#TANO ZA JUMA #49 2018; Jinsi Ya Kuvuta Chochote Unachotaka, Hatua 7 Za Kutengeneza Mtazamo Wa Mafanikio, Jinsi Ya Kuvuta Fedha Ije Kwako Na Kinachotokea Sasa Ni Matokeo.

Hongera sana rafiki yangu kwa juma hili la 49 ambalo tumekuwa nalo kwa mwaka huu 2018. Najua ni juma ambalo limekuwa la mafanikio makubwa sana kwako. Kama umekuwa unaiishi misingi ambayo nakushirikisha kila siku kwenye makala mbalimbali, basi juma hili litakuwa limeleta vitu vipya kwako. Tunakwenda kulimaliza juma letu bora, na kujiandaa na juma jingine... Continue Reading →

Hivi Ndivyo Elfu Moja Kila Siku Kwa Siku 20 Inavyoweza Kuyabadili Maisha Yako Na Kukufikisha Kwenye Utajiri.

Rafiki yangu mpendwa, Salamu zangu za mafanikio zikufikie popote pale ulipo sasa, wakati unaendelea na mapambano ya kuyaboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. Kumbuka nipo na wewe kwenye safari hii, kila wakati nikikushirikisha maarifa bora sana kwako ili uweze kufika kule unakotaka. Kwa sababu kama ambavyo nimekuwa nakusisitizia, hakuna kinachoweza kukuzuia kufanikiwa ila wewe... Continue Reading →

#TANO ZA JUMA #48 2018; Sanaa Ya Kupata Fedha, Ishinde Tabia Ya Kuahirisha, Kuwashwa Na Pesa Na Siku Inayokuridhisha.

Hongera sana rafiki yangu mpendwa kwa kulimaliza juma namba 48 la mwaka huu 2018. Naamini lilikuwa juma bora sana kwako, kwa hatua ulizoweza kupiga na matokeo uliyoyapata. Kila matokeo uliyopata ni muhimu sana kwako, matokeo mazuri yanakusogeza mbele na matokeo mabaya yanakupa funzo. Hivyo usinung’unike wala kukata tamaa kwa matokeo yoyote uliyopata, bali yatumie kupiga... Continue Reading →

SEMINA; TABIA ZA KITAJIRI; Ahadi Kumi Za Kuishi Kila Siku Ili Kufikia Utajiri Na Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha.

Rafiki yangu mpendwa, Ninayo furaha kubwa sana kukupa taarifa muhimu sana za semina yetu kubwa ya kwenda kuuanza mwaka 2019. Ni semina ambayo itakuwa na maarifa yatakayoleta ukombozi mkubwa sana kwenye maisha yako. Kwani semina hii inakwenda kugusa eneo muhimu sana kwenye maisha yako, eneo ambalo linagusa kila sehemu ya maisha yako ukiacha tu hewa... Continue Reading →

Mahitaji Makuu Manne (04) Ya Watu Ambayo Kila Mjasiriamali Anapaswa Kuyafahamu Na Kuyatimiza.

Rafiki yangu mpendwa, Mafanikio kwenye biashara na ujasiriamali hayaanzii kwako mwenyewe, bali yanaanza kwa wale ambao unawahudumia. Hii ina maana kwamba, kama unataka kufanikiwa kwenye biashara na ujasiriamali, basi unapaswa kwanza kuwawezesha wengine wafanikiwe. Biashara na ujasiriamali ni eneo ambalo halihitaji ubinafsi hata kidogo. Ni eneo ambalo linakutaka ujali kwanza kuhusu wengine kabla hujajali kuhusu... Continue Reading →

#TANO ZA JUMA #47 2018; Mawazo 151 Ya Kuongeza Mauzo, Tumia Majuto Kufanya Maamuzi Sahihi, Pesa Siyo Makaratasi Na Amini Kwenye Uzuri Wa Ndoto Zako.

Rafiki yangu mpendwa, Juma namba 47 la mwaka 2018 linakwenda kuachana na sisi, masaa 168 tuliyoyaanza mwanzoni mwa juma hili, yanakwenda kumalizika. Lakini wakati muda huu unatuacha, hatupaswi kubaki watupu, hatupaswi kuwa kama tulivyolianza juma hili. Kama tutaruhusu hilo litokee, tutakuwa tumechagua kupoteza juma letu zima. Kila juma tunapaswa kujifunza vitu vipya ambavyo hatukuwa tunavifahamu... Continue Reading →

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumia Majuto Kama Kipimo Cha Kufanya Maamuzi Bora Kwenye Maisha Yako.

Rafiki yangu mpendwa, Kitu kinachojenga au kubomoa maisha yetu, kinachofanya tufanikiwe au kushindwa, ni maamuzi ambayo tunayafanya kwenye maisha yetu. Kila siku tunafanya au kuepuka kufanya maamuzi fulani, na hayo ndiyo yametufikisha pale tulipo sasa. Hapo ulipo leo ni matokeo ya maamuzi ambayo ulifanya au kutokufanya siku zilizopita. Kwa mfano kama hapo ulipo una kipato... Continue Reading →

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑