Hii Ndiyo Falsafa Bora Unayopaswa Kumjengea Mtoto Wako

Mpendwa rafiki yangu, Watoto wengi zama hizi wanapitia changamoto nyingi na wakati mwingine hakuna mtu anayewasikiliza matatizo yao wanayopitia. Huenda wazazi wako bize sana na kazi kiasi cha kusahau watoto wao. Watoto hawapati muda wa kukaa na wazazi wao, wazazi wanatakiwa kutenda muda wa kukaa na watoto wao kuwauliza nini kinaendelea katika maisha yao,wanapitia nini,... Continue Reading →

Tano Za Juma Kutoka Kitabu Can’t Hurt Me; Jinsi Ya Kutawala Akili Yako Ili Chochote Kisikuumize Na Upate Mafanikio Makubwa.

#TANO ZA JUMA #13 2019; Kuumia Ni Kuchagua, Jinsi Ya Kutawala Akili Yako Ili Usiumizwe, Kanuni Ya Asilimia 40 Ya Kujisukuma Zaidi, Usitake Fedha Kabla Hujakomaa Kiakili Na Cha Kubobea Ili Ufanikiwe. Rafiki yangu mpendwa, Karibu kwenye tano za juma la 13 la mwaka huu 2019. Hapa nimekuandalia mambo matano makubwa ya kujifunza na kuchukua... Continue Reading →

Kanuni Ya Asilimia 40; Jinsi Unavyoweza Kuusukuma Mwili Wako Kufanya Makubwa Kuliko Ulivyozoea.

Rafiki yangu mpendwa, Kila mtu anapenda kufanya makubwa na kufanikiwa sana kwenye maisha yake. Lakini wengi wanapojaribu kufanya makubwa, wanakutana na kikwazo kikubwa ambacho kinawazuia wasiweze kufanya makubwa. Kikwazo hicho ni miili yetu. Miili yetu haina tofauti na gari, ndani yetu tuna kidhibiti mwendo (speed governor) ambacho kinatuzuia tusiweze kupiga hatua zaidi. Kama ambavyo gari... Continue Reading →

Mambo Manne (4) Unayopaswa Kuzingatia Ili Kuweza Kuanzisha Blogu Na Kuitumia Kutengeneza Kipato.

Rafiki yangu mpendwa, Kwa zaidi ya miaka sita nimekuwa kwenye tasnia hii ya kuanzisha na kuendesha blogu mbalimbali. Na pia nimekuwa natumia blogu hizo kuingiza kipato. Nimekuwa pia nawashirikisha watu jinsi ya kuanzisha blogu zao na jinsi ya kuzitumia kutengeneza kipato. Niliandika kitabu JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO KWA KUTUMIA BLOG, ambacho kimewasaidia wengi kuanzisha blogu... Continue Reading →

Hii Ndiyo Tahajudi Rahisi Itakayokupa Utulivu Mkubwa Na Kukuwezesha Kupata Chochote Unachotaka Kwenye Maisha Yako.

Rafiki yangu mpendwa, Tahajudi au kama inavyofahamika kwa Kiingereza Meditation ni zoezi la kiakili ambalo linatuwezesha kuwa na udhibiti wa fikra zetu, kitu ambacho kinatuletea utulivu mkubwa na kutuondolea msongo wa mawazo. Kwa asili fikra zetu huwa haziwezi kutulia sehemu moja, unafanya kitu hiki lakini fikra zako zipo kwenye kitu kingine. Kwa hali hii tunakosa... Continue Reading →

Maeneo Kumi Na Mbili (12) Muhimu Sana Kwa Mafanikio Ya Maisha Yako, Malengo Ya Kujiwekea Kila Eneo Na Vitabu Vya Kusoma Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.

Rafiki yangu mpendwa, Maisha yetu ni mjumuiko wa maeneo mbalimbali yanayohusu maisha haya. Hivyo ili kuwa na mafanikio ya kweli kwenye maisha, lazima kuwe na mlinganyo katika mafanikio tunayopata kwenye kila eneo. Watu wengi wanaokazana kufanikiwa wamekuwa hawapati mafanikio ya kweli kwa sababu huweka juhudi kwenye eneo moja au machache ya maisha na kusahau maeneo... Continue Reading →

Jinsi Ya Kubadili Hisia Mbaya Za Wivu Na Chuki Kwenda Hisia Nzuri Za Heshima Na Upendo.

Rafiki yangu mpendwa, Changamoto na matatizo mengi ambayo tunakutana nayo kwenye maisha yetu, chanzo chake kikuu ni hisia ambazo tunazokuwa nazo. Ndiyo maana wanafalsafa wamekuwa wakifundisha sana kuhusu udhibiti wa hisia zetu, kwa sababu tukishaweza kuzidhibiti hisia zetu, hakuna kitakachotushinda kwenye maisha yetu. Watu wengi wamefanya maamuzi makubwa kwenye maisha yao kwa kusukumwa na hisia,... Continue Reading →

Kweli Tatu Chungu Unazopaswa Kuzijua Kuhusu Dunia Ili Uwe Na Maisha Ya Utulivu Na Mafanikio.

Rafiki, Tangu enzi na enzi, binadamu tumekuwa tunafanya kila juhudi kuukimbia ukweli. Kwa sababu ukweli unaumiza na haubembelezi, basi wanadamu tumekuwa hatuupendi. Hivyo tumekuwa tunatafuta kila namna ya kuukwepa au kuuficha ukweli. Na ukiangalia jinsi dunia inavyokwenda, taasisi nyingi ambazo zina wafuasi wengi, hazijajengwa kwenye misingi ya ukweli. Ukianzia kwenye taasisi kama nchi, mashirika makubwa,... Continue Reading →

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑