Blog yako AMKA MTANZANIA imepata mafanikio makubwa sana kwa mwaka 2013. Na mafanikio hayo yameletwa na wewe msomaji mzuri wa blog hii. Watu wengi wamejifunza na wengi wameanza kuyabadili maisha yao kwa kuhamasishwa na makala mbalimbali zinazopatikana kwenye blog hii.
Kwa mengi zaidi juu ya mafanikio ya blog yako mwaka 2013 soma; Shukrani nyingi kwako mtanzania uliyeamka.
Mpaka kufikia terehe 31/12/2013 blog ina makala 193, zote ni makala nzuri na wasomaji wengi wamekuwa wakitoa mrejesho chanya wa jinsi makala hivyo zilivyowasaidia.
Katika makala hizo nyingi kuna makala 10 ambazo zimesomwa sana kupita makala nyingine. Sijajua sababu kuu ya makala hizi kusomwa kuliko nyingine ila ujumbe unaopatikana kwenye makala hizi umewagusa wengi katika nyanja mbalimbali.
Huenda hukupata nafasi ya kuzisoma makala hizi, ama huenda ulikuwa hujaijua blog hii wakati makala hizo zimetoka. Leo nakupa nafasi ya kuzipitia makala hizo kumi hapa ili uweze kupata ujumbe mzuri uliopo kwenye makala hizo. Kama ulizisoma makala hizi sio vibaya ukachukua muda kidogo na kuzisoma tena ili kujifunza zaidi.
Hizi ndizo makala kumi zilizosomwa zaidi mwaka 2013 kwenye blog yako ya AMKA MTANZANIA. Bonyeza ili kusoma.
10. Hii ndio sababu kuu ya wewe kushindwa kuondoka kwenye ajira
09. Hivi ndivyo unavyokufa na miaka 35 na kuzikwa na miaka 65.
08. Wajue watu hawa na waepuke kwenye maisha yako
07. Kabla hujaanza kuzunguka na bahasha soma hapa
06. Fursa tano zinazopatikana kwenye ajira ukiacha mshahara
05. Hiki ndicho unachotakiwa kufanya kila siku ili ufanikiwe.
04. Saa moja ya maajabu maishani mwako
03. Kama unaweza kupata kitu hiki kila siku basi unaweza kupata chochote unachotaka maishani.
02. Hii hapa ndio biashara inayolipa.
01. Kama una tabia hii usijaribu kujiajiri kabla hujaibadili
Hizo ndizo makala 10 zilizosomwa sana mwaka 2013. Washirikishe wengine ili nao wapate mambo haya mazuri.
Nakutakia kila la kheri kwa mwaka 2014 uwe mwaka wa mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Endelea kutembelea blog yako AMKA MTANZANIA ili uendelee kujifunza na kujihamasisha kila siku. Mwaka 2014 kuna mambo mengi mazuri sana yatakujia kupitia blog hii.