3289; Kusubiri kuanza.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama kuna kitu ambacho unataka kukifanya, lakini kwenye kuanza unasubiri kwanza, hujakitaka kweli kitu hicho.
Kadiri unavyosubiri kwa muda mrefu kuanza kufanya kitu, ndivyo inavyokuwa vigumu kuanza kukifanya na hata kupata mafanikio. Hiyo ni kwa sababu kusubiri kunapooza kitu na kuondoa ule msukumo na uharaka wa kuchukua hatua.
Kitu ambacho wengi huwa wanasingizia kwenye kusubiri kwa muda mrefu ni kufanya maandalizi ya kutosha.
Lakini hilo ni kujidanganya tu, huhitaji maandalizi makubwa sana ndiyo uanze kufanya kitu.
Unatakiwa kuanza kwanza, halafu mengine yafuate.
Ukianza kabla hata ya kukamilisha maandalizi, utajua ni maandalizi gani ya muhimu zaidi.
Kuamini kwamba siku fulani zijazo utakuwa tayari zaidi kuanza kuliko sasa ni kujidanganya tu.
Wakati ambao upo tayari zaidi kuanza kufanya kitu ni pale unapokuwa umepata wazo la kukifanya.
Hapo ndipo unakuwa na shauku kubwa ya kufanya, ambayo kadiri muda unavyokwenda inakuwa inapungua.
Muda unavyokwenda, kitu kinapoa na ule msukumo wa kukianza unapungua na kuondoka kabisa.
Mwishowe unajikuta ukiwa na sababu nyingi za kutokufanya kuliko sababu za kufanya.
Kuwa mtu wa kuanza kufanya mara moja yale unayokuwa unayataka.
Usiwe mtu wa kusubiri mpaka ufanye maandalizi fulani, anza na maandalizi mengine yataendelea.
Maandalizi unayokuwa unayafanya wakati unaendelea kufanya huwa yanakuwa sahihi kuliko yale unayofanya ukiwa unasubiri.
Kama kweli kuna kitu unachokitaka sana, basi unapaswa kukipambania kwa ukubwa sana.
Unapaswa kuanza kukifanyia kazi mara moja na kwenda ukiboresha kulingana na matokeo unayoyataka.
Kusubiri ni kiashiria kwamba hukitaki kitu hasa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Tabia ya kuahirisha mambo ndiyo imekuwa kaburi kubwa la kua ndoto za mafanikio makubwa kwenye maisha yetu
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante kocha,nitaanza mara moja bila kusubiri.Kusubiri ni kiashiria kwamba hukitaki kitu hasa na chochote nachokitaka nitaanza mara moja bila kusubiri.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha kwa ujumbe mzuri kusubiri ni kiashiria kwamba hutaki kile kitu
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kusubiri kuanza jambo lolote ni kutokuwa tayari na kitu hicho. Nitajitahidi kufanya kila jambo kwa wakati wake bila kusubiri.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kama kweli kuna kitu unachokitaka sana, basi unapaswa kukipambania kwa ukubwa sana.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Anza mara Moja kufanya kitu, kusubili ni kujidanganya
Asante
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kuendelea kufanya wakati unaendelea na maandalizi zaidi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Muda sahihi wa kuanza ni pale unapokuwa na wazo fulani
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kusubiri kunapooza kitu na kuondoa ule msukumo na uharaka wa kuchukuwa hatua
LikeLike
Ndiyo
LikeLike