Sikiliza hapa;

Rafiki yangu Mpendwa,

Inapokuja kwenye swala la mafanikio, kila mtu huwa ana ushauri mzuri sana. Hata wale ambao hawajafanikiwa kabisa, wanakuwa tayari kutoa ushauri kwa watu waliowazidi mafanikio.

Kitu ambacho kinashangaza ni kwa nini watu wasitumie wenyewe ushauri mzuri ambao wanakuwa wanawapa watu wengine? Jibu la swali hilo ni kitu kinachofungua ukweli kuhusu asili yetu binadamu, huwa tunajidanganya sisi wenyewe.

Kulielewa hili vizuri, chukua mfano wa mtu ambaye amepata changamoto fulani, labda msiba wa mtu wa karibu. Utampa pole na maneno mazuri ya faraja katika hicho kipindi. Lakini wewe unayetoa maneno hayo, unapokutwa na hali kama hiyo, huwezi kujiambia na hata watu wakikuambia unaona hawaelewi na hayafanyi kazi kwako.

Huo ni udhaifu ambao binadamu tunao, ambao kama hatutaujua na kuutumia vizuri, hatutaweza kupata mafanikio makubwa tunayoyataka.

Ndiyo maana kwenye hii #BaruaYaKocha tunaenda kujifunza jaribio rahisi ambalo litakusaidia kuacha kujidanganya na kujikwamisha kufanikiwa.

1. Udhaifu Wetu Wa Kushindwa Kujiona Kwa Usahihi.

Udhaifu mkubwa ambao kila binadamu anao ni upofu wa kushindwa kujione yeye mwenyewe kwa usahihi. Kuna mambo ambayo wengine wanayaona kwa wazi kabisa kuhusu sisi, lakini kwetu yanakuwa ni giza kubwa.

Hili ni tatizo kubwa, ambalo limeleta madhara makubwa sana kwa wale ambao hawajui uwepo wa tatizo hili. Kumekuwa na viongozi wengi, ambao wanakuwa na nia njema kabisa za kujenga kitu chenye manufaa. Lakini kwa kujiamini zaidi wao wenyewe na kutokuchukua mawazo ya watu wengine, wamekuwa wanaishia kuanguka vibaya.

Hakuna binadamu yeyote aliyekamilika, kila mmoja ana huu upungufu wa kushindwa kujiona yeye mwenyewe kwa usahihi. Mtu anaweza kujiona yuko sawa kwenye kila jambo, lakini wanaomzunguka wanakuwa wanaona wazi ni wapi ambapo hayupo sawa.

Kitu kikubwa cha kuondoka nacho hapa ni kukubali kwamba huwezi kujiona kwa usahihi wewe mwenyewe. Kuna mambo mengi unaweza kujiona uko sawa kabisa, lakini wengine wanaona wazi jinsi ambavyo haupo sawa.

Na kujua hili hakukulazimishi ubadili mambo makubwa, bali kunakutaka utambue ni wapi una udhaifu na jinsi ya kuuzuia usikukwamishe kupata kile unachotaka.

2. Uimara Wetu Kwenye Kuwaona Wengine Kwa Usahihi.

Inapokuja kwenye kutoa maoni, ushauri na kukosoa wengine, huwa tupo vizuri sana. Hata kama sisi wenyewe hatuwezi kufanya kile wanachofanya, huwa hatukosi maoni juu ya hicho wanachokuwa wanafanya.

Pamoja na kukosa ujuzi na uzoefu kwenye mambo ya wengine, huwa tunaweza kuwa na maoni mazuri kwa sababu hatupo kwenye kufanya kitu hicho moja kwa moja. Kama ambavyo shabiki anayeangalia mchezo anaweza kuona anapokosea mchezaji, kwa nje ni rahisi kuona vitu kwa usahihi. Lakini ukiwa ndani kunakuwa na upofu mwingi unaokuzuia kuona mambo kama yalivyo.

Huu ni uimara tunaopaswa kuujua na kuutumia kwetu wenyewe, badala ya kupeleka kwa watu ambao hawawezi kuutumia. Mara nyingi maoni, ushauri na ukosoaji unaokuwa nao kwa watu wengine huwa haupokelewi vizuri. Badala ya kupoteza rasilimali zako kwenye hilo, unaweza kutumia huu uimara kwenye kufanya mambo yako na ukapata mafanikio makubwa unayoyataka.

Endelea kusoma #BaruaYaKocha hapa; #BZK117; Fanya Jaribio Hili Ili Uache Kujidanganya Wewe Mwenyewe Na Kujizuia Kufanikiwa