
Kakaa/Dadaa…
Unasema unataka kubadilisha maisha yako.
Unasema unataka pesa.
Unasema unataka mafanikio.
Lakini bado kila siku unaamka bila mpango.
Unavua pajama saa nne asubuhi.
Unadamkia kucheki status za whatsApp.
Halafu mwisho wa siku unaanza kusema: Siku yangu ilikuwa ndefu sana.
Bro, HAPANA!
Mafanikio hayawezi kumngoja mtu asiye na mpango.
Hayawezi kumwangalia mtu anayepoteza siku yake ovyo.
Kila siku unachelewa.
Kila siku unasema Nitafanya kesho.
Kila siku unaweka mipango kichwani bila kuiandika.
Na kila jioni unajilaumu kwa sababu siku imepita bila matokeo.
Inauma, siyo?
Kujua kuwa ungeweza kufanya zaidi… lakini hukufanya.
Kujua kuwa ulikuwa na nafasi… lakini uliichezea.
Wewe mwenyewe unajua kuna kitu kinakosekana.
Na hicho kitu ni KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO.
Siku ya mafanikio haianzi kwa kuamka tu.
Inaanza na KANUNI.
Mpango.
Ratiba.
Uamuzi wa kusimama kama mshindi, kila asubuhi.
Wengi wanajidanganya:
Wacha tu niende na flow ya siku.
Niache maisha yajiendeshe yenyewe.
Hiyo ni NDOTO!
Maisha hayaendeshwi kwa flow, bro.
Maisha huendeshwa kwa kanuni.
KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO ni kama ramani ya kila siku.
Unaiandika kabla ya siku haijaanza.
Inakuambia:
Nani wa kumpigia?
Nini cha kufanya saa nne?
Ni lipi la kuanza, lipi la kuahirisha?
Nini kikikamilika kitakufanya useme: Leo nimefanya kweli!
Hii sio ratiba ya kawaida.
Ni RAMANI ya mafanikio.
Unaiishi. Unaiheshimu. Unaiendea bila kubabaika.
Na ikishika… bro, hakuna wa kukuzuia.
Kuna time niliamka nikiwa nimechoka kimaisha.
Kila kitu kilikuwa kinanichanganya.
Mara sipati wateja, mara nashindwa kuandika vizuri, mara stress.
Nikagundua tatizo: siku zangu hazikuwa na msimamo.
Nilikuwa naamka tu bila direction.
Siku moja nikasema:Leo, natunga kanuni yangu.
Nikaandika mambo 3 tu ya muhimu ya kufanya siku hiyo.
Nikaanza nayo.
Bro, siku ile nilihisi kama nimevaa suti ya Superman.
Nilihisi control.
Nikapiga simu ya mauzo. Nikaandika content.
Nikamaliza kazi kabla ya saa kumi.
Na ikaanza kuwa kawaida.
Sasa hivi?
Kabla siku haijaanza, kanuni iko tayari.
Na kila siku huwa na ladha ya ushindi.
Ndio maana nakuambia:
NDIYO LEO.
Anza leo.
Tunga kanuni ya siku yako ya mafanikio.
Ishi kwa hiyo kanuni kila siku.
Na maisha yako yatabadilika kwa kasi ya ajabu.
Usisahau:
Mafanikio hayaanguki kama mvua.
Yanatengenezwa kila siku kwa kanuni, kwa mpango, kwa uthubutu.
Na yote yanaanza kwa uamuzi mmoja…
NDIYO LEO.
Uko tayari?
Kama upo tayari, kuipata kanuni yako ya siku ya maneno,
Tuma ujumbe NATAKA KANUNI
Kwenda 0756694090.
Karibu.
Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan.