‎Kakaa/Dadaa…
‎
‎Unasema unataka kubadilisha maisha yako.
‎
‎Unasema unataka pesa.
‎
‎Unasema unataka mafanikio.
‎
‎Lakini bado kila siku unaamka bila mpango.
‎
‎Unavua pajama saa nne asubuhi.
‎
‎Unadamkia kucheki status za whatsApp.
‎
‎Halafu mwisho wa siku unaanza kusema: Siku yangu ilikuwa ndefu sana.
‎
‎Bro, HAPANA!
‎
‎Mafanikio hayawezi kumngoja mtu asiye na mpango.
‎
‎Hayawezi kumwangalia mtu anayepoteza siku yake ovyo.
‎
‎Kila siku unachelewa.
‎
‎Kila siku unasema Nitafanya kesho.
‎
‎Kila siku unaweka mipango kichwani bila kuiandika.
‎
‎Na kila jioni unajilaumu kwa sababu siku imepita bila matokeo.
‎
‎Inauma, siyo?
‎
‎Kujua kuwa ungeweza kufanya zaidi… lakini hukufanya.
‎
‎Kujua kuwa ulikuwa na nafasi… lakini uliichezea.
‎
‎Wewe mwenyewe unajua  kuna kitu kinakosekana.
‎
‎Na hicho kitu ni KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO.
‎
‎Siku ya mafanikio haianzi kwa kuamka tu.
‎
‎Inaanza na KANUNI.
‎
‎Mpango.
‎
‎Ratiba.
‎
‎Uamuzi wa kusimama kama mshindi, kila asubuhi.
‎
‎Wengi wanajidanganya:
‎
‎Wacha tu niende na flow ya siku.
‎
‎Niache maisha yajiendeshe yenyewe.
‎
‎Hiyo ni NDOTO!
‎
‎Maisha hayaendeshwi kwa flow, bro.
‎
‎Maisha huendeshwa kwa kanuni.
‎
‎KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO ni kama ramani ya kila siku.
‎
‎Unaiandika kabla ya siku haijaanza.
‎
‎Inakuambia:
‎
‎Nani wa kumpigia?
‎
‎Nini cha kufanya saa nne?
‎
‎Ni lipi la kuanza, lipi la kuahirisha?
‎
‎Nini kikikamilika kitakufanya useme: Leo nimefanya kweli!
‎
‎Hii sio ratiba ya kawaida.
‎
‎Ni RAMANI ya mafanikio.
‎
‎Unaiishi. Unaiheshimu. Unaiendea bila kubabaika.
‎
‎Na ikishika… bro, hakuna wa kukuzuia.
‎
‎Kuna time niliamka nikiwa nimechoka kimaisha.
‎
‎Kila kitu kilikuwa kinanichanganya.
‎
‎Mara sipati wateja, mara nashindwa kuandika vizuri, mara stress.
‎
‎Nikagundua tatizo: siku zangu hazikuwa na msimamo.
‎
‎Nilikuwa naamka tu  bila direction.
‎
‎Siku moja nikasema:Leo, natunga kanuni yangu.
‎
‎Nikaandika mambo 3 tu ya muhimu ya kufanya siku hiyo.
‎
‎Nikaanza nayo.
‎
‎Bro, siku ile nilihisi kama nimevaa suti ya Superman.
‎
‎Nilihisi control.
‎
‎Nikapiga simu ya mauzo. Nikaandika content.
‎
‎Nikamaliza kazi kabla ya saa kumi.
‎
‎Na ikaanza kuwa kawaida.
‎
‎Sasa hivi?
‎
‎Kabla siku haijaanza, kanuni iko tayari.
‎
‎Na kila siku huwa na ladha ya ushindi.
‎
‎Ndio maana nakuambia:
‎
‎NDIYO LEO.
‎
‎Anza leo.
‎
‎Tunga kanuni ya siku yako ya mafanikio.
‎
‎Ishi kwa hiyo kanuni kila siku.
‎
‎Na maisha yako yatabadilika kwa kasi ya ajabu.
‎
‎Usisahau:
‎
‎Mafanikio hayaanguki kama mvua.
‎
‎Yanatengenezwa kila siku kwa kanuni, kwa mpango, kwa uthubutu.
‎
‎Na yote yanaanza kwa uamuzi mmoja…
‎NDIYO LEO.
‎
‎Uko tayari?
‎
‎Kama upo tayari, kuipata kanuni yako ya siku ya maneno,
‎
‎Tuma ujumbe NATAKA KANUNI
‎
‎Kwenda 0756694090.
‎
‎Karibu.
‎Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan.
‎
‎
‎
‎
‎
‎
‎
‎
‎