JE WEWE NI BAHARIA AMA ABIRIA?

  Umepanda meli na humo kwenye meli mpo watu wengi baadhi ni abiria tu wanaosafirishwa na wengine ni sehemu ya mabaharia wanaohakikisha meli inafika inakoelekea. Ghafla hali ya bahari inabadilika na meli inayumba sana na ili kuweza kuendelea na safari inabidi baadhi ya watu watoswe majini ili kupunguza uzito. Unafikiri ni watu gani watakaotoswa majini? Abiria ama baharia?

  Sote tunakubali kwamba watakaotoswa majini ni abiria. Hakuna anaeweza hata kufikiria kwamba baharia atoswe majini. Kwa nini baharia asitoswe na abiria wengine waweze kutoswa? Wote si ni binadamu sawa? Katika hali kama hiyo kinachojalisha sio ubinadamu bali umuhimu. Baharia anaachwa kwa sababu yeye ni wa muhimu kwenye chombo kuliko abiria wa kawaida.
  Jiulize wewe je kwenye meli uliyopanda wewe ni abiria wa kawaida ama sehemu ya mabaharia?
  Kwenye maisha yako kuna meli nyingi ulizopanda, baadhi ya meli hizo ni ajira, na nafasi mbali mbali kwenye jamii.
  Kwa mfano kwenye ajira kama kampuni ama shirika unalofanya kazi likipata msukosuko na kuhitaji kupunguza wafanyakazi watakaoanza kupunguzwa ni wale ambao hawana umuhimu mkubwa kwa shirika. Yaani watapunguzwa wale ambao ni mzigo, ambao hata wasipokuwepo hakuwezi kuwa na athari kubwa sana.

  Jitafakari kwenye ajira yako wewe ni baharia ama abiria? Je kuna kipi cha muhimu sana ambacho kampuni ama shirika linapata kutoka kwako. Je ni rahisi tu kwa wewe kupunguzwa ama kufukuzwa?
  Sio lazima uwe mkurugenzi ama injinia mkuu ndio uwe wa muhimu sana kwenye sehemu yako ya kazi. Hata kama wewe ni mfanya usafi tu unaweza kuamua kuwa wa muhimu sana kiasi kwamba sio rahisi kwa wewe kuondolewa. Kwa sababu hata wapunguzwe wafanyakazi kwa asilimia 70 bado lazima atabakishwa mfanya usafi japo mmoja. Unafikiri kitatumika kigezo gani kumbakisha huyo mmoja?
  Kwenye kitengo chochote unachofanya kazi unaweza kuwa wa muhimu sana na kufanya iwe ngumu kuondolewa kirahisi.
  Ili uwe wa muhimu ni lazima kile unachofanya ufanye kwa utofauti na kwa kiwango cha hali ya juu. Ni rahisi kwako kuweza kufanya hivyo kama utatumia uwezo na vipaji vya pekee ulivyonavyo.
  Hakikisha chochote unachofanya unaleta mabadiliko kwako na kwa wanaokuzunguka. Mabadiliko hayo yatakufanya uwe wa pekee na kuwa wa muhimu kwenye kazi unayofanya.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: