Wengi tunaposikia neno mafanikio akili yetu moja kwa moja inakwenda kwenye majumba na magari ya kifahari, vyeo vya kikazi na mengine mengi ambayo watu wakiyaona wanaona mwenye nayo kafanikiwa. Kwa mtazamo huo mafanikio yanaonekana ni kuwa na fedha nyingi ili kuweza kumiliki vyote hivyo vinavyoonekana ni vya waliofanikiwa. Kwa kuwa tunapima mafanikio kwa fedha, inalazimu watu kufanya kazi nyingi na kwa muda mwingi ili kupata fedha hizo nyingi, kupata vyeo na heshima kwenye jamii.

MAFANIKMAFANIKIO

  Kwa kipimo hicho cha mafanikio tutakuwa tumefanikiwa pale tu watu wengine watapoona tumefanikiwa. Yaani wewe kama wewe huwezi kujiona umefanikiwa mpaka watu watakapoanza kukuzungumzia wewe, ama utapopata cheo kikubwa. Ili kuweza kufikia mafanikio hayo wengi wanafanya kazi kupitiliza, wanachoka sana na wengi wanaishia kupata msongo wa mawazo hasa pale wanapokuwa wamefanya kila njia ila bado hawajaonekana kufanikiwa.

  Mafanikio yanafananaje hasa?

  Mafanikio yanafanana na wewe, mafanikio ni wewe pale unapfanya lile ulilothamiria kulifanya na ukafanikiwa kulifanya. Mafanikio ni pale unapofanya vizuri kwenye kitu ambacho umebobea. Tukiweza kuyapima mafanikio kutokea ndani ya nafsi zetu maisha yatakuwa ya furaha sana.

  Tumia kipaji cha pekee ulichonacho kuisaidia dunia, fanya kitu fulani kwenye jamii inayokuzunguka, fanya kile ambacho unafurahia kufanya na hapo utakuwa umefanikiwa.

  Usifanye kwa kutaka kuonekana fanya kwa bidii hata kama hakuna anaekuona, kuwa wewe kama wewe na fanya kwa kipaji chako chote. Kwa njia hii utafikia mafanikio ya ndani ya nafsi yako na kuyafurahia maisha.

  Ubaya wa kupima mafanikio kutokana na vitu mtu anavyomiliki ni kwamba inamkatisha tamaa ambae hana vitu hivyo. Kuna watu wanafanya mambo mazuri sana na kwa kiwango cha hali ya juu ila kwa vile hawana vinavyonekana kama mafanikio basi hakuna anaeona wamefanikiwa. Na vibaya zaidi na wao wanakubali kwamba hawajafanikiwa hivyo wanashindwa kupata msukumo wa kuendelea kufanya mambo mazuri wanayofanya.

mafanikio1

  Usitumie muda mwingi kufikiria juu ya mafaniki ya vitu, bali tumia muda mwingi kufikiria jinsi ya kuyafurahia maisha kwa kile unachopenda kufanya.