3126; Usichezee ‘matirio’
Rafiki yangu mpendwa,
Hebu pata picha mtu amenunua basi lenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 30, lakini anaamua kulitumia kama usafiri binafsi.
Kwa hakika utashangazwa na jinsi rasilimali hiyo itakavyokuwa imetumika vibaya.
Au mtu ananunua kompyuta yenye uwezo mkubwa wa kurahisisha majukumu mengi, ila mtu anaamua kuitumia kusikiliza muziki pekee.
Japo mtu huyo anakuwa na uhuru wa kutumia vitu vyake atakavyo, anapovitumia chini ya kiwango kilichozoeleka, anaishia kuwashangaza watu.
Sasa njoo kwenye hili kosa ambalo umekuwa unalifanya kila siku.
Una akili na mwili wenye uwezo wa kufanya makubwa sana bila ya ukomo wowote.
Lakini unaamua kutumia uwezo huo mkubwa kufanya kazi au biashara yako kwa mazoea, kuangalia tv, kuzurura kwenye mitandao na kufuatilia maisha ya wengine.
Kwa hakika ni matumizi mabaya mno ya rasilimali kubwa ambayo tayari unayo.
Upo hapa duniani kwa kusudi maalumu, ambalo ni kugusa maisha ya watu wengi zaidi kwa namna chanya, na kuwaacha wakiwa bora zaidi ya walivyokuwa kabla ya kukutana na wewe.
Umekuwa kikwazo kwako wewe mwenyewe kwa muda mrefu sasa.
Kuna fursa nyingi za kufanya makubwa ambazo zimekuwa zinajitokeza ila umekuwa unashindwa kuzitumia vyema.
Na kwa hili huna cha kujitetea.
Unaweza kusema kuna vipaji ambavyo umekosa ndiyo maana umeshindwa kufanya makubwa.
Lakini kuna watu anbao wanafanya makubwa mno huku wakiwa na vipaji vichache kuliko wewe.
Matumizi sahihi ya ‘matirio’ makubwa uliyonayo ili uweze kuzalisha matokeo makubwa pia ni kama ifuatavyo;
1. Kuwa na malengo na mipango mikubwa ambayo unaifanyia kazi hatua kwa hatua.
2. Kujifunza endelevu ili kujenga ujuzi unaohitajika ili kupata kile unachotaka.
3. Weka kazi kubwa na kwa juhudi kubwa sana.
4. Jenga tabia sahihi ambazo zinarahisisha maamuzi yako na hatuz unazochukua.
5. Kuwa na fokasi kubwa na kujikinga na usumbufu wa kukimbizana na vitu vipya kila wakati.
Kwenda kinyume na hayo matano ni kujidharau wewe mwenyewe.
Kupoteza ‘matirio’ mengi uliyonayo kwa kuhangaika na mambo yasiyo na tija.
Wale unaowaona wamepiga hatua kubwa kuliko wewe, siyo kwamba wana uwezo mkubwa sana kukiko wewe, bali wamechagua kutumia vizuri uwezo ambao tayari wanao, ambao hata wewe mwenyewe unao pia.
Inzi na nyuki wote wanaruka ruka siku nzima.
Lakini wakati nyuki anaishia kuzalisha asali tamu na yenye manufaa, inzi anakuwa amesambaza magonjwa kwa kukaa kwenye vinyesi na mazingira mengine machafu.
Nyuki hatumii muda wake kumshawishi inzi aachane na mambo yake ya kijinga, bali anakazana na wajibu wake wa kuzalisha asali.
Amua sasa kama unakuwa nyuki au unakuwa inzi.
Usiharibu na kutumia vibaya uwezo mkubwa uliopo ndani yako.
Kwa chochote ambacho umeshaweza kufanya mpaka sasa, unaweza kufanya kwa ukubwa zaidi ya ulivyowahi kufanya.
Uwezo tayari unao, ni matumizi sahihi tu kwa upande wako ndiyo yanahitajika ili uweze kuzalisha matokeo bora na makubwa zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kwa chochote ambacho umeshaweza kufanya mpaka sasa, unaweza kufanya kwa ukubwa zaidi ya ulivyozoea.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nyuki hatumii muda wake kumshawishi inzi aachane na kazi yake
Twende kinyume na mazoea ili tuzalishe matokeo
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante Kocha,
Moja ya matumizi mabaya sana ya akili na miili yetu ni kufuatilia mambo ya wengine, umbea na mambo mengine kama hayo.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Chochote ninachofanya nitajiuliza je ninakuwa nzi au nyuki?
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mimi nitakuwa nyuki na sitahangaika na kumshawishi inzi awe nyuki.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Tunaweza kufanya makubwa zaidi kama tutaweza kutumia uwezo wetu mkubwa tuwe kama nyuki na si kama inzi
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitahakikisha natumia vizuri matiria niliyonayo ili kujiletea maendeleo.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Amua sasa kama unakuwa inzi au unakuwa nyuki.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kutotumia uwezo mkubwa ulio ndani yangu na kufanya mambo matano bila kuacha ni kujidharau mimi mwenyewe.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Kila mmoja wetu ana uwezo mkubwa sana ndani yake lakini hatutumii vizuri uwezo huu na kutokutumia uwezo huu ndiyo kuchezea matirio
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante kocha,kweli kila mtu amezaliwa na nguvu kubwa ya kufanya makubwa zaidi hivyo inatakiwa tuwe kama nyuki na sio inzi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
unaweza kufanya kwa ukubwa zaidi ya ulivyowahi kufanya.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mtapambana zaidi kutochezea material niliyokuwa nayo
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nakuwa nyuki
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana kocha,tunajifunza ili tuchukue hatua sahihi, nitaendelea kutumia klla rasilimali niliyonayo vizuri ili kufikia ndoto zangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
ASANTE KWA MAKALA HII NZURI
INZI NA NYUKI WOTE WANASIKU INAYOFANANA LAKINI NYUKI ANAJITAMBUA NINI ANAFANYA
HUKU INZI AKIENDELEA KUZURULA BILA MAKAZI MAALUMU
LikeLike
Kabisa
LikeLike