Unaamka asubuhi unaelekea kwenye shughuli zako, unafanya kazi, unarudi nyumbani, unapumzika na kuangalia tv ama kuingia kwenye mitandao ya kijamii, unakula, unaenda kulala. Kesho tena unafanya hivyo hivyo na unarudia hivyo kwa sehemu kubwa ya maisha yako.

routine5routine2

  Kwenye maisha yako kuna vitu unavifanya mara kwa mara na unavifanya kwa mbinu na mtindo ule ule kila mara. Inaweza kuwa kwenye maisha ya kawaida, kwenye kazi ama hata jinsi ya kufikiri.

routine

  Ni vizuri kuwa na utaratibu ama mpangilio wa maisha ila haimaanishi maisha yawe kama amri isiyobadilishwa. Kuishi maisha yale yale kwa kufanya vitu vile vile kia siku inapunguza uwezo wa kufkiri na ugunduzi.

  Ni vigumu sana kupata mawazo mapya ama kugundua kitu kipya kwa kufanya yale yale unayofanya kila siku na kwa mtindo ule ule unaofanyia.

  Pia kufanya mambo mara kwa mara kwa njia moja tu ni chanzo mojawapo cha msongo wa mawazo.

routine4

Baadhi ya mambo unayoweza kuyabadili leo na uanze kufurahia maisha ni haya;

  Kama kila siku unakwenda kwenye shughuli zako kwa kupita njia moja basi leo jaribu kupita njia tofauti. Hakikisha unapita njia tofauti tofauti kila siku kwa sababu unavyoviona vinaweza kubadili mtizamo wako. Kama unaona vile vile kila siku hata mtizamo wako unakuwa vile vile.

  Kama huwa unakwenda kwenye shughuli zako za kila siku kwa kutumia usafiri wako binafsi siku moja moja panda usafiri wa jumuia(daladala). Kuna mengi sana utajifunza humo ambayo ni vigumu sana kuyapata ukiwa kwenye gari lako mwenyewe.

daladalagari

  Kama unafanya kazi ofisini na unakaa meza ile ile na kiti kiko sehemu ile ile kila siku leo badili hata mpangilio wa kiti. Kwa kukaa tu tofauti na kila siku unavyokaa kunachochea kutafakari kwa utofauti.

  Angalia njia tofauti unayoweza kufanya kazi yako ama kutoa huduma yako. Kwa kuwa na utofauti kutakufanya uifurahie kazi yako na hata wale unaowafanyia kazi ama kuwapa huduma watafurahishwa pia.

Binadamu hatupaswi kuwa kama ‘robot’ lazima tuyabadili mazingira yanayotuzunguka ile tuweze kuwa na furaha na pia kuwa wabunifu. Jitahidi kubadili kila unachoona kinaweza kubadilika kwenye maisha yako.