ufanye nini.
Watu wamekuwa wanakimbizana na njia za mkato tangu enzi na enzi, lakini haijawahi kupatikana njia ya uhakika ya mafanikio ambayo haihusishi kufanya.
Watu wamekuwa wanatumia muda mrefu kuahirisha kufanya yale wanayojua wanapaswa kuyafanya.
Muda wanaokuwa wameahirisha, hakuna chochote cha maana wanakuwa wanafanya, bali kuupoteza kwa mambo yasiyokuwa na tija.
Halafu wanashangaa kwa nini hawafanikiwi.
Halafu kuna wale ambao muda wote wametingwa.
Wapo ‘bize’ kweli kweli.
Wanamaliza siku zao wakiwa wamechoka sana.
Lakini wakiangalia, hakuna hatua wanazopiga.
Hawa wakisikia unawaambia hakuna kitu wanafanya, wanaona kama unawadhihaki.
Lakini ukweli unabaki pale pale, wanakuwa wameshindwa kufanya kwa usahihi.
Wanakosa vipaumbele, hivyo wanahangaika kufanya vitu ambavyo havina tija kabisa.
Kwa kila mafanikio unayokuwa unayataka, kuna vitu unapaswa kuvifanya ili kuyapata.
Ni muhimu sana ujipime kwenye ufanyaji wa vitu hivyo kama unataka kupata mafanikio makubwa.
Kama hujapata mafanikio unayoyataka, tatizo ni hujafanya kile unachopaswa kufanya ili ufanikiwe.
Na kama umefanya, basi siyo kwa ukubwa, muda na msimamo unaohitajika.
Kitu chochote sahihi unachofanya, ukakifanya kwa ukubwa, kwa muda mrefu na kwa msimamo bila kuacha, lazima kitakupa matokeo makubwa.
Jua kinachopaswa kufanyika na kifanye.
Usitafute njia za mkato.
Usiahirishe kufanya.
Usikate tamaa kwa kuona matokeo hayaji.
Usiridhike kwa matokeo madogo unayopata kwa haraka.
Kaa kwenye ufanyaji sahihi na utaweza kupata matokeo makubwa unayoyataka na yanayokupa mafanikio unayoyataka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kama hujapata mafanikio unayoyataka, tatizo ni hujafanya kile unachotakiwa kufanya ili ufanikiwe. Na umefanya sio kwa ukubwa, muda na msimamo unaohitajika.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Chochote ninachochogua kufanya nitafanya kwa ukubwa,muda na msimamo.Baada ya hapo ni matokeo tu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kama hujapata mafanikio unayoyataka, tatizo ni hujafanya kile unachotakiwa kufanya ili ufanikiwe. Na kama umefanya sio kwa ukubwa, muda na msimamo unaohitajika.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ukitaka matokeo makubwa
Fanya kwa usahihi
Fanya kwa muda mrefu
Fanya bila kuasha
Fanya kwa ukubwa na subiri utayaona matokeo
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kufanya ambako kunazalisha matokeo huwa kuna sifa tatu ambazo ni kama ifuatavyo;
Kufanya kwa ukubwa,
Kufanya kwa muda mrefu,
Na kufanya kwa msimamo bila kuacha.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kama hupati matokeo, basi shida inaanzia kwenye kufanya.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ahsante sana @,Kocha kwa makala hii
Sitakata tamaa wala kuacha kufanya kwa kutokuona matokeo ya ninachokifanya!!.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
nini.
Watu wamekuwa wanakimbizana na njia za mkato tangu enzi na enzi, lakini haijawahi kupatikana njia ya uhakika ya mafanikio ambayo haihusishi kufanya.
Asante sana
LikeLike
Kufanya hakukwepeki.
LikeLike
Kuzalisha matokeo itatokana na;
Kufanya kwa ukubwa,
Kufanya kwa muda mrefu,
Na kufanya kwa msimamo bila kuacha. Asante sana.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha,naona sasa kwenye biashara yangu tatizo ni ufanyaji, Mimi kama kiongozi nahitaji kukaa chini na kubadilisha/kuboresha namna ya ufanyaji kazi ili kupata mabadiliko ktk mauzo
LikeLike
Fanya.
LikeLike
Asante Kocha,
Ili nipate matokeo makubwa , nitafanya kile sahihi kwa ukubwa, kwa muda mrefu na kwa msimamo bila kuacha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
nji za mkato hazitotufikisha kwenye mafanikio makubwa
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Watu wamekuwa wanakimbizana na njia za mkato tangu enzi na enzi.
LikeLike
Ndiyo, na hawajawahi kuzipata.
LikeLike
Kwa msimamo, kwa ukubwa na kwa muda mrefu kwa mchakato nitapata matokeo makubwa na mazuri na sio njia za mkato.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ahsante sana, hakuna utofauti wa kufanya na matokeo
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante kocha,Nitakaa kwenye ufanyaji kazi na nitaweza kupata matokeo makubwa.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Nikweli kabisa hili ninaushuda Kwa maisha yangu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
ilikuona matokeo ya kazi unayofanya:-
Fanya kwa ukubwa
2.Fanya kwa muda mrefu
Fanya kwa muda msimamo bila kuacha.
Na hapa ndipo tunaposema kaa kwenye mchakato.
Asante
LikeLike
Mchakato haukwepeki.
LikeLike