3200; Kushindwa ni kuacha.
Rafiki yangu mpendwa,
Karibu kila mtu kwenye maisha anataka kupata mafanikio makubwa.
Lakini kwenye uhalisia ni wachache sana ambao wamefanikiwa.
Wengi sana wameshindwa.
Na unapoangalia kwa karibu wale walioshindwa,
Unagundua siyo kwa sababu ya kukosea au kukutana na ugumu.
Bali ni kwa sababu waliacha kufanya.
Iko hivi, wanaofanikiwa na wanaoshindwa wote huanza na malengo ya aina moja.
Na kuanza kuchukua hatua ili kufikia malengo hayo.
Halafu wanakutana na ugumu.
Hapo ndipo wanapoachana.
Wanaoshindwa huwa wanaacha kufanya pale wanapokutana na ugumu.
Wanaenda kwenye vitu vingine wanavyoona ni rahisi zaidi.
Lakini huko pia wanakutana na ugumu.
Na hilo ndiyo linapelekea wawe wanaanza mambo mengi na kuishia njiani.
Wanaofanikiwa wanaendelea kufanya licha ya kukutana na magumu.
Wanajua magumu yapo kila mahali na hivyo hawajaribu kuyakimbia.
Badala yake wanayakabili na kuyavuka.
Wakikosea wanarekebisha makosa yao na kuendelea.
Hakuna hata wakati mmoja wanakuwa na fikra za kuacha kufanya kile walichopanga kufanya.
Safari nzima ya mafanikio ni mwendelezo wa fursa na mrejesho.
Pale mtu anapopata matokeo aliyokuwa anayataka yanafungua fursa kwake kufanya kwa ukubwa zaidi.
Na pale mtu anapopata matokeo ya tofauti na aliyokuwa anayataka unakuwa ni mrejesho kwake kwamba kuna kitu hafanyi kwa usahihi.
Hivyo anarudi kujitathmini kwenye kila anachofanya na kuona wapi anahitaji kufanya kwa ukubwa zaidi, ubora zaidi au hata kufanya kwa upya kabisa.
Wanaofanikiwa wanaujua vizuri mwendelezo huo wa fursa na mrejesho na wanaenda na kila wanachopata.
Wanajua chochote wanachopata siyo mwisho, bali ni sehemu ya safari.
Na hilo linawawezesha kupiga hatua kubwa zaidi.
Wanaoshindwa kila kitu kwao ni mwisho.
Wakipata wanachotaka wanajiona tayari wamemaliza.
Hawajisumbui tena kama awali na hilo huwa linapelekea wapate anguko hata baada ya kuwa wamepiga hatua fulani.
Na wakikosa wanachotaka wanajiona hawawezi kukipata kamwe, hivyo wanakata tamaa na kuacha.
Kama unataka kujihakikishia mafanikio kwenye jambo lolote lile, chagua kufanya kwa mwendelezo na msimamo bila kuacha.
Unachopaswa ni kupokea kila matokeo kama fursa na mrejesho.
Matokeo mazuri ni fursa ya kufanya kwa ukubwa zaidi
Na matokeo mabaya ni mrejesho wa wapi unahitaji kurekebisha kwenye ufanyaji wako.
Marekebisho huwa ni ya aina tatu.
Kwanza ni kufanya kwa wingi na ukubwa. Hapa unaongeza kiwango cha ufanyaji. Na hilo pekee linatatua mengi yanayokuwa yanamkwamisha mtu.
Mkwamo mkubwa ambao watu wanakutana nao ni kwa sababu wanafanya kwa kiwango kidogo kuliko inavyohitajika.
Baada ya kufanya kwa ukubwa wote unaowezekana na bado matokeo yasiwe mazuri, unaenda kwenye hatua ya pili ambayo ni ubora.
Hapa unaboresha zaidi kila unachofanya.
Unafanya kwa namna ambayo ni bora ukilinganisha na ulivyokuwa unafanya awali.
Hilo linakuwa na nguvu ya kuleta matokeo ya tofauti.
Na kama maboresho wamefanyika mpaka mwisho ila matokeo bado siyo mazuri, ndiyo hatua ya tatu inaweza kufanyiwa kazi.
Hatua hiyo ni kufanya kitu kipya.
Hapa unaanza kitu kingine kipya kwenye safari hiyo hiyo uliyochagua.
Kwa bahati mbaya sana, watu huwa wanakimbilia kufanya vitu vipya kabla hata hawajafanya kwa ukubwa na ubora.
Na hilo linawapelekea kuanza vitu vingi vipya lakini hawafiki navyo mbali.
Wewe umeshajifunza haya na hivyo unakuwa tofauti kabisa na walio wengi.
Hutashindwa kamwe kwa sababu hutaacha kufanya kwa namna yoyote ile.
Utatumia kila fursa na kila mrejesho kufanya kwa ukubwa, ubora na upya kwa maisha yako yote.
Hayo ndiyo maisha ya ushindi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hakika, kushindwa ni kuacha. Asante sana Kocha Dr.Makirita Amani.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kushindwa ni kuacha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ahsante sana kocha, Matokeo mazuri ni fursa ya kufanya kwa ukubwa zaidi
Na matokeo mabaya ni mrejesho wa wapi unahitaji kurekebisha kwenye ufanyaji wako.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante kocha kumbe Kushindwa nikuacha inamaana ushindi nikufanya Kwa muendelezo bila kuacha okay nimeelewa vizuri
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Utatumia kila fursa na kila mrejesho kufanya kwa ukubwa, ubora na kwa maisha yako yote
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Katika maisha hakuna atakayeshindwa kama hajaacha kufanya. Nitajitahidi kufanya kwa wingi na ubora hadi nione matokeo. Asante sana kocha
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Sawa kabisa
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante Kocha,
Niliyopanga kufanya nitaendelea kufanya hata pale nina pokutana na ugumu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kwa walifanikiwa wamefanya kwa msimamo na wakaingia kwenye kuboresha
Kwa ukubwa na kuuza kwa wingi na baadae kuendelea tena kubaresha kwa kufanya kwa ubora na kama haijaleta matokeo wanaaangalia upande mwingine na kuanza mchakato upya na kukua nao hadi kupata ushindi
LikeLike
Hiyo ndiyo kanuni.
LikeLike
Ili ufanikiwe usiache kufanya na fanya Kwa ukubwa, ubora na kama vyote hivyo vitashindwa fanya kitu kipya.
Hakuna kuacha mpaka kieleweke
Asante sana
LikeLike
Hakika, tusiache.
LikeLike
“Utatumia kila fursa na kila mrejesho kufanya kwa ukubwa, ubora na upya kwa maisha yako yote.
Hayo ndiyo maisha ya ushindi.”
Hakika hii ni nguvu ya kufanya kwa Msimamo na ushindi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante sana kocha.Kwenye kushindwa niondoke ma somo na kuendelea kuboresha si kukimbia
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Sitaacha kufanya!
Kushindwa ni kuacha.
LikeLike
Hakuna kuacha.
LikeLike
Kushindwa ni pale ninapoamua kuacha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hakika sitaacha nitaendelea na mapambano Hadi kieleweke
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Katika safari ya kutafuta mafanikio makubwa, walioshindwa sio wale waliokosea au kukutana na magumu bali ni wale walioamua kuacha. Mimi nitapambana na sitaacha pale nitakapokosea au kukutana na magumu na kuendeleza mchakato siku zote.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike