3237; Mchezo unaocheza.
Rafiki yangu mpendwa,
Maisha ni mchezo mmoja mkubwa sana ambao ndani yake kila mtu anacheza mchezo wa aina yake.
Na hiyo ndiyo sababu kila mtu anapata matokeo ya tofauti na ya wengine, kwa sababu michezo haifanani.
Japokuwa mchezo ni ule ule, namna ya uchezaji inatofautiana baina ya watu.
Na hivyo pia ukubwa wa mafanikio unatofautiana sana.
Kuna ngazi tatu za huu mchezo wa maisha ambazo zinatofautishwa na namna ya uchezaji na matokeo yanayopatikana.
Ngazi ya chini kabisa ni ya wale wanaocheza kwa ugeni.
Hawa wanacheza ili kutokupoteza.
Namna yao ya uchezaji ni ya kulinda ili wasipoteze.
Kwa sababu wanalenga zaidi kutokupoteza, hawapati ushindi.
Na hilo hawalijali sana, wanachoangalia ni kwamba hawajapoteza au kushindwa.
Kutokushindwa siyo sawa na kushinda.
Watu hawa huwa hawapati mafanikio, licha ya juhudi kubwa wanazoweka kwenye kile wanachofanya.
Kwa sababu wanaridhika na kutokupoteza.
Ngazi ya kati ni ya wale wanaocheza kwa mazoea.
Hawa wanacheza ili kupata ushindi.
Namna yao ya uchezaji ni kushambulia ili wapate ushindi.
Kwa sababu wanalenga zaidi kupata ushindi, huwa wanaupata.
Na hapo ndipo penye mtego mkubwa sana, kwani wanaridhika na ushindi waliopata na kubweteka.
Kwa kuwa wameshapata ushindi, wanaacha kuweka zile juhudi ambazo ziliwafikisha kwenye ushindi huo.
Na hilo linawapelekea kupoteza ushindi ambao wameupata na kujikuta wanarudi tena chini.
Watu wa ngazi hii huwa wanapata ushindi na kupoteza mara kwa mara.
Na pale wanapochoka, wanabaki kwenye kushindwa.
Ngazi ya juu ni ya wale ambao ni wabobezi.
Hawa wanacheza kwa sababu wanapenda kucheza.
Namna yao ya uchezaji ni ili waendelee kucheza, wanaendelea kubaki kwenye mchezo kwa kipindi chote cha maisha yao.
Kwa sababu hawaachi kucheza, ushindi unakuwa endelevu kwao, kwa sababu ushindi mkuu ni kwa wanaodumu kwa muda mrefu zaidi.
Watu wa ngazi hii huwa hawahofii chochote, kwa sababu mapenzi yao kwenye mchezo ni makubwa kuliko kingine chochote.
Siyo watu wa kuruka ruka na vitu vipya kila wakati, bali wanatulia kwenye kile walichochagua kwa muda mrefu na hilo kuwapa mafanikio makubwa na endelevu.
Rafiki yangu mpendwa, wewe upo kwenye ngazi ipi ya mchezo?
Shirikisha kwenye maoni hapo chini na ushahidi wa ngazi unayosema upo.
Kama kweli unayataka mafanikio makubwa na ya kudumu, basi hakikisha unaupenda sana mchezo kiasi cha kuwa tayari kuucheza kwa maisha yako yote.
Kama huna mapenzi ya aina hiyo kwenye mchezo wako wa maisha, ni bora kuachana nao na kwenda kwenye kitu kingine.
Kwa sababu mafanikio ni magumu sana kwa kitu ambacho hujajitoa kukifanya kwa viwango vya juu kwa muda mrefu zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hakika huu mchezo nitaucheza kwa maisha yangu yote.
LikeLike
Safi sana.
Huo tayari ni ushindi.
LikeLike
Ubobezi na kufanya kwa maisha yng yote mchezo niliochagua kucheza
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mimi Nipo kwenye ngazi ya ubobezi ninaupenda mchezo na ninafanya Kwa msimamo ili kuleta matokeo yamayohitajika
Asante sana
LikeLike
Mimi nipo ngazi ya juu(Wabobezi)
Kwasababu mimi sio mtu wa kuruja ruka na kufanya vitu vipya kila wakati. Kwa kuwa ushindi mkuu ni kwa wanaodumu kwa muda mrefu kwenye kitu kimojs
LikeLike
Safi sana, hakika huo ndiyo ushindi mkuu.
LikeLike
Safi sana na kila la kheri.
LikeLike
Nitaendelea kufanya biashara na kujifunza katika kipindi chote cha maisha ya uhai hapa duniani..na kamwe sitaacha kujiendeleza katika msingi mkuu ambao ni Ubobezi katika lugha ya KICHINA(普通话),kwa haya bila Shaka Niko Ngazi No 3-Ubobezi
“Kama kweli unayataka mafanikio makubwa na ya kudumu, basi hakikisha unaupenda sana mchezo kiasi cha kuwa tayari kuucheza kwa maisha yako yote.”
LikeLike
Safi sana na kila la kheri.
LikeLike
Mimi niko ngazi ya tatu kwenye uwekezaji wa kilimo huu utaniua,siachi.
LikeLike
Safi sana.
Huo pekee ni ushindi.
LikeLike
Asante Kocha,
Ngazi ya juu (ubobezi). Nilichochagua kufanya ninafurahia. Haijalishi matokeo, yakiwa nisiyotegemea bado nina kazi nayo; na kazi yenyewe ni maboresho.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Hii kauli nimeipenda sana, nakwenda kuifanyia KAZI mara moja”Haijalishi matokeo, yakiwa nisiyotegemea bado nina kazi nayo; na kazi yenyewe ni maboresho.”
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nipo kwenye ngazi ya ubobezi ambapo mchezo ni maisha yenyewe.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Nipo kwenye ngazi ya tatu ya mchezo wa ubobezi, maana tayari najua nini natakiwa nifanye na kwa namna gani
LikeLike
Safi, kaa humo.
LikeLike
Nami nimeamua kukaa kwenye ubobezi.Nitaendelea kubobea kwenye biashara na uwekezaji kwa kufanya kwa maisha yangu yote.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Niko ngazi ya juu nitacheza mchezo kwa maisha yangu yote.
LikeLike
Vizuri na kila la kheri.
LikeLike