Huwa kuna kauli kwamba kama kufanya kazi kwa juhudi ingekuwa ndiyo ufunguo wa mafanikio, basi punda wangekuwa wamefanikiwa kuliko wanyama wote.
Inaweza kuonekana ni kauli yenye ukweli, hasa ukizingatia hata kwa binadamu, watu wanaofanya kazi kwa juhudi kubwa sana ndiyo pia hawana mafanikio makubwa. Ukienda kwenye taasisi yoyote kubwa, unakuta mfanyakazi wa chini anafanya kazi ngumu sana, lakini kipato chake ni kidogo, wakati mkurugenzi mkuu hafanyi kazi ngumu ila kipato chake ni kikubwa.

Hiyo ni kwa sababu juhudi zote hazilingani, siyo kila juhudi inayowekwa inaweza kuchangia mafanikio. Kuna juhudi nyingine siyo tu zinakwamisha mafanikio, bali pia zinakupeleka kwenye njia inayokupoteza kabisa kwenye mafanikio.
Kwa bahati mbaya sana, hivyo ndivyo maisha ya watu wengi yalivyo, wapo kwenye njia ambazo zinawapoteza kabisa kulingana na mafanikio wanayotaka kuyajenga. Ni muhimu sana mtu kujikagua kazi unayotaka kuweka kama ni sahihi kabla hata hujaiweka.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeshirikisha njia ya upotevu ambayo wengi wanapita na inawafanya wakose mafanikio ambayo wanayataka. Karibu ujifunze hapa ili uache kujipoteza wewe mwenyewe na juhudi unazoweka kwenye yale unayochagua ziweze kuwa sahihi na zenye tija.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.