3142; Sikosi hela ya kula.
Rafiki yangu mpendwa,
Matokeo yoyote ambayo mtu unayapata yanalingana na fikra ambazo mtu unakuwa nazo.
Unachopata ni sawa sawa kabisa na picha uliyonayo kwenye fikra zako.
Kwa mfano kama kwenye fikra zako unajisifu kwamba kwenye shughuli zako hukosi hela ya kula, hicho ndiyo utakachoishia kupata, hela ya kula.
Hata upambane kiasi gani, bado utaishia tu kupata hela ya kula.
Siyo kwa sababu huna uwezo wa kupata zaidi, bali kwa sababu hicho ndiyo unachoridhika nacho.
Kwenye maisha huwa hatupati kile tunachostahili kupata, bali tunapata kile tunachokubali na kuvumilia kupata.
Hivyo kama ukipata hela ya kula unakubali na kuridhika, hakuna namna utapata zaidi ya hapo.
Na hata ikitokea kwa bahati umepata zaidi ya hiyo hela ya kula, utaishia hata kuumwa, ili tu usiendelee kutafuta zaidi ya hapo.
Hivyo basi rafiki, kabla ya kuhangaika na matokeo unayopata, anza na fikra ulizonazo juu ya matokeo hayo.
Ni kitu gani huwezi kukubali au kuvumilia? Hicho ndiyo utakachoishia kupata.
Huwa natoa mfano huu wa maeneo ya mjini. Huwa ni nadra sana kusikia mtu amekufa kwa njaa mjini, lakini ni kawaida kuona watu wakiwa wamelala nje, yaani hawana pa kulala.
Watu hao ambao hawana pa kulala, huwa wanahakikisha wanapata chakula, kwa namna yoyote ile.
Lakini wakishapata chakula, wanaridhika, hata kulala nje hakuwaumizi sana.
Kiwango ambacho watu wanakulipa na hata heshima ambayo watu wanakupa, huwa vinaanzia kwenye kile unachokubali kupokea.
Utapata kile tu ambacho umekubali kupokea, unaweza kuvumilia na siyo zaidi ya hapo.
Hata aina ya watu unaowapata kwenye maisha yako, ni wale unaoweza kuwavumilia.
Unaweza kuwa na ndoto na malengo makubwa sana kwenye maisha yako, lakini kama utakubali kupokea chochote chini ya hapo, hicho ndiyo utaishia kukipata.
Kama kupata hela ya kula kunakuridhisha, kimuujiza utakuwa unaishia kupata hela ya kula tu na siyo zaidi ya hapo.
Chochote kile unachotaka kupata, kataa kata kata kupokea na kuvumilia kilicho chini yake.
Utaona wengine wakipata na kufurahia kiwango hicho, lakini wewe hupaswi kufanya hivyo.
Tena wengi watakuambia uridhike kwa sababu unapata vizuri, hupaswi kukubaliana nao.
Ng’ang’ana kupata kile unachotaka na siyo chini ya hapo na hivyo ndivyo utakavyoweza kupata matokeo makubwa zaidi.
Hilo linakwenda hata kwa juhudi unazoweka, kama unaridhishwa na juhudi za kawaida, hizo ndiyo utajikuta unaziweka muda wote.
Ukishaweka juhudi hizo za kawaida, utachoka kabisa na kuona umefanya makubwa sana.
Lakini pale unapokataa kuridhika na juhudi za kawaida, unapata nguvu na hamasa ya kuendelea kuweka juhudi kubwa zaidi.
Maisha ni maigizo, tunachopata ni matokeo ya uhusika tuliochagua kuuvaa.
Kama unataka kupata matokeo ya tofauti na unayoyapata sasa, anza kwa kuvaa uhusika wa tofauti na unaouvaa sasa.
Kuwa na fikra mpya kabisa,
Jione wa tofauti kabisa,
Na kataa kata kata kupokea chochote chini ya kile unachotaka.
Utaanza kwa kupata chini ya kile unachotaka, lakini kwa sababu hutaridhika na hilo, utaendelea kujisukuma zaidi na kupata kile unachotaka.
Adui mkubwa kwenye kupata makubwa ni kuridhika na kujivunia kwa madogo.
Ukishajiona uko na shauku ya kujisifia kwa matokeo madogo unayoyapata, jua hutapata zaidi ya hayo.
Kama huoni aibu na kukasirishwa na matokeo unayoyapata, hutaweza kupata zaidi ya hapo.
Wengi wanataka sana kupata matokeo makubwa, lakini fikra zao zinawasaliti. Ile picha wanayokuwa nayo kwenye fikra zao ndiyo wanayoishia kuipata.
Anza na fikra zako na picha unayokuwa nayo na kataa kata kata kukubali chochote chini ya hapo.
Kama unaridhika kupata hela ya kula, kwa uhakika hutakufa njaa. Lakini pia kwa uhakika hutapata zaidi ya hiyo hela ya kula. Siyo kwa sababu Mungu au asili inakupenda sana usife njaa, bali kwa sababu wewe ndiye umepokea na kuvumilia hayo. Chochote ambacho hutaki, usikubali kukivumilia kwa namna yoyote ile.
Hii dunia ina utele wa kila kitu.
Kuna fursa za kila mtu kuweza kupata kile anachotaka.
Lakini hilo linaanzia ndani ya mtu kwanza kabla ya kile ambacho dunia inampa.
Kama unataka dunia ikupe zaidi, kataa kupokea chochote ambacho ni chini ya unachotaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
ahsante kocha.
nitakuwa na fikra chanya na kukataa madogo hili kupata makubwa ninayohitaji.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kama unataka dunia ikupe zaidi kataa kupokea chini ya unachotaka.
LikeLike
Kataa kata kata.
LikeLike
Adui mkubwa kwenye kupata makubwa ni kuridhika na kujivunia kwa madogo.
Ukishajiona uko na shauku ya kujisifia kwa matokeo madogo unayoyapata, jua hutapata zaidi ya hayo.
Kama huoni aibu na kukasirishwa na matokeo unayoyapata, hutaweza kupata zaidi ya hapo.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Hakika
LikeLike
Tukatae kupokea chini ya tunachotaka na pia tukatae kuridhika na hela ya kula kila siku tuone tunapaswa kupanua akili zetu
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Sitavumilia chochote ambacho sikitaki,hii dunia ina utele wa kila kitu kuna fursa kubwa ya kila mtu kupata na kufikia kile anachokitaka,nairuhusu akili yangu kuamini kwenye kufanya na kufikia makubwa na nitafanya kazi kwa juhudi kubwa bila kuruhisu sababu yoyote inikwamishe ili asili iweze kuniletea fursa kunwa ninazozitaka na niweze kufikia ndoto kubwa nilizo nazo kwenye maisha yangu.
Asante kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha,Nitafanya kwa bidii zaidi na kukataa kata kupokea chochote ambacho kipo chini ya malengo yangu na kukikubali.hivyo lazima nijisukume ili nipate matokeo zaidi ya lengo.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kamwe sitaridhika na juhudi ndogo ndogo na za kawaida ili nipate hamasa ya kuweka juhudi kubwa ili kufanya makubwa.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Sitafikiri tena kwa uchache, nitapambana sana kuhakikisha nalifikia lengo sio tu kuishia kupata hela ya kula na kunywa
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Sitakubali kupokea chini ya kiwango nilichojiwekea. Asante sana kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kama unataka dunia ikupe zaidi Kataa kupokea kile ambacho kipo chini ya kiwango. Kama akili yako inaishia kufikiria kupata hela ya kula basi hapo ndio mwisho wako, huwezi kupata zaidi ya hapo .
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Unapata kile unachovumilia
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Dunia ina utele wa kila kitu,
Kujisifia hela ya kula ni kujifungia fursa za kupata pesa nyingi
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante sana Kocha. Nakataa chochote ambacho ni chini ya viwango nilivyojiwekea. Kwa Sasa KAZI iliyopo mbele yangu ni kuufikia lakionea.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitakataa kupokea chochote kilicho chini ya kile ninachokitaka
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Sitoridhika na kile ninacho vumilia …..
Nitabadili fijra zangu kutokuruhusu kuishi ili nipate pesa ya kula hii inaua ndoto za wengi sana.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kwenye maisha tunapata kile tunachokubali na kuvumilia kikipata.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nifikiri kwa ukubwa na kukataa chochote chini ya hapo. Asante sana Kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni ukweli mchungu.
Kwenye Maisha huwa hatupati kile tunachostahili kupata. Bali tunapata kile tunachokivumilia.
Suruhisho .
Ni kubadili fikla na mtazamo hapo tutabadili matokeo
Asante kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitaendelea kupambana kubadili huu mtazamo kuwa tunapata kile tunachovumilia siyo tunachostahili, binafsi nahitaji kupata kile ninachostahili kupata.
LikeLike
Kipambanie.
LikeLike
Ni kweli kabisa ukikubali jambo dogo unaendelea kupata madogo.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Adui mkubwa kwenye kupata makubwa ni kuridhika na kujivunia kwa madogo.
Ukishajiona uko na shauku ya kujisifia kwa matokeo madogo unayoyapata, jua hutapata zaidi ya hayo.
Kama huoni aibu na kukasirishwa na matokeo unayoyapata, hutaweza kupata zaidi ya hapo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Maisha ni maigizo
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Anza na fikra zako na picha unayokuwa nayo na kataa kata kata kukubali chochote chini ya hapo.
Asante Kocha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Bado sijalidhikana na chochote nilichonacho Sasa napambana kuhakikisha nafikia levo ya juu zaidi
LikeLike
Vizuri, fanya hivyo.
LikeLike
Nitajitahidi kutokurudhika na kukataa kupokea ninachopata Bali kufanya kazi Kwa bidii ili nipokee ninachotaka,hapo lazima malengo na mahitaji yangu yawe makubwa ili nijivute kuongeza kipato ili kuyatimiza. Asante Sana kocha
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nabadili fikra na viwango nilivyo kupangua kwasababu ni mda mrefu nipo pale pale
Naweka viwango vipya kwa kuzidisha mara kumi zaidi
LikeLike
Pambana
LikeLike
Naikataa kupokea chochote chini ya kiwango
LikeLike
Safi sana.
LikeLike