Watu Hawa Wanakurudisha Nyuma, Kuwa Makini Nao.

  Katika mafunzo ya semina ya jinsi kuweka malengo makubwa utakayoyafikia nilisema kwamba ILI UPATE KITU AMBACHO HUJAWAHI KUPATA NI LAZIMA UWE MTU AMBAE HUJAWAHI KUWA. Huu ndio ukweli wa kwanza mchungu unaotakiwa kujua kuhusu mafanikio.

  Huwezi kubadili maisha yako kwa kuendelea kuishi unavyoishi. Huwezi kupanga malengo makubwa na ukayafikia kwa kuendelea na maisha hayo unayoishi sasa hivi ambayo hujawahi kufikia malengo hayo. Mipango yote mikubwa inaanza na wewe kubadilika kwa kiasi kikubwa. Hakuna kinachoweza kubadilika kama wewe hutobadilika.

           KATAA

  Kwa kujua hilo huenda umeshaamua kubadilika ili kuweza kufikia malengo makubwa uliyojiwekea. Au umeamua kubadilika ili kubadili maisha yako kwa kiasi fulani. Kuna watu wanaweza kukusababisha ushindwe kufikia mabadiliko ya kweli na kuweza kufanya mambo makubwa.

  Inawezekana hii sio mara yako ya kwanza kutamani kufanya mabadiliko kwenye maisha yako. Huenda umewahi kupanga kubadili maisha yako ila baada ya muda ukashindwa kufanya hivyo. Umejaribu kufanya kila njia ili ubadilike lakini baada ya muda unajikuta unarudi kwenye mambo yale yale ya zamani.

  Kama unapitia wakati huo mgumu waangalie watu walioko karibu yako. Waangalie marafiki zako na watu ambao unakuwa nao muda wako mwingi. Watu hawa wanamchango mkubwa sana wa hapo ulipo.(soma; wanaokuzunguka wana mchango mkubwa kwako)

  Kama ukichunguza kwa makini utajikuta maisha yako na ya wale ambao unakuwa nao muda mwingi hayana tofauti kubwa. Kama ni maendeleo wote mtakuwa hamtofautiani sana na mtazamo wenu kwenye maisha mara nyingi unakuwa sawa. Kama ni kulalamikia maisha magumu wote mnakuwa sawa na kama ni kukata tamaa pia hamtofautiani. Hii sio bahati mbaya, ndivyo ilivyo kwamba mafanikio yetu ni wastani wa watu watano tunaokuwa nao muda wetu mwingi.

  Hivyo kama unashindwa kufanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yako licha ya kujipanga sana hebu angalia kwanza wale ambao wanakuzunguka. Kama wao hawana mipango mikubwa kwenye maisha yao basi wewe unapoteza muda, maana hutofikia mipango yako.

  Kwa kuwa watu hawa wako karibu sana na wewe ni rahisi sana kuigana tabia hasa ile inayofanywa na wengi. Ni rahisi sana kukukatisha tamaa pale unapofanya jambo la tofauti na pia ni rahisi sana kwa wewe kukubaliana nao pale wanapotoa maoni yao. Watu hawa wanaweza kuwa kikwazo kikubwa sana kwako kufikia malengo yako makubwa.(soma; wajue watu hawa na waepuke kwenye maisha yako)

 Ufanye nini kama marafiki zako wa karibu ni kikwazo kwenye malengo yako?

  Kama marafiki zako wa muhimu sana kwenye maisha wanakuwa kikwazo kwa wewe kufikia mafanikio makubwa una mambo mawili unayoweza kufanya ili kujisaidia katika hali hii.

1. Wavute nao waone umuhimu wa kubadili maisha yao. Kama unaweza kuwashawishi nao wakawa na ndoto kubwa kwenye maisha yao mtaenda sawa katika maisha yenu ya kila siku. Ila hii ni kazi ngumu inayohitaji ushawishi kutegemeana na aina ya marafiki ulioko nao.

2. Punguza muda unaokaa nao na tafuta watu wenye malengo makubwa na maisha yao na uanze kukaa nao karibu. Najua ni marafiki zako wa karibu sana na mmetoka mbali sana ila kama wanakuwa kikwazo kwako kufikia ndoto zako kubwa hakuna haja ya kuendelea kupoteza muda mwingi kwao. Sikuambii ugombane nao, hapana, punguza muda unaokuwa nao kwa sababu unapokuwa nao muda mwingi ndivyo wanavyokupandikiza mawazo yasiyo na maana ama ndivyo wanavyozidi kukukatisha tamaa.

  Ni vyema ufike mahali na uanze kuangalia mchango wa kila mtu anayekuzunguka. Kama mtu ana mtizamo hasi na mara nyingi ni mtu wa kukatisha tamaa ni vyema ukakaa nae mbali maana ni rahisi sana kuambukizwa tabia hizo. Usimchukie mtu yeyote bali tumia muda mwingi kuwa na watu ambao mna malengo makubwa na maisha yenu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s