3286; Kushangazwa na dunia.
Rafiki yangu mpendwa,
Kanuni rahisi ya furaha inahusisha matarajio na uhalisia.
Pale matarajio yanapokuwa makubwa kuliko uhalisia, mtu unakosa furaha.
Na pale matarajio yanapokuwa madogo kuliko uhalisia, mtu unapata furaha.
Inapokuja kwenye matarajio na uhalisia, dunia huwa inatushangaza.
Tunapokuza sana kimoja, kingine huwa kidogo mpaka kutushangaza.
Hivyo dunia inaweza kutushangaza kwa uchanya, pale uhalisia unapokuwa mkubwa kuliko matarajio.
Au ikatushangaza kwa uhasi, pale uhalisia unapokuwa mdogo kuliko matarajio.
Itakuwa ni vyema kama dunia itatushangaza kwa uchanya.
Hivyo tunachopaswa kufanya ni kuweka matarajio yetu chini sana, huku tukiweka juhudi zetu juu sana.
Hapo matokeo yoyote yatakayokuja, lazima yatatushangaza kwa uchanya.
Hivyo sivyo wengi wanavyofanya.
Kwa sababu watu wanapenda kujipa matumaini hewa.
Ni matumaini hewa kwa sababu juhudi wanazoweka zinakuwa haziendani kabisa na matarajio wanayokuwa nayo.
Matumaini yanakuwa sahihi pale juhudi zinapozidi matarajio yanayokuwepo.
Na kwa kuwa dunia lazima itakushangaza, anza wewe kwa kuishangaza dunia.
Ishangaze dunia kwa juhudi kubwa sana unazoweka ambazo ni zaidi ya matarajio unayokuwa nayo.
Weka juhudi ambazo hakuna mwingine anayeweka kwa kiasi hicho.
Japokuwa dunia itakupa matokeo ya tofauti na matarajio, hilo lisikushangaze kwa namna yoyote ile.
Kubali kila matokeo yanayokuja na yatumie ili kufanya kwa ubora zaidi.
Kumbuka huidai dunia chochote,
Ulikuja ukaiacha na utaondoka ukaiacha.
Wajibu wako ni kujua kile unachotaka, kuweka juhudi kubwa kwenye kukipata na kupokea kila aina ya matokeo yatakayopatikana.
Tumia matokeo hayo kuboresha zaidi ili kusogea karibu zaidi na kile unachotaka.
Waache wengine washangazwe na dunia, wewe nenda nayo kwa namna sahihi kwako ili kupata kile unachotaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni ukweli kabisa siidai chochote dunia.Wajibu wangu ni kujua nini ninachotaka,kuweka juhudu kukipata na kupokea kila aina ya matokeo yatakayopatikana.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Muhimu niende na Dunia kwa namna sahihi kwangu ili kupata kile ninachotaka tu. ✍️
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Juhudi zetu zinapaswa kuwa juu huku matarajio yetu yakiwa chini.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Nenda na Dunia inavyotaka na sio unavyotaka wewe
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
tunashukuru kocha kwa ujumbe huu mzuri
LikeLike
Karibu Macha
LikeLike
Juhudi zinapaswa kuwa kubwa kuliko matarajio kuishangaza dunia.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Naweka juhudi kubwa zaidi ya matarajio niliyonayo
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kabisa kuweka matarajio juu Sana basi matokeo yatatushangaza na kupelekea kujilaumu na kujutia. Wela matarajio chini ili kuitunza Imani ya nafsi na Amani ya moyo. Dunia haidaiwi chochote inaenda kadri ya asili inavyotaka
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kumbuka huidai dunia chochote,
Ulikuja ukaiacha na utaondoka ukaiacha.
Wajibu wako ni kujua kile unachotaka, kuweka juhudi kubwa kwenye kukipata na kupokea kila aina ya matokeo yatakayopatikana.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha kwa ujumbe mzuri kitu cha msingi kabisa ni kujua hasa nini ninachotaka na kuweka juhudi ili kukipata nakupokea kila aina ya matokeo yatakayopatikana
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Swala la muhimu hapa ni kuweka matarajio kiasi na kudanya kwa ukubwa yaani kwa bidii sana na pale unapopata matokeo boresha boresha kwa wingi na kwa ukubwa na kuendelea na juhudi kwa msimamo bila kuacha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Sawa juhudi kubwa matarajio kidogo
Shukurani kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike