Kuna mijadala mingi kuhusu nani anaweza kuwa mjasiriamali na kuweza kufanikiwa. Kuna wanaosema wajasiriamali huzaliwa na wengine wanasema wajasiriamali wanatengenezwa.

  Wanaosema wajasiriamali wanazaliwa wanaamini kwamba tabia za kijasiriamali mtu anazaliwa nazo na wala sio kujifunza. Wanaamini kwamba kwa wanaoingia kwenye ujasiriamali na kushindwa ni kwa sababu hawajazaliwa na tabia ya ujasiriamali. Kwamba hata wakikazana kwa kiasi gani bado hawana kile kinachohitajika ili kufanikiwa kwenye ujasiriamali.

mjasiriamali

  Kwa wanaosema wajasiriamali wanatengenezwa, wanaamini mtu anaweza kufundishwa na kuwa mjasiriamali. Wanaamini mtu akipewa mafunzo mazuri ya ujasiriamali anaweza kuwa mjasiriamali mzuri na kufanikiwa sana.

mjasiriamali2

  Kabla ya kusema moja kwa moja ni wazo lipi hapo ni sahihi na ni lipi hapo sio sahihi kwanza tuangaie tabia za binadamu kiujumla na tabia za wajasiriamai.

  Mjasiriamali ni mtu anaejiamini, mwenye ndoto na mwenye ujasiri wa hali ya juu.

  Kuweza kuanza ujasiriamali kunahitaji kujiamini kwa hali ya juu na kuweza kufanya mambo ya hatari(kutake risk) kunahitaji ujasiri mkubwa. Na ili aweze kundelea mbele licha ya matatizo unayokumbana nayo ni lazima mjasiriamai awe na ndoto na maengo makubwa aliyojiwekea.

  Tabia hizo tatu kuu za ujasiriamali hakuna anaezaliwa nazo ila tunazipata kutoka kwenye mazingira tunayokulia na tunayoishi mara nyingi.

  Mtoto aliekulia kwenye familia ama jamii inayomjengea kujiamini moja kwa moja naye atajiamini. Mtoto aliekulia kwenye jamii ya watu wanaotake risk moja kwa moja nae atajenga tabia hiyo. Kwa kifupi tabia zinaambukizwa. Ndio maana unaweza kuona baadhi ya makabila ni wafanya biashara maarufu wakati kuna baadhi ya makabila wanapenda kazi ndogondogo.

  Sio kwamba kuna mbegu moja kwenye kabila fulani na mbegu nyingine kwenye kabila jingine, hapana, kinachotokea ni kuambukizana tabia. Kumbuka wanaokuzunguka wana mchango mkubwa sana wa hapo ulipofikia.

  Hivyo basi kuchukulia uambukizano huu wa tabia kama tabia za kuzaliwa tunaweza kujumuisha kwamba wajasiriamali huzaliwa. Je hii ina maana kama mtu hajakaa kwenye mazingira yanayoweza kumuambukiza tabia hizo hawezi kuwa mjasiriamali?

  Mtu yeyote, narudia tena yeyote anaweza kuwa mjasiriamali kama tu atafanya MAAMUZI. Kikubwa kinachopima kufanikiwa ama kutofanikiwa kwa mjasiriamali ni maamuzi. Mtu yeyote anaeamua kwa moyo mmoja kwamba maisha yake sasa ni ujasiriamali na hakuna kitakachomtoa kwenye maisha hayo anauwezekano mkubwa sana wa kufanikiwa katika ujasiriamali.

  Mtu akishafanya maamuzi thabiti moja kwa moja ataanza kutafuta njia za kufanikiwa kwenye ujasiriamali na hapo ndipo atajifunza tabia za kuweka ndoto na maengo makubwa, ujasiri, kujiamini na kufanya mambo ya hatari.

  Tusiubeze uwezo wa akili na maamuzi ya binadamu, binadamu anauwezo mkubwa sana wa kufanya chochote anachoweza kukifikiria kwenye akili yake.

mjasiriamali3

  Fanya maamuzi sasa ya kuwa mjasiriamali na uyamiliki maisha yako. Usiogopeshwe na waliokuzunguka ama historia ya familia yako. Wewe ni wa pekee na una uwezo mkubwa sana wa kueta mabadiliko. Ukifanya maamuzi ambayo hayatetereki lazima utafikia ndoto na maengo yako. Hakuna anaekujua wewe zaidi ya wewe mwenyewe. Tumia uwezo na vipaji vyako kuleta mabadiliko kwako na kwa jamii inayokuzunguka.