Unajua kwamba kwenye kila kitu watu wanachofanya kuingiza kipato kuna wanaolipwa zaidi ya wengine? Yaani kwa lolote lile ambalo watu wana ujuzi na wanafanya kupata fedha kuna wachache wanaolipwa zaidi ya wengine.

  Mwanafalsafa Vilfredo Pareto(15 July 1848 – 19 August 1923) aligundua sheria(Paretal Principle) kwamba asilimia 80 ya majibu inatokana na asilimia 20 ya jitihada ama watu. Ina maana kwenye sekta yoyote asilimia 80 ya mafanikio yote inaletwa na asilimia 20 ya watu waliko kwenye hivyo sekta. Kwa mfano asilimia 80 ya utajiri wa dunia nzima umechangiwa na asilimia 20 ya watu. Hata kwenye kazi unayofanya asilimia 80 ya matokeo mazuri imesababishwa na asilimia 20 ya wafanyakazi, na asilimia 80 ya mapato yote yanalipwa kwa asilimia 20. Kwa hiyo wale walioko juu ndio wenye mchango mkubwa kwenye matokeo yoyote yanayotokea walipo na ndio wanaolipwa zaidi kuliko wengine.

paretopareto2

  Je unataka kuwa ndani ya asilimia 20 ya wale wanaosababisha mambo mazuri? Na je unataka kuwa asilimia 20 juu kwenye asilimia 20 ya wanaoleta mabadiliko(20% ya 20% ni 4%). Unaweza kabisa kuwa kwenye asilimia 4 ya watu wanaosababisha matoke mazuri na wanaolipwa zaidi kwa chochote unachofanya.

  Unaweza kuwa umeshaanza kupata majibu kwamba ninachotaka kukuambia ni fanya kazi kwa bidii na maarifa na uwe na mipango na malengo ili uweze kulipwa kuliko wengine wote. Ni kweli kufanya hivyo kutakusaidia kufika huko juu ila kuna kitu kimoja ambacho hujakifikiria na wengi huwa hawakitilii maanani. Kitu hicho ni kubobea. Hakikisha kwenye jambo ama kazi yoyote unayofanya wewe ndio umebobea kuliko wengine wanaofanya unachofanya. Hakikisha wewe unafanya vitu vyako kwa utofauti mkubwa kiasi kwamba yeyote anaetaka kazi yake ifanyike kwa ustadi basi anakutafuta wewe ama anaelekezwa kwako. Hii inawezekana kwa wewe kuifanya kama ukiamua kwa maana kila mmoja wetu ana vipaji na uwezo wa pekee ambao haufanani na wengine.

  Chagua kile unachoweza kufanya kwa utofauti mkubwa na tumia muda wa kutosha kujiendeleza mpaka kuwa mtaalamu uliebobea. Kujiendeleza kwa dunia ya sasa ni uamuzi wako mwenyewe tu na sio mpaka ukasome ‘masters degree’. Ukishabobea wala haitakuwa shida kwako, badala ya kuomba watu wakupe kazi watu watakuwa wanakuomba uwafanyie kazi zao. Umewahi kuombwa umfanyie mtu kazi? Si maanishi kuombwa ufanye kwa msaada, hapana, namaanisha unaombwa kupewa fedha, yani umaombwa kulipwa!!

money chasemoney chase2

Kama hujapata nafasi hiyo ya kuombwa kulipwa basi bobea kwenye jambo unalofanya na baada ya muda watu wataanza kukukimbilia wakiomba kukulipa. Ukishafikia hatua hiyo basi wewe utakuwa mmoja kati ya watu wanaolipwa sana kwenye fani unayofanya.