Rafiki yangu mpendwa,

Karibu kwenye makala ya ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufanikiwa. Kama ambavyo nimekuwa nakuambia mara kwa mara, usiombe kutokukutana na changamoto, bali omba kuwa imara ili uweze kukabiliana na kila aina ya changamoto. Kwa sababu changamoto hazitaisha, ila kadiri unavyokuwa imara ndivyo unavyoweza kuzikabili na kushinda.

Kwenye makala ya leo nakwenda kukushauri kuhusu kujua usahihi wa biashara ya mtandao na kuepuka kutapeliwa.

Kabla hatujaangalia njia za kujua usahihi wa biashara ya mtandao, tupate maoni ya msomaji mwenzetu aliyetuandikia kuhusu hili;

Mimi pia nilishauriwa na rafiki yangu kuingia kwenye hiyo biashara ya mtandao, lakini kufika kule kitu cha bei ya chini kabisa ni saa ambayo ili niinunue na kujiunga inatakiwa tsh 5500,000/: nitampeleka nani aweze kununua? Huku mtaani sina mtaji iyo 5500,000 naipata wapi? – E. Obadia.

Rafiki, dunia ya sasa inabadilika sana, na mabadiliko mengi yanafanya maisha kuwa rahisi sana.

Kwa mfano kuingia kwenye biashara kwa zama tunazoishi sasa siyo tena kitu kigumu, kwa sababu hata kama huna mtaji mkubwa, huna sehemu ya kufanyia biashara na huna uwezo wa kusajili biashara, unaweza kuingia kwenye biashara ambayo inafanya hivyo vyote kwa ajili yako.

Kazi yako wewe ni kutumia bidhaa na ukawashawishi watu wa karibu yako nao wajiunge na biashara na kununua bidhaa hizo. Kwa watu kujiunga na biashara hiyo na kununua bidhaa au huduma zinazotolewa na biashara hiyo, wewe unalipwa sehemu ya faida ambayo kampuni inatengeneza.

Hii ndiyo biashara ya mtandao, ambayo kwa majina mengine inajulikana kama NETWORK MARKETING au MULTI LEVEL MARKETING. Ni biashara ya zama hizi ambayo ukiweza kuifanya vizuri, yaani kuchagua kampuni sahihi, kujifunza na kuweka juhudi, itakuwezesha kupiga hatua sana.

Lakini changamoto kubwa ni kwamba, karibu kila siku kuna kampuni mpya inakuja ya kufanya biashara kwa mfumo huu wa mtandao. Kuna kampuni nyingi kiasi kwamba kujua usahihi wa kila kampuni ni kazi ngumu sana. Na pia huna muda na hata fedha za kujaribu kila kampuni ili uweze kujua usahihi wake.

Hivyo hapa unahitaji kuwa na msingi wa kukuwezesha kufanya maamuzi muhimu kuhusiana na biashara unayokuwa unaambiwa ujiunge nayo.

Ili kuweza kupata uelewa mpana kuhusu biashara hii na kuepuka kuingia kwenye biashara isiyo sahihi, nimekuandikia kitabu kizuri sana kinachoitwa IJUE BIASHARA YA MTANDAO. Ni kitabu kinachoeleza biashara hii kwa kina, kinakupa sifa za kuangalia wakati unachagua kampuni na viashiria vya kampuni ambayo ni utapeli.

Nakushauri sana, na hata kukuomba, usiingie kwenye biashara yoyote ya mtandao kabla hujasoma kitabu hichi. Kitabu ni tsh elfu 5 pekee na kinatumwa kwa email, hivyo unaweza kukipata popote ulipo. Unachohitaji kufanya ni kulipa elfu tano kwa namba 0755953887 au 0717396253 kisha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizi ambao una email yako na jina la kitabu, IJUE BIASHARA YA MTANDAO na utatumiwa kitabu.

NETWORK MARKETING

Kwa kuwa mengi utayapata kwenye kitabu, hapa nikushirikishe machache kuhusu kuepuka biashara za mtandao ambazo ni utapeli.

Ukiona yafuatayo kwenye biashara yoyote ya mtandao, kaa mbali nayo, kuna utapeli zaidi kuliko biashara.

  1. Faida pekee ambayo mtu anapata kwenye biashara hiyo ni kutokana na wanachama ambao mtu anawaingiza. Faida inapaswa kutokana na manunuzi yanayofanywa na wale uliowaingiza na siyo kwa kuwaingiza pekee.
  2. Kama biashara haina bidhaa au huduma ambayo watu wanaihitaji na wanaweza kuimudu kaa nayo mbali. Hivyo kile unachotaka kuuziwa, angalia uhitaji wake na utayari wa watu kukipata na kukilipia, kama hakuna anayekihitaji, kaa mbali.
  3. Kama watu wanakuambia utatajirika haraka bila haya ya kufanya kazi, kama wanakuambia kwa miezi michache tu utakuwa tajiri mkubwa bila ya kufanya kazi kubwa, kaa mbali, kuna utapeli hapo. Biashara halisi ya mtandao unahitaji kufanya kazi sana na unahitaji muda kabla hujaanza kupata faida.
  4. Kama fedha zako inabidi umpe yule anayekuunganisha, au kama ukimuunganisha mtu inabidi fedha akupe wewe ndiyo uende kumlipia au ulipe kulingana na pointi ambazo wewe unazo ila fedha anakupa wewe, kaa mbali na biashara ya aina hiyo. kuna harufu ya utapeli hapo kuliko biashara. Hata kama malipo inabidi yafanywe nje ya nchi, kila mtu anapaswa kulipia kwenye biashara husika na siyo kulipana wenyewe kwa wenyewe.
  5. Kama biashara ni mpya na haijawa na wanachama au watumiaji wengi, siyo lazima ikawa ni utapeli, ila ni vigumu kujua. Kipimo kizuri cha usahihi wa biashara ni kwa muda gani imedumu. Kama biashara ina zaidi ya miaka miwili, na haijawahi kushukiwa kama ni utapeli basi uwezekano mkubwa hiyo ni biashara sahihi.

Rafiki yangu, ndani ya kitabu utakachosoma baada ya kulipia na kupata, utasoma sifa nyingine tano za kuepukana na utapeli, pia utajua sifa kumi za biashara zenye mafanikio na pia jinsi ya kuchagua biashara sahihi kwako.

Pata kitabu hichi sasa na ukisome ili uepuke kutapeliwa.

Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TOA CHANGAMOTO YAKO USHAURIWE

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja ya makala zijazo kila siku ya jumatatu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog