Kwenye maisha ya sasa kila kunapokucha afadhali ya jana, maisha yanazidi kuwa magumu kadri siku zinavyozidi kwenda. Kazi zinakuwa ngumu, hela hazionekani na gharama za maisha zinapnda kila kukicha. Yote haya yanakufanya kuwa na mawazo sana kuhusu maisha na hata kukufikisha kwenye msongo wa mawazo. Inawezekana fedha sio tatizo kwako ila maisha ya familia, mahusiano, kazi na hata jamii kwa ujumla vikakuweka kwenye matatizo yanayopelekea kuwa na msongo wa mawazo.

kikwete stressed

  Unaweza kufikiri kwamba hakuna njia ya kuweza kuepuka msongo wa mawazo, gharama za maisha zinaendelea kupanda kila siku, kazi zinaendelea kuwa ngumu, muda hautoshi na maisha ya familia bado yanakusumbua. Una nguvu kubwa ya kuweza kundokana na msongo wa mawazo zaidi ya unavyofikiri. Kuweza kukabili msongo wa mawazo ni wewe kuchukua hatua ya kudhibiti mawazo yako, hisia zako, ratiba zako na jinsi unavyokabiliana na matatizo unayokutana nayo.

stress2

  Kijue chanzo cha msongo wa mawazo

 Kabla ya kutafuta njia za kukabiliana na msongo wa mawazo ni vyema ukajua ni nini hasa kinacholeta msongo kwenye maisha yako. Je ni kazi unayofanya, familia, mahusiano, maisha magumu ama watu fulani? Msongo wa mawazo ulionao wewe umeutengeneza kutokana na mazingira, yajue mazingira hayo ili uweze kuondokana na msongo.

 Njia za kukabili msongo wa mawazo

 Baada ya kujua chanzo cha msongo, unaweza kuukabili kwa njia zifuatazo;

1. Kuepuka msongo usio na lazima. Kuna mambo mengi yanatuletea msongo kwenye maisha yetu ila yanaweza kukabilika yani unaweza kuyaepuka. Kwa mfano kama unapata msongo kwa kuwa na kazi nyingi, unaweza kuepuka kwa kukataa kupokea kazi nyingi za kufanya ili kuweza kumaliza ulizonazo bila msongo. Kama unapata msongo kutokana na kufikia tarehe ya mwisho ya kumaliza kazi ama jambo lolote unaweza kuepuka kwa kupanga kunza kufanya mapema.

stress4

2. Badili hali ama mazingira yanayoleta msongo. Kama huwezi kuepuka msongo basi badili hali ama mazingira yanayosababisha msongo huo. Kwa mfano matatizo ya kwenye mahusiano, kunakuwa na kutoelewana kutokana na jambo fulani. Ni vyema kukaa chini na kulizungumzia jambo hilo mpaka kupata muafaka, na muda mwingine inabidi kukubaliana na jambo ulilokuwa unapinga ili kuweza kusonga mbele(kama mbele kuna faida nyingi)

3. Badilika kutokana na mazingira. Kama huwezi kubadili mazingira yanaysababisha msongo basi badilika wewe kutokana na mazingira hayo. Badala ya kujiumiza kwa jambo ambalo huwezi kulibadili ni vyema kujifunza kutumia jambo hilo kwa faida. Kwa mfano badala ya kujipa msongo kwa kuwa kwenye foleni kwa muda mrefu, tumia hiyo nafasi kama sehemu ya kujifunza. Kama up kwenye foleni hata ukafikiri vipi bado huwezi kuibadili foleni hivyo ni bora kukubaliana na hali na kisha kufanya jambo jingine wakati unasubiri kufika unapkwenda, unaweza kusoma ama kusikiliza kitabu, ama kusikiliza wimbo unaoupenda.

4. Kubali kuna mambo ama vitu huwezi kuvibadili. Chanzo kikuu cha msongo wa mawazo ni kujaribu kubadili vitu ambavyo hatuwezi kuvibadili ama vilivyo nje ya uwezo wetu. Kwa mfano ni ngumu sana kubadili tabia ya mtu(hasa watu wazima), badala ya kila siku kukasirishwa na matendo yao unaweza kuchagua jinsi ya kuguswa na matendo yao. Kubali watu wana mapungufu yao na ishi nao kwa jinsi walivyo. Pia jifunze kusamehe, itakusaidia sana kupunguza msongo wa mawazo.

5. Tenga muda wa kupumzika na kufurahia kila siku. Hata kama kazi yako ni ngumu kiasi gani hakikisha kila siku una muda wa kupumzika na kufurahia maisha. Kaa karibu na watu unaowapenda na kuwafurahia, fanya kitu unachokipenda na kukufurahisha kama michezo. Hii itakusaidia sana kuondokana na msongo wa mawazo.

stress3

6. Jenga afya yako. Ni rahisi sana kukabiliana na msongo wa mawazo kama utakuwa na afya njema. Fanya mazoezi ya viungo, kula mlo kamili, epuka vileo na madawa ya kulevya, kunywa maji ya kutosha na pata usingizi wa kutosha.

  Matatizo mengi ya kiafya yanayotukumba binadamu yanatokana ama yanazidishwa na msongo wa mawazo. Unaweza kusema matatizo yanaleta msongo wa mawazo ila msongo wa mawazo ndio unaoleta na kuzidisha matatizo. Epuka ama kabiliana na msongo wa mawazo ili uweze kuwa na maisha yenye furaha.