3292; Kuvutiwa na maneno.
Rafiki yangu mpendwa,
Maneno huwa ni rahisi sana kuyatoa,
Na matendo huwa ni magumu sana kuonyesha.
Watu ni rahisi kukupa maneno mazuri na yanayoshawishi.
Lakini inapokuja kwenye matendo, wengi huwa siyo watekelezaji wazuri wa yale wanayoongea.
Hivyo basi, unapaswa kuwa makini sana na maneno ya watu.
Usiyape maneno uzito mkubwa kama hayajaambatana na matendo yanayodhihirisha maneno hayo.
Usiwe rahisi kuvutiwa na maneno pekee, hata kama anayeyatoa anakuwa na ushawishi kiasi gani.
Sikiliza, lakini subiri uone matendo kabla hujavutiwa na maneno peke yake.
Kwa bahati mbaya sana, wale wanaojieleza sana, ambao pia ndiyo wanaoshawishi, huwa siyo watendaji wazuri.
Kuvutiwa na maneno ya watu wa aina hiyo na kuweka matumaini makubwa kwao ni kujiandaa kuangushwa na kukatishwa tamaa.
Umeshasikia maneno mengi sana mpaka sasa, lakini matendo ni machache.
Weka thamani kubwa kwenye matendo kuliko maneno ili usiangushwe na matumaini hewa.
Kwa upande wa pili, yaani kwako mwenyewe, usiwe mtu wa maneno mengi.
Bali kuwa mtu wa matendo zaidi.
Fanya kile unachokuwa umesema utafanya.
Hiyo ndiyo njia rahisi ya kuaminika na hata kupata mengi unayotaka.
Fanya kile kilicho sahihi na kinachopaswa kufanywa.
Na ukimaliza nenda kwenye kingine kinachopaswa kufanywa.
Usipoteze muda kwenye maelezo mengi, wanaokuelewa hawayahitaji hayo maelezo na wanaoyahitaji bado hawatakuelewa hata uwaelezeje.
Matendo yana nguvu kubwa kuliko maneno.
Weka thamani kubwa kwenye matendo na utapunguza usumbufu mwingi na matumaini hewa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Matendo dhidi ya maneno
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Matendo yana nguvu kubwa zaidi kuliko maneno.Nitaweka matendo zaidi na sio maneno.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Fanya kile kilicho sahihi na kinachopaswa kufanywa.
Na ukimaliza nenda kwenye kingine kinachopaswa kufanywa.
Usipoteze muda kwenye maelezo mengi, wanaokuelewa hawayahitaji hayo maelezo na wanaoyahitaji bado hawatakuelewa hata uwaelezeje.
Ahsante sana Kocha.
Nimekuelewa vizuri.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Matendo yana nguvu kubwa kuliko maneno.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Matendo yana nguvu kubwa kuliko maneno.
Weka thamani kubwa kwenye matendo na utapunguza usumbufu mwingi na matumaini hewa.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Acha maneno weka kazi
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Wengi wanaweza kukupa maneno, wachache sana watakupa vitendo. Mimi nikiwa wa vitendo zaidi, nitajitofuatisha nao.
Asante Kocha.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Umesikia maneni mengi Sana mpk Sas,
Lakini matendo ni machache.
🙏🙏🙏
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Matendo yana nguvu kubwa kuliko maneno
Muhimu ni kuweka nguvu kwenye matendo.
Asante sana kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ni muhimu kutenda zaidi kuliko kiongea sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kazi kweli kweli.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ndiyo maana nauamini mchakato wa Bolionea Mafunzini na nakaa humo. Naweka kazi na sitaki maneno Wala ahadi zingine
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike